Penzi la umauti

Duhuu
*PENZI LA UMAUTI-02*

Nilikuwa nikiishi Magomeni mtaa wa Mwinyimkuu, nilifanikiwa kupanga nyumba yenye vyumba viwili. Maisha ya ndoa yalionekana kuwa mazuri sana, yalibadili mfumo mzima wa maisha yangu ukitofautisha na mfumo ule wa maisha tegemezi niliyokuwa nikiishi nyumbani kwetu Kimara kwa Mama Dominick.

Mke wangu Julieth alikuwa ni zaidi ya mke mwema kwangu, hakukuwa na tofauti yoyote katika maisha yetu ya ndoa, kila siku nilizidi kujifunza mambo mengi sana hususani yale ya ndoa.

Nilijifunza juu ya uvumilivu, upendo, upole na busara katika kufanya maamuzi. Vitu hivi ndiyo ngao ambayo niliitumia katika kuishi vizuri na ndoa yangu.

Japo kazi yangu ya ufundi simu haikuwa ikiniingizia kipato kikubwa lakini hiyo haikuwa sababu ya kunifanya nishindwe kuwa mwaminifu wa ndoa yangu, nilikuwa mwaminifu haswaa wala siongopi ninapoyasema haya. Nayamaamisha kutoka katika kitako cha moyo wangu.
Julieth alikuwa ndiye mshauri wangu, alikuwa akinishauri mambo mengi sana hata yale ambayo nilikuwa siyafahamu pia aliweza kunijuza.

Alikuwa na kipaji cha kuniongoza vyema katika maisha yangu, hakupenda kuona naanguka kimaisha hivyo kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu yeye alikuwa ndiye rubani wangu, alikuwa akiniongoza. Hakika elimu yake ya darasa la saba aliitumia katika dhana ya kipekee sana wala sikutaka kuamini.

“Mume wangu pole na kazi,” aliniambia Julieth wakati ambao nilikuwa nimerudi nyumbani, ilikuwa ni majira ya jioni.
“Asante sana mke wangu,” nilimwambia kisha kabla sijakaa kwenye kochi alinipokea kwa kumbato na kunivua begi lililokuwa mgongo mwangu, lilikuwa ni begi lenye vifaa vyangu muhimu vya kazi.

Upendo ulitawala katika maisha yangu, nilihisi kupendwa sana na hii ndiyo sababu iliyopelekea nikazidi kuyasahau yale matusi na maneno ya kejeli niliyokuwa nikiambiwa na ndugu pamoja na marafiki zangu juu ya Julieth mke wangu, walikuwa wakimsema kuwa alikuwa ni mwanamke ambaye hakuwa amesoma.

Kwa upendo aliyokuwa akinionyesha Julieth kwa kweli nilimchukulia kuwa kama zaidi ya msomi, sikuhitaji msomi mwingine ukimtoa Julieth pambo la moyo wangu, furaha ya maisha yangu.

“Nakupenda sana Julieth wangu,” kinywa changu hakikuacha kumkumbusha maneno haya kila siku, ilikuwa ni desturi yangu. Haikuweza kupita siku bila kumsifia Julieth kutokana na uzuri aliyokuwa nao, nakumbuka kuna baadhi ya sifa nilikuwa nikiongezea chumvi.

Hahaha! Ila wanasema yote haya ni mapenzi tu! mapenzi yanahitaji mambo mengi sana yanayoleta furaha ila chunga shubiri isije ingia katika mapenzi yako, utatamani dunia igeuke miguu juu kichwa chini, hutatamani kupenda tena.

“Wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu, nakufananisha na kila kitu ninachokihitaji katika maisha yangu. Sijutii kukuchagua katika maisha yangu.

Naomba utambue kuwa wewe ni zaidi ya kiungo muhimu katika mwili wangu,” nilimwambia maneno ambayo yalijawa na ushawishi wa utamu wa mapenzi ya dhati .
“Dominick nakupenda pia mume wangu,” aliniambia Julieth.

