Pepo la baba mwenye nyumba lagoma kutoka, ahama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pepo la baba mwenye nyumba lagoma kutoka, ahama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 17, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]HATIMAYE maombi yaliyofanywa na msichana mmoja akishirikiana na waumini wenzake kumuondoa pepo chafu baba m,wenye nyumba ili asihame kwenye nyumba hiyo lagoma kutoka na ahama[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Msichana huyo juzi alionekana akihamsiha vitu vyake kwenye chumba alichokuwa amepanga baada ya mmiliki wa nyumba hiyo kumtaka ahame kwa kuwa alikuwa akikiuka maagizo aliyompa awali ya kutowasumbua wapangaji wenzake

  Msichana huyo awali alimuomba mmiliki wa nyumba hiyo asimuhamishe kwa kuwa alivutiwa na nyumba hiyo na nyumba hiyo ilikuwa jirani na alipokuwa akisali bila kutumia gharama ya nauli ya mabasi ya kila siku

  Hata hivyo ombi hilo liligonga mwamba na alichukua uamuzi wa kumfanyia maombi kuondoa pepo chafu lakini maombi hayo yalionekana kugonga mwamba na kuonekana pepo hilo kukataa kuondoka kwa mmiliki huyo na kuendelea kusimamia msimamao wake wa kumtaka aondoke

  Hivyo juzi msichana huyo alionekana kuhamisha mali zake akisaidiwa na waumini wenzake na alihamia sehemu ambayo haijafahamika mara moja

  Awali msichana huyo alikuwa akiendesha maombi katika moja ya chumba alichopanga katika nyumba hiyo na kusababisha upotevu wa amani ka kusababisha kelele endelevu katika nyumba hiyo na kuwasumbua wapangaji wengine waliokuwa wamepanga katika nyumba hiyo

  Hata hivyo ilidaiwa mmilikiwa nyumba hiyo alimtaka msichana huyo akifanya maombi afanye tahadhari asisumbue wenzake lakini ilishindikana na kuendeleza maombi hayo na waumini wenzake hata usiku jambo ambalo lilishindwa kuvumuliwa na wapangaji wenzake[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...