Penzi la udanganyifu

Light saber

JF-Expert Member
Nov 3, 2017
4,129
7,447
PENZI LA UDANGANYIFU. Ilinyesha kama haijawahi kunyesha hapo awali, siku ile ilikuwa ni ya kipekee. Nilionekana nadhifu na mtanashati ndani ya suti yangu nyeusi, na nilinukia kama mfalme. Sikutaka chochote zaidi ya kutegemea mazuri kutwa nzima.
FDU50ReXEAQwTSZ

"Siyo mimi ni wewe" Nilipokea ujumbe kwenye simu yangu"usijilaumu sidhani kama ninastahili kuwa na wewe" "Ninaamini inakupasa uendelee na maisha yako Heriduki"

Nilifungua mlango na kutoka nje kwenye mvua huku nimevaa suti yangu, nilikimbia zaidi ya kilometa moja, machozi yakinibubujika , lakini hakuna aliyeweza kutambua , labda waridi langu lilikuwa na miiba na nililikamata barabara kwa mikono yangu miwili au labda nilikuwa nikiimba Wimbo ambao nilikuwa siujui, Nisahihi kabisa nilikosea kuyaanda maisha yangu, nilijilaumu. Nilikuwa kwenye huzuni yenye kukatisha tamaa, nikitamani uponyaji lakini nilikuwa nishaumizwa na mapenzi, Tafadhali mvua usiache kunyesha nilijisemea.

Kwa mara nyingine nilirudi kuwa mkiwa na mpweke.


Credits: Heriduki alerwasen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom