Rais Samia apandisha kiwango cha Posho ya Kujikimu ya Safari za Ndani ya Nchi na Malipo ya Kazi Maalum kwa Watumishi wa Umma

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,518
Perdiem.
Tsh
250k , 220k,170k,150k
kwa Jiji

200k,180k,150,130k
kwa Manispaa

130k,120k,100k, 80k
kwa Halmashauri

Extra duty per day ni Tsh.60,000.0 Maafisa, 40,000.00 watumishi wengine, 30,000.00 wahudumu madereva.

Hapo unaongezea 23.5% ya lile jambo lenu

Wastaafu kulamba 33% pensheni na monthly ya 67% kwa miaka 12.5 tu.

Habari kamili tukutane July Mosi.

Updates
=======++++===========
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN APANDISHA KIWANGO CHA POSHO YA KUJIKIMU YA SAFARI ZA NDANI YA NCHI NA MALIPO YA KAZI MAALUM KWA WATUMISHI WA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuupiga mwingi kwa kutoa kibali cha kurekebisha posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma na kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi wa Umma nchini ambapo utekelezaji wake unaanza rasmi tarehe 01 Julai, 2022.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro jijini Dodoma wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma chenye lengo la kutathmini utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Ndumbaro amesema kutokana na kibali hicho cha Mhe. Rais, posho ya kujikimu ya safari za ndani ya nchi kwa Watumishi wa Umma kwa kiwango cha juu imepanda kutoka shilingi 120,000/= hadi 250,000/= na kiwango cha chini kutoka shilingi 80,000 hadi 100,000/=.

Ameongeza kuwa, kiwango cha malipo ya kazi maalum (Extra Duty) kwa Watumishi wa Umma kimeongezeka kwa ngazi zote, ambapo kwa ngazi ya chini kimepanda kutoka shilingi 15,000/= hadi 30,000/=, kwa ngazi ya kati kimeongezeka kutoka shilingi 20,000/= hadi 40,000/= na kwa ngazi ya juu kimeongezeka kutoka shilingi 30,000 hadi 60,000/=.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, viwango hivyo vipya vitalipwa na Serikali kupitia bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, hivyo taasisi zisiombe nyongeza ya bajeti ili kuwalipa viwango hivyo watumishi wake.

Kufuatia ongezeko hilo, Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini kufanya kazi kwa bidii, maarifa, weledi na nidhamu ya hali ya juu ili kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Mhe. Rais za kuboresha masilahi wa Watumishi wa Umma.

“Watumishi wa Umma tuwajibike kwa hiari bila kushurutishwa, tuwe wabunifu zaidi ili kutoa mchango katika maendeleo ya taifa na ustawi wa nchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunatatua kero zinazowakabili wananchi,” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.
 
Back
Top Bottom