Penzi la Kichina

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Yapo mengi ya aina,
Mapenzi ya kila namna,
Ya wazee na vijana,
Mioyo inapeana;
Na lipo penzi la kichina!

Yapo yale ya kizungu,
Ya weupe na wanungu,
Yapo hata ya machangu,
Na ya kufukuzwa na rungu,
Na lipo penzi la kichina!

Yapo yakubembeleza,
Na mengine ya kuliza,
Macho mtu alegeza
Yapo ya kubangaiza
Na lipo penzi la kichina!

Yapo ya kunyemelea
Ya fisi kuchekelea,
Gizani mwatokomea
Kama wanga mwajigea
Na lipo penzi la kichina!

Na yapo ya kuibia
Mapenzi yenye udhia
Mkibambwa mwakimbia
Aibu mwajipatia
Na lipo penzi la Kichina!

Yapo na ya desturi
Hadi kutoa mahari
Na mengine yenye shari,
Yenye kuleta munkari
Na lipo penzi la kichina!

Natunza hili moyoni
Ni siri siwambeni
Ya kichina tamanini
Ni mapenzi ya kigeni
Penzi hilo la Kichina!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Shairi safi sana hili.

Kigezo kipi wasema
ni safi shairi mwana
bujibuji umekwama
wastahili lawama

Ungeliweka bayana
Uzuri Ulo unena
Tungehitilafiana
Japo kwa kukwaruzana

Umechotwa Bujibuji
Mzee Mwanakijiji
Kizuri kwa alhaji
Si kizuri kwa Rufiji

Uchambuzi yakinifu
Ni muhimu maradufu
Kwa hoja kuwa tukufu
Uichambue kwa urefu

Nakuacha Bujibuji
Namwendea wa kijiji
Hujaona wa Ujiji
La Kichina kama uji

Mapenzi kila aina
Kayashusha ye Rabana
Tangu aumbe Karima
Kuna penzi la kichina

Yote yatofautiana
Kwa ladhaye na aina
Kwa saizi ni bayana
La Kichina na Kighana.
 
Back
Top Bottom