Maisha yetu yalitawaliwa na furaha sana, utamu wa maisha ya ndoa ukanifanya nisahau kabisa shida nilizokuwa nazo, nikazidi kunawiri japo maisha hayakuwa mazuri sana lakini kiupande wa pili wa sarafu wale waliokuwa wakinitazama walikiri kuwa hakika ndoa ilinipenda.

“Aisee Dominick umebadilika kabisa ndugu yangu,” aliniambia Chrispine rafiki yangu ambaye urafiki wetu ulikuwa kama ndugu, nilikuwa nikisaidiana naye mambo mengi sana, hata katika suala hili la mimi kumuoa Julieth alihakikisha anasimama kidedea mpaka nafanikiwa kumuoa.

Alikuwa akifanya kazi katika duka la kuuza Compact Disk (Cd) Kariakoo.
“Ah! Wapi wewe acha mambo yako, huoni jinsi nilivyokondeana hivi?” nilimuuliza swali la kiutani huku kicheko kikishika hatamu yake, nilikuwa nikicheka kwa wakati huo.

“Sasa unacheka nini wakati nakwambia ukweli,” aliniambia Chrispine huku akinitazama, nikazidi kucheka sana.
“Hahaha! Shemeji yako anafanya kazi yake bhana,” nilimwambia maneno ambayo yakamfanya atokwe na tabasamu pana.

“Naam! Hilo ndiyo neno ambalo nilikuwa nataka kulisikia kutoka kwako,” aliniambia.

“Hii ndiyo kazi ya shemeji yako.”
“Hata mimi naona ndugu yangu unapendeza tu!”
“Hahahaha!”

Kila neno alilokuwa akilizungumza Chrispine lilikuwa likinichekesha sana, nilizoea kuzungumza naye kwa utani.
Alipenda kuona nikiishi maisha mazuri ya ndoa yangu, hakupenda kuona nikinyanyasika na mapenzi naweza kusema alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akinipa somo kubwa kuhusu maisha ya ndoa.

Katika maisha yake aliwahi kubahatika kuoa lakini kutokana na mkasa uliyowahi kumtokea hakuweza kuendelea kuishi na mke wake, waliachana.

Aliwafahamu sana wanawake, alifahamu kila kitu kuhusu wanawake na hata kipindi ambapo nilikuwa nikiambiwa na watu kuwa nimuache Julieth nikamuoe mwanamke mwingine hakuweza kukubaliana nalo.

Kwa maisha ya furaha ambayo alikuwa akiona nikiishi baada ya kuoa hakika alifurahi sana, sikumbuki kama kuna neno baya ambalo aliwahi kuniambia ila ninachokikumbuka mimi aliwahi kuniambia kuwa nimuheshimu sana mke wangu.

“Inabidi umuheshimu sana mke wako Dominick, usikubali hata siku moja katika maisha yako itokee ukamuudhi, utakuwa umefanya makosa makubwa sana, jitahidi atamani kuwa na wewe kila siku za uhai wake,” aliniambia Chrispine siku moja tulipokuwa kwenye mgahawa mmoja mtaa wa Kariakoo tukipata chakula cha mchana, alionekana kuwa na mengi sana ya kuniambia siku hiyo.

“Nimekuelewa sana ndugu yangu,” nilimwambia huku nikikitikisa kicha changu kumuonyesha kuwa nilimuelewa sana.

“Unajua wanawake ni viumbe wa ajabu sana, mimi napenda kuwaita sometime jua sometime mvua,” aliniambia maneno aliyoyafumba.
“Kwanini?” nilimuuliza.

“Hawatabiriki yani unaweza ukahisi ni jua kumbe ni mvua aisee,” aliniambia maneno ambayo yalikuwa na fumbo ndani yake, sikuweza kulifumbua kwa haraka, ikabidi nimuulize kuwa alikuwa na maana gani hasa, wakati huo alikuwa akicheka.
“Sasa hapo ni lipi usilolielewa Dominick?”
“Umesema jua mara mvua sijui unamaanisha nini?”

