Pepo/jini hawezi kutoka bila kumtafutia makazi salama

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,905
6,689
Kuna wakati Mitume wa mungu aliwahi kuwaamuru mapepo wamtoke mtu waliokuwa wameweka makazi kwake..

Wakamuuliza tukitoka tutaenda wapi? Akawaamuru waende kuingia kwenye kundi la nguruwe... Nao kwa kasi ya ajabu wakawaingia wale nguruwe na nguruwe nao wakakimbilia baharini....

Huko hawakupona, walikufa wote na mapepo yale yakabaki yakitangatanga bila kikao maalum... Yaliingizwa mkenge na Mtume... Mapepo na majini ni viumbe roho hivyo havikai kwenye mwili mfu...

Mapepo na majini yale yaliyowaingia wale kundi la nguruwe wameendelea kuwepo wakitangatanga huko na kule wakitafuta hifadhi kwenye miili ya wanadamu........

Lakini sasa wame elimika huwezi kuwaingiza mkenge tena.

Mitume na manabii wengi wakiwepo waombaji wengine wenye karama na vipawa vya kuombea huwa wanakosea padogo sana...

Kuwaamuru mapepo na majini yamtoke mtu walimoweka kikao bila kuwaambia waende wapi... Nao kwa kulitambua hili huuliza tutoke twende wapi?

Mara nyingi wakiambiwa watoke warudi walikotoka.Ama warudi kuzimu... Thubutuuu kama wamekukimbia huko leo unawaambia warudi huko unadhani watakubali kweli?

Imagine mtu kakimbia hali mbaya ya maisha nchini mwake kisha leo uamwamuru atoke huku aliko arudi kule!!! Hili ni jambo lisilowezekana kabisa.

Mapepo na majini pamoja na kuwa ni viumbe roho vyenye nguvu lakini hupenda kuweka makao yao kwenye miili ya wanadamu wanao wachagua, hivyo usidhani kumtoa pale ni kazi rahisi lazima upate bingwa

Mitume na manabii wengi si wakamilifu na hutumia na nguvu za giza katika huduma zao hivyo wanapokemea mapepo yatoke wanashindwa kwa kuwa hawatendi kwa jina la Mungu kwa asilimia mia...

Ila kinachotokea either mapepo huamua kukaa kimya kuepusha kelele ama kujifanya yametoka na kuwaingiza watumishi husika mkenge.

Wanajua wazi hawawezi kutoka wataenda wapi wakati wameshajichagulia kuwa yale ndio makazi yake?

Ukiona pepo limetoka moja kwa moja jua hilo lilikuwa on transit tu. Jaribu kufuatilia wengi wenye hilo tatizo litapoa tu lakini baada ya muda litarudi tena.
 
Nanukuu

Mapepo na majini yale yaliyowaingia wale kundi la nguruwe wameendelea kuwepo wakitangatanga huko na kule wakitafuta hifadhi kwenye miili ya wanadamu........

Kwaiyo bwana mtumishi unataka kutuambia kwa kipindi kile ambacho vitabu vinatuambia yesu alimtoa mapepo yule afsa aitwae jeshi hakukua na mtu mwingine duniani kwa wakati huo mwenye mapepo zaidi ya huyo jeshi?

Kama kulikua na watu wengine wenye mapepo zaidi ya huyo jeshi kivipi utumie refer ya mapepo yaliyomtoka jeshi kwamba ndio yamekua yakitangatanga kutafuta binadamu wa kumuingia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom