Pepo la kuoa kwa mkumbo linaelekea kunishinda nguvu, maombi yenu wapendwa na wenye kujali

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,330
26,601
Amani iwe kwenu.

Kwanza kabisa ilaaniwe JF kwa kunivurugia mtazamo wangu juu ya ndoa, nimekua nikiamini ndoa ni kitu chema na hatua muhimu kuelekea mafanikio kimaisha.

Ila tangu nijiunge na familia kivuli hii, imekuwa kimbilio na chanzo cha maarifa mengi na ya kuaminika. Naamini kuwa akili ya kuambiwa nichanganye na ya kwangu, ila bado nguvu hasi ya JF kuhusu ndoa imekula kichwa changu na kuharibu mustakbali wa maisha yangu.

Awali niliamini katika kuoa singo mama nikiamini katika uzoefu wao na maumbile halisi baada ya kujifungua, hofu yangu ilikuwa kuoa mwali kisha umbo lake kuharibika mno kwa uzazi na kupoteza mvuto, kwamba singo mama tayari alikuwa na mwonekano wa ‘kudumu’.

Ila mambo yamepinduka humu kila siku ni tahadhari na vitisho kukandiwa hawa viumbe, hii sio singo mama tu bali ndoa kwa ujumla zimekuwa zikipigwa vita sana. Basi nami siishi dunia ya pekee nikawa nafuata mapigo ya ngoma, taratibu mziki umenikolea nikaanza kuucheza mazima.

Umri sio miaka, na nyakati sio milele, ghafla washkaji zangu wanaenea ndoani, utasema wao sio wanachama wa JF kumbe huenda ndo wakandiaji hodari wa ndoa nyuma ya keyboard zao.

Nina mtoto mmoja nilimpata enzi za ujana, hii pia ilichangia kujiona nimeyapatia maisha na sina cha kuharakia. Mtoto sasa ni mkubwa na huenda ana akili kuliko baba yake, katika presha zote ni hii ambayo mtoto wangu mwenyewe amediriki kunihoji “Baba unaoa lini..?”

Ni swali ambalo limekuwa si geni kwangu kutoka kwa jamii yangu kwa wanaodhani nimekwiva kumudu familia, ila kutoka kwa kinywa cha mwanangu lilinipa uzito wa kipekee, nikajisemea kwa vile ametoka likizo [kwa mama yake ambaye ameolewa na kupata watoto wengine] huenda ‘katumwa’ hilo swali kutoka upande huo.

Nilizugazuga bila majibu ya kueleweka ila kichwani limeniingia, ghafla nimeanza tabia ya ajabu ya kumtamani kila mwanamke mjamzito.

Nimekuwa nikiwaona hawa viumbe napandwa na wivu haswa na tamaa ya kuwa kwanini ‘isiwe yangu’ hii mimba, mabinti wawili wamezinyofoa ‘zangu’ hapa kati baada ya kuwapa ukweli kuwa sijawa tayari kuwaoa [kwa vipindi tofauti].

Na hata sasa kuna binti mmoja ‘anayo’ kama ya mwezi hivi, naye amekazana kushnikiza ajue kauli yangu kama nitampa ndoa. Sijajua uamuzi wake nikisema siko tayari, ila kiukweli huyu yuko mbali mno na mstari wa viwango hivyo naona ikinyofolewa tena.

Umri umesogea na hata wategemezi wangu wanaona nimekwiva na nimechelewa, najikuta naanza kubadili mitazamo hasi juu ya ndoa japo ukweli utabaki kuwa sintobadili ukweli ulivyo ndoani.... ila msukumo wa kuingia huko umenizidia pamoja na kujua fika kuna moto.

Wajameni yamenifika hapa, najiona punde naingia upande niliokuwa nikiubeza kwa miaka kadhaa, natamani maneno japo machache yenye tija yachagize uchanya wa hatua hii ambayo punde tu nitalazimika kuivagaa.

Ningetamani kikombe kiniepuke, nimekwepa nilivyoweza ila kwa wimbi hili sioni pa kutokea ni suala la muda tu.... hebu nipeni faraja au mbinu za kuukabili ukweli huu mchungu.

Natanguliza shukrani wakuu.
 
Ningetamani kikombe kiniepuke, nimekwepa nilivyoweza ila kwa wimbi hili sioni pa kutokea ni suala la muda tu.... hebu nipeni faraja au mbinu za kuukabili ukweli huu mchungu.
Mkuu "sio vyema mtu huyo awe peke yake" hii issue ni unkwepable....

Badili mtazamo wako kwanza na uone ndoa ni mpango wa Mungu.
Tulia kwa Imani yako, badili Tania na mwenendo wako, tafuta kusudi la muumba wako la wewe kuingia kwenye hiyo ndoa,ukifaulu hapa atakuomgoza mahali sahihi pa kupata msaidizi wa kulitimiza Hilo kusudi.

