Pepo baya la kisiasa laanza kuinyemelea Chadema, mambo si shwari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pepo baya la kisiasa laanza kuinyemelea Chadema, mambo si shwari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ipole, Mar 26, 2009.

 1. I

  Ipole JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pepo baya la kisiasa laanza kuinyemelea Chadema,mambo si shwari

  Na Ramadhan Semtawa

  UPEPO wa kisiasa katika kambi ya upinzani unavuma vibaya, kufuatia hali ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwa tete.

  Hali tete ya kisiasa ndani ya Chadema imekuja wakati viongozi wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), wakiwa katika hali ya malumbano makali kuelekea kwenye uchaguzi. Nacho chama cha CUF kiliingia kwenye hali ya wasiwasi kisiasa kipindi cha uchaguzi wa viongozi wake hivi karibuni.

  Wakati upepo huo mbaya ukizidi kuvuma kwa kambi hiyo, Chadema moja ya vyama makini chenye historia ya kutatua mambo yake kimyakimya na kuwa na misingi imara ya uongozi kutoka kwa waasisi akina mzee Edwin Mtei na Bob Nyanga Makani, sasa nacho mambo si shwari.

  Tathimini ya kichambuzi na duru za kiuchunguzi juu ya mwelekeo wa mambo kwa kuangalia mtiririko wa matukio, mpasuko huo ndani ya Chadema unatokana na suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans.

  Kutofautiana kwa mawazo na misimamo kwa viongozi wa juu ndani ya Chadema kuhusu Dowans, ni jambo ambalo limesababisha mgawanyiko ndani ya chama.

  Msuguano huo wa fikra na misimamo, ambao umeonekana katika kipindi cha muda wa wiki takriban tatu sasa, ukiwahusisha zaidi Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni mwanasiasa mwenye nguvu, Zitto Kabwe na viongozi wenzake kama akina Dk Wilbrod Slaa, unaonyesha chama hicho sasa kinapita katika wakati mgumu kisiasa.

  Chadema tayari, kilipita katika wakati mgumu kisiasa baada ya kuondokewa na akina Dk Amaan Kabour, aliporejea Chama Cha Mapinduzi( CCM) na wakati kifo cha Makamu Mwenyekiti marehemu Chacha Wangwe.

  Wakati wa kuondoka kwa Dk Kabour, Chadema ilipigwa na mawimbi mazito kisiasa kisha ikaweza kuvuka, ndipo mwaka jana ukatokea mvutano mwingine kati ya Wangwe na viongozi wa juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe katika kutaka kuchukua nafasi ya Mwenyekiti taifa.

  Hata hivyo, joto hilo la kisiasa la sasa ambalo linatokana na ununuzi wa mitambo ya Dowans ambao umekuja katika kipindi kigumu cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na mkuu hapo mwakani, unaweza kuisumbua Chadema.

  Tayari, nyufa ndani ya Chadema zinazotokana na ununuzi wa mitambo ya Dowans, zimeanza kujitokeza kufuatia viongozi hao kutoa kauli zinazoonyesha misimamo tofauti kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans.

  Wakati Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, akisimamia kidete ununuzi wa mitambo hiyo, viongozi wengine wa Chadema wakiongozwa na Dk Slaa pamoja na Mwenyekiti Mbowe, wanapinga.

  Katika kudhihirisha ufa huo, wakati Zitto alimtaka mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe, atangaze maslahi yake katika Kampuni ya Power Pool East Africa, Dk Slaa alinukuliwa na gazeti la Mwanachi Jumapili akisema hakupaswa kutangaza maslahi.

  Dk Slaa katika kauli hiyo, anaonekana kupingana na msaidizi wake wa karibu ambaye ni Zitto katika msimamo kuanzia Dowans na hata uanahisa wa Dk Mwakyembe katika Power Pool.

  Msuguano huo unaangaliwa kama moja ya chanzo, kinachoweza kuleta mpasuko ndani ya Chadema.