“Inabidi utumie akili nyingi sana kuishi na hawa viumbe aisee hawachelewi kukupa kovu la maisha,” aliniambia Chrispine huku akikipigapiga kijiko katika sahani, alikuwa akitabasamu, sikujua tabasamu lake lilimaanisha nini hasa, nikamuuliza tena.

“Kuna nini?”
“Mkeo anakupenda sana.”
“Ndiyo nalifahamu hilo.”
“Basi jitahidi kuishi naye vizuri ila usiombe wale waliyokutabiria mabaya yakakutokea kweli utahisi dunia imekuelemea.”
“Sawa nimekuelewa.”

“Mpende sana mkeo Dominick naamini wewe ni mpambanaji, pigania penzi lako, pigania ndoa yako usikubali kumpoteza mkeo kwa maneno ya ndugu na marafiki,” aliniambia kisha akanyamaza kidogo halafu akaendelea tena kuzungumza.
“Kuna kitu kimoja inabidi ujifunze,” aliniambia.

“Kitu gani hicho?” nilimuuliza.
“Ishi maisha ya kumpenda kila mtu,” aliniambia Chrispine.
Maneno ya Chrispine yalizidi kunijenga sana, yalikuwa yakiniimarisha vyema, nilisimama imara na ndoa yangu ambayo kila siku nilikuwa nikiifurahia.

Nakumbuka Mama yangu hakuwa akimpenda Julieth hata kidogo hapo awali lakini kupitia maneno na ushauri wa Chrispine niliweza kuutumia katika kumfanya Mama yangu akampenda Julieth, sikumbuki kama ni kweli alimpenda ama la lakini ninachokikumbuka alikuwa akimpenda, yale maneno mabaya aliyokuwa akiyasema kuhusu Julieth yalimuisha.

Ukurasa wa maisha ya ndoa yangu ulikuwa ni wa aina yake, tuliishi kwa upendo sana na mke wangu, alijivunia kuwa na mimi hata mimi pia nilijivunia kuwa na yeye maishani, alikuwa ni hakimu wa moyo wangu, kila kitu ambacho alikuwa akiamua nilikifuata bila kupinga, waliokuwa wakinitazama waliniambia kuwa nimelogwa.

Sikutaka kuyapa nafasi maneno yao yatanitawale, nilichokuwa nikikitazama kwa wakati ule ni maisha mazuri yaliyogubikwa na amani niliyokuwa nikiishi na mke wangu.
“Siamini kama Mama yako amekubali kabisa mimi kuolewa na wewe,” aliniambia Julieth siku moja usiku tulipokuwa kitandani.

“Inabidi uamini sasa Mama yangu anakupenda sana,” nilimwambia huku nikimbusu katika paji la uso wake, alitabasamu kisha nikaitumia mikono yangu vyema katika kumpapasa mgongoni mwake, alikuwa na mwili laini sana uliyonisisimua kimapenzi.

“Furaha yangu sasa naweza kusema imerudi,” aliniambia Julieth kwa sauti ya chini, ilikuwa na utulivu wa aina yake.
“Kwani ilienda wapi?” nilimuuliza kiuchokozi, akatabasamu wakati huo nilikuwa nikiendelea kumpapasa.
“Umeshaanza vituko vyako,” aliniambia.

Haikuchukua dakika nyingi mwisho nikajikuta tayari nimeshazipandisha hisia za Julieth, alionekana kuwewesa kimapenzi, alikuwa akihangaika katika kifua changu.

Sikumbuki ni nini kilitokea ila nilishangaa Julieth akiwa juu yangu tena akiwa uchi wa mnyama, kitendo kilichofuata hapo ilikuwa ni kufanya mapenzi usiku kucha.

Je, nini kitaendelea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom