G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Juzi nikiwa mkoani Tanga nilijikuta nikisimamishwa na askari polisi akaniambia kuwa kilomita 9 kabla ya kituo chao nilipigwa tochi tena mwanzo wa kibao kinachomalizia limit ya spidi ya 50 km/hr. Nilipoiangalia picha ilipigwa kwa nyuma ya gari ikionyesha nina 53 km/hr. Kwa maana nyingine nilianza kuongeza spidi nilipokaribia kibao hicho.
Hoja hapa ni nini?
Nilimdadisi yule askari wa usalama barabarani na nikaichukua simu yake ili kujiridhisha. Lakini nilipokuwa naiangalia simu yake zikawa zinatumwa picha nyingi sana za magari yaliyozidisha spidi kwenye eneo lile ambalo kimsingi hapakuwa na askari yeyote aliyekuwa akichukua picha. Wapo wanaosema kuwa zile picha huwa zinatumwa na askari aliyejificha kichakani. Nikabaini ni uongo. Asingeweza kuchukua picha zile kwa kiwango kile.
Kufuatilia magari lukuki ambayo mengine yanaanza kupunguza spidi mwanzo wa kibao cha speed limit wengine wwnaanza kuongeza mwishoni na kutuma picha mfululizo vile isingewezekana.
Nilichogundua.
Askari alijichanganya kwa kusema kuwa maeneo haya huwa kuna minara ina "scan" magari kwa kuangalia "speed limit" kwenye vile vibao vyao. Kwakweli nikagundua kuwa vibao vingi vya "Speed limit" barabara ya Tanga na Bagamoyo vipo maeneo ambayo kuna minara ya Vodacom! Hili nimejidhihirisha wakati nikiendelea na safari na kila kwenye kibao cha "speed limit" vingi ya hivyo nimekutana na minara hiyo! Upo uwezekano kuwa wafanyakazi wa Vodacom ndiyo hasa wanaohusika na picha zile na huenda ndiyo hata sababu ya wao kuwa sehemu ya kukusanya tozo za barabarani.
Jihadhari sana usiendeshe zaidi ya spidi 50 kwenye vibao ambavyo ukivikagua utakutana na hii minara ya mawasiliano.
Vilevile ushahidi mwingine ni kuwa zile kamera za askari wetu huwa zinaanza kusoma kuanzia 60 km/hr! Yupo askari mmoja wa kike aliwahi kunikamata maeneo ya Pwani na akaniambia kuwa nimezidisha mwendo ila bahati ni kuwa tochi lake lilikuwa linaanza kusoma kuanzia 60. Na kweli nilikuwa na spidi ya 56. Siku hizi hata 51 tu unaonyeshwa! Jiongeze uchukue tahadhari!