  Tayari, msimamo huo wa Zitto kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans na kurusha makombora kwa Dk Mwakyembe, umekuwa ukimfanya ahusishwe na harufu ya ushawishi wa nguvu ya fedha za watuhumiwa wa ufisadi.

  Hivyo, kauli za vigogo hao wa Chadema kupinga ununuzi wa mitambo ya Dowans, ni sawa na msimamo wa chama kukana kauli ya Naibu Katibu Mkuu wake.

  Hata hivyo, akiwa katika mikutano ya Operesheni Sangara Mkoani Kilimanjaro, Mbowe pia alinukuliwa na gazeti la Mwananchi Jumapili, akisema chama hicho kimekuwa kikijiendesha kwa taratibu.

  Mbowe alifafanua kwamba, wabunge wake wanaweza kujadili mambo yao katika kamati lakini si msimamo wa chama.

  Kauli hiyo ya Mbowe ambaye ni Mwenyekiti, ilikuja mahususi kujibu swali kuhusu vipi Zitto aunge mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans na msimamo wa chama ni upi.

  Hata hivyo, kauli hiyo bado inaonekana kushindwa kuondoa wingu zito ndani ya Chadema, kwani Mbowe alimtaka Dk Mwakyembe ahamie chama hicho kwa maelezo kwamba hawezi kupambana na ufisadi ndani ya CCM.

  Mbowe katika kauli hiyo, alisema mfumo ambao Dk Mwakyembe anautumikia hauwezi kupambana na ufisadi, kauli ambayo ilikuwa ni pigo jingine kwa Zitto kwani tayari amekuwa katika malumbano ya kisiasa na mbunge huyo wa Kyela hadi kurushiana makombora akimtaka ajiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Madini.

  Pia, tangu mjadala wa Dowans, Zitto hajawahi kushiriki vema katika mikutano ya operesheni Sangara mkoani Kilimanjaro, huku mara nyingi akiwa Dar es Salaam.

  Wiki hii Zitto alizungumza na gazeti la Mwananchi katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam, ambako aliulizwa kuhusu mjadala wa Dowans na kujibu kwamba aliufunga.

  Zitto akiwa mchangamfu, alisema mjadala huo hauna tija kwa Watanzania kwani umekuwa ukiwagawa badala ya kuleta umoja.

  Akifafanua, alisema jambo la msingi ni kuwepo mjadala wa viongozi kuhusu upatikanaji umeme.

  Zitto ambaye alirusha kombora la mwisho, alisisitiza kwamba ufisadi wa Dowans ni mkubwa kwani hadi Mei mwaka jana ilikuwa imelipwa sh 221 bilioni na serikali.

  Alisema mbali ya kulipwa fedha hizo, pia ununuzi wa mitambo yake iwapo kesi itakwisha ni sh 174 bilioni, na ghara,a ya kuibadili kutoka matumizi ya dizeli kwenda gesi ni sh 35 bilioni.

  ''Sasa, hapa ndipo watu wanapaswa kuangalia wenyewe, mitambo hii wanayosema tununue ni sh 174 bilioni, tumeshalipa sh 221 bilioni, kubadili kutoka dizeli kwenda gesi ni sh 35 bilioni, tupime faida na hasara,'' alisema Zitto baada ya kuulizwa kuhusu ripoti ya uchunguzi inayoonyesha gharama hizo.

  Alisema, hakutetea Dowans kwa kupewa rushwa wala kitu kingine, bali ni kwakuwa yeye ni mchumi na ametumia vigezo vya kitaaluma ya uchumi.

  Hata hivyo, licha ya Zitto kuonekana kutoa vigezo hivyo, bado Chadema, hasa viongozi wenzake wanaona kama kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans ni kukitumbukiza chama katika tuhuma za kutetea ufisadi, kwani Dowans ilirithi mkataba tata wa Richmond.