Changamoto hazitakosekana lakini utazivuka na zitasimama kwa ajili ya kukenga na kukufundisha pengine ama kukuongezea ujasiri lakini hazitaharibu kamwe kwasababu alichokiunganisha Mungu kamwe hakivunjwi na yeyote isipokua yeye mwenyewe....
 
Mtazamo wangu ndoa ni mpango Wa Mungu ila wanaume tumepewa jukumu zito la kuishi kwa akili na hawa viumbe,,ushauri wangu chagua mtu sahihi ambaye mnasikilizana vzurii kwenye mazurii na mabaya,,maana changamoto kubwa siku hizi ni wanandoa kutokusikilizana kila mmoja anataka kuwa juu ya mwenzie,,,,utulivu wa mtu sahihi ni muhimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Listen son, you're struggling from social conformity stop harbouring in that naivety. The modern marriage is a female institution. The man draws absolutely no benefit from it. Utakua unajitolea tu zaidi, you'll sacrifice your freedom, your ambitions, your hobbies, your future, your health, your friends and family in some instances, the list goes on and on.

I have to admit most women are smarter than men when it comes to dating or marriage, it was a textbook operation by the lady - well calculated. I'm pro marriage though, kama umeamua kuingia hakikisha you're in full aware and sober mind kwa nilichoandika aya ya kwanza. They say happy wife, happy life. Nothing rhymes with husband.
 
Mleta mada analalamika hataki ndoa kwenye paragraph moja, then analilia ndoa kwenye paragraph nyingine. Au mimi ndio nazeeka?

Sitaki ndoa ni moja ya msimamo kwa wakati fulani niliopitia, kulilia ndoa kwa sasa ni kwa shinikizo kama nilivyoeleza.... hoja ni kwamba nguvu ya mkumbo inaelekea kunishinda hivyo nishauri niikabili au niikubali kwa namna gani?
 
Mkuu we ingia tu kwenye maisha ya ndoa mbona wengine tupo ndoani na tunapambana na changamoto sote kabla tuliogopa tukaamua kuyavulia maji na tukayaoga na maisha yanaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app

Yaliyomo yamo..?

Inanilazimu kuingia ili kukidhi matarajio fulani, naingia nikiwa na mtazamo hasi ni kama najipalia mkaa.... nitawezaje kuigiza ili maisha yaendelee..?
 
Mkuu kama kweli unataka kuoa, nenda kakae na watu waliofanikiwa katika ndoa zao watakupa mawaidha muafaka.

Baadhi yetu humu ndoa zimetushinda wala hatutakupa ushauri wa maana.

Asante mkuu, “wengi wetu” humu walioshindwa ndoa si ndo wamefanikiwa kuniharibia mtazamo wangu juu ya ndoa.... sasa napambana kumkabili ‘adui’ ambaye taarifa zake nilizonazo ni zile nyingi za kutisha.

Hao wa mtaani waliofanikiwa watanishauri mbinu zao, au pengine watakiri wamebahatisha tu pamoja na kuwa hata wao wanaamini ugumu wake.... je hii itafanya ‘nipuuze’ ukweli mchungu ambao nimekuwa nikijifunza JF..?
 
Mtazamo wangu ndoa ni mpango Wa Mungu ila wanaume tumepewa jukumu zito la kuishi kwa akili na hawa viumbe,,ushauri wangu chagua mtu sahihi ambaye mnasikilizana vzurii kwenye mazurii na mabaya,,maana changamoto kubwa siku hizi ni wanandoa kutokusikilizana kila mmoja anataka kuwa juu ya mwenzie,,,,utulivu wa mtu sahihi ni muhimu

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante sana mkuu, maelezo na ushauri wako vimeegemea katika utilifu sana.... ndoa ilipaswa kuwa hivyo lakini je ni rahisi kiasi gani kuuishi utimilifu huo..?
 
Listen son, you're struggling from social conformity stop harbouring in that naivety. The modern marriage is a female institution. The man draws absolutely no benefit from it. Utakua unajitolea tu zaidi, you'll sacrifice your freedom, your ambitions, your hobbies, your future, your health, your friends and family in some instances, the list goes on and on.

I have to admit most women are smarter than men when it comes to dating or marriage, it was a textbook operation by the lady - well calculated. I'm pro marriage though, kama umeamua kuingia hakikisha you're in full aware and sober mind kwa nilichoandika aya ya kwanza. They say happy wife, happy life. Nothing rhymes with husband.

Wewe jamaa umezidi kuwa mwiba mkali, umekuwa ukigongelea misumari ya moto sana when it comes to marriage life.... nikiri tu wewe ni mmoja wa watu mliochangia kunivuruga.

Your first para ni full of naked bitter truth, asante mkuu.
 
Hapa watakwambia oa!!

Siku ukija na uzi "simuelewi wife" watakwambia "PIGA CHINI HUYO SHETANI"

MB; ndoa ni ziada tu mkuu kimbembe ni wakuingia nae humo!

Sent using Jamii Forums mobile app

Watakuja hapa kina Joh Doe et al watasema “Marriage is a life sentence jail where rivals do share a single room and bed, so choose your partner prisoner wisely”.
 
Back
Top Bottom