  Duru za ndani zinaonyesha kwamba, katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema, huenda ikawa ni nafasi ya chama hicho pia kuangalia namna ya kuweza kujisafisha na upepo huo wa Dowans katika nafasi zake nyingine za uongozi.

  Chadema hadi sasa, kinaonekana kuwa makini katika kushughulikia migogoro yake mikubwa kama huo wa Zitto, kwani hadi sasa jinamizi la kifo cha Wangwe bado lingali likikitafuna.

  Kifo cha Wangwe hadi sasa bado kipo kichwani mwa vigogo wa Chadema, ambao walijikuta katika wakati mgumu kuweza kuzima suala hilo.

  Taarifa za ndani zinaonyesha, Kamati Kuu ya Chadema, huenda ikakaa wakati wowote kujadili upepo wa kisiasa ndani ya chama hicho huku Zitto akiwa mada muhimu.

  Juhudi za kuwapata Mbowe na Dk Slaa, hazikuweza kufanikiwa kwani simu zao za viganjani ziliita bila mafanikio.

  Zitto aliondoka juzi kuelekea Uingereza, ambako haijafahamika bayana kitu gani hasa kilichompeleka nchini humo.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chadema nawasihi sana msimfanyie Zitto mzaha,achunguzwe vizuri nyendo zake asijekuwa Kaburu,Walid au Tambwe.Chadema tunaitegemea iiokoe nchi hii 2010 hivyo ijipange vema na kuweka tahadhari kwa mamluki.Mapambano hadi kieleweke,Mungu ibariki TZ,wabariki na wapinga ufisadi wote.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  yaani unaitegemea CHADEMA iokoe nchi watu wengine sijui mmelogwa ,ivi CHADEMA ndio tegemeo lenu ,sawa maana ukipenda Chongo utaliona kengeza ,Chadema ambao uongozi wake unaonyesha rangi za kutumiliwa na makundi ya CCM ,si tunaona wanampa sapoti ya wazi kundi la Mwakiembe ,hivi ah bola ninyamaze maana sikio la kufa halisikii dawa.
   
 4. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Zitto Kaona ukweli na kasema haki.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unajua hivi sasa Zitto anaonekana adui ndani ya Chadema kuna mikutano kibao inafanywa na Zitto hapewi taarifa ,japo wenyewe wanaficha lakini huo ndio ukweli ,ni wakati tu ndio utatujulisha.
   
 6. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Zitto kwa Chadema ni assett, sasa wakiichezea sababu ya kuwa wazi watakuja kulia CCM imewachukulia mtu wao. Kila mtu ana kosa aliyetakasika ni Mungu tu.
   
 7. I

  Ipole JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bwana TIMTIM siyo kweli kwamba kila analolifanya Zito ni sahihi hoja siyo kuwaunga mkono CCM hoja ni kuangalia uwezo na hoja zinazotolewa zina maslahi gani kwa wananchi na nikueleze ndugu yangu hiyo chadema ni chama cha ukabila kama hutoki kaskazini basi hupaswi kuwa kiongozi na ndiyo maana tumeambiwa kuwa mhe Zito haitwi kwenye vikaokwa sababu tu hatoki kaskazini
   
 8. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naamini na mkipinga sawa,ukweli ni kwamba sisemi ndo wanaoivuruga CHADEMA! na hii ina maana kuwa watanzania watazidi kuteswa na chama kimoja mpaka hapo yesu atakapo rudi,Mungu ibariki Tanzania.
   
 9. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa Mbowe kazungumza jambo la maana sana kwa Chama kinachofuata demokrasia. Sio kila kitu amabacho Mbunge anakiamua, anakitetea, anakijadili, anakizungumzia kiwe lazima ni msimamo wa chama, bali anatakiwa kuangalia maslahi ya Taifa. Tukiwa kila kitu kinasimamiwa kwa misimamo ya chama hatuwezi kuendelea hata siku moja.
   
 10. S

  Sumaku Member

  #10
  Mar 28, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto Kabwe alifanya mahojiano mazuri na TBC1,akasema tuangalie maslahi ya Taifa kwanza na pia akashauri kuwa Kamati mbili za Bunge-ya Mashirika na ile ya Nishati zikutanishwe na maofisa husika ili upatikane uamuzi,kwani mambo ni vikaoni. Mzee wa Urambo akakataa.Je,leo mgao huu unaliingizia taifa hasara kiasi gani? Tatizo siasa imeingizwa ktk utendaji,kila jambo linatazamwa kisiasa na pia nani atapata nini na nani atakosa nini! Ndio maana kauli:BORA NCHI IWE GIZANI KULIKO...imetamkwa.
  Kwa hili,niko pamoja na Zitto Kabwe,alikuwa sahihi
  .
  Na kama si uadilifu,giza hili la umeme lingepelekwa ktk Jimbo la Mh.aliyesema kuwa bora nchi ikae gizani! si mnakumbuka kauli-afadhali watu wale nyasi lakini'UROPLENI" ya yule mkubwa inunuliwe? Mh.Kawambwa,Samahani nimekumbuka!Peleka hoja ili tuiuze!
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu SUMAKU,heshima mbele.
  Mheshimiwa Zitto kachemka kwa kiwango cha kutisha.Hakupaswa kuwa mpiga debe wa Downs.Mheshimiwa Zitto pengine alifikiri watanzania ni wavivu wa kuchambua mambo au niwa sahaulifu.Kamati ya bunge ya kuchunguza sakata la Richmond iliishauri serekali siku nyingi kununua mitambo ya kuzalisha umeme inashangaza wahusika hawakuta kufuata maelekezo ya kamati pengine walijua watakuja na mkakati dhaifu wa kuwatisha wananchi eti mtambo wa Dowans usiponunuliwa nchi itaingia gizani.

  Wapo watu wengi wanaojaribu kumtetea mheshimiwa Zitto kwamba kateleza lakini bado hajaanguka,mara oho nchi itaingia gizani lakini ukijaribu kufuatilia hoja zao kwa makini utagundua wanamtetea Zitto kwasababu yuko Chadema.Laiti Mheshimiwa Zitto angekuwa yuko CUF,TLP,NCCR,CCM watu hao hao wangekuja na hoja tofauti kabisa wanavyojaribu kutudanganya sasa.


  Zitto Kabwe hajateleza kama baadhi ya wafuasi wake wanavyotaka tuaamini,kama Zitto kateleza ni kwanini mpaka sasa hajatoa kauli ya kuwaomba radhi wananchi!.Nidhahiri Zitto alikuwa anajua alichokuwa akifanya,napenda kuamini Zitto alivutiwa kitu kidogo kwasababu alijua mwaka 2010 hatagomea tena ubunge ?.

  Zitto si asset kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini kwa kauli yake ya kutetea ununuzi wa mitambo chakavu inayomilikiwa na mafisadi {Rostam Azziz}bado anaendelea kuwa asset?.Huyu mtu mnataka afanye dhambi gani ili aonekane liability katika chama na taifa kwa ujumla?.Tuache tabia ya kupenda kutetea dhambi za watu kwasababu za kujuana au huyu ni mwenzeti,watanzania siku hizi si mabwege tena.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mtanataka mnikumbushe ya marehemu Chacha wangwe na CCM ile ishu ya kuonana na RA hapo kwa hotel mmmmh!Siasa Bongo ni kutumia bongo yako lasivyo watoto watakuwa hawaendi au hawapigi trip toilet oooh.
   
 13. C

  Chuma JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii ni Hatari ktk nchi yetu, kutofautiana mawazo baina yetu kunapelekea kuamini kuwa mmoja wetu amekula kitu kidogo(kuonekana msaliti)...watu watapenda kuunganisha dots ili tu conclusion zao zitimie...

  Pia Tujenge culture ya kuwa kama imetokea kumchukia MTU, basi isitupelekee kutomfanyia uadilifu...
   
Loading...