Pentagon yakiri droni za Iran ni "pasua kichwa" kwa Ukraine, USA🇺🇸 na NATO, hakuna 'kinetic interceptors' za kuzidungua!

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,919
15,604
Pentagon yakiri kuwa droni zinazonasibishwa na Muajemi (Iran) zimekuwa "pasua kichwa" kwa Ukraine, US na NATO kwa ujumla. Afisa mwandamizi wa Pentagon amesema droni hizo zinachoma vibaya magarivita ya NATO yaliyopelekwa Ukraine (armored vehicles), mifumo ya ulizi wa anga, mikusanyiko ya wanajeshi wa Ukraine pamoja na zana za mizinga za NATO zilizopelekwa Ukraine (artillery).

Afisa huyo mwandamizi wa Pentagon ameongezea kuwa ni vigumu kujikinga dhidi ya mashambulizi ya droni hizo, kwani Marekani NATO wote hawana 'kinetic interceptors' zenye kuweza kudungua droni hizo.

Akichambua zaidi uwezo wa droni hizo, afisa huyo wa ngazi ya juu wa Pentagon amedokeza kuwa droni hizo zinazohusishwa na Uajemi ni za ajabu. Kwani mbali ya uwezo wake uliotukuka wa kushambulia na kuchoma zanavita mbalimbali ikiwemo mifumo ya Ulinzi wa anga, pia zinafanya missions za sampuli tofauti tofauti ikiwemo kukusanya taarifa za kiintelijensia (intelligence), kufatilia zana na majeshi ya adui (surveillance) , na uchunguzi wa maeneo yenye majeshi ya adui (reconnaissance) na hivyo kuyafanya majeshi ya Ukraine na zana zao kuwa hatarini kushambuliwa na droni hizo wakati wowote.

Taarifa hii imeripotiwa na Marekani yenyewe (The National Interest)
=====

SmartSelect_20221026-101910_Chrome.jpg

A senior Pentagon official did not confirm the exact number of Shahed 136 drones being used to support the Russian effort but made it clear that such an initiative would not be surprising. The Iranian “kamikaze” drones are a loitering munition that can attack from ranges as far as 2,500 kilometers away.

Thousands more Iranian drones may be headed to Ukraine as Russian forces continue to use them to attack armored vehicles, air defenses, troop concentrations, and mobile artillery.

“We do know that Iran has provided Russia with drones for use on the battlefield in Ukraine. While I don't have anything specific to provide in terms of potential future deliveries, it would not -- we would not be surprised were that the case,” a Pentagon official told reporters during a background briefing.

These kinds of weapons present a serious threat to Ukrainian forces as they can be quite difficult to defend against. Large numbers of swarming drones would be quite difficult to target with any kind of kinetic interceptor. These systems also operate at a lower altitude and can be organically launched from dismounted units in close proximity. Finally, these kinds of drones could conduct intelligence, surveillance, and reconnaissance (ISR) missions as well, making Ukrainian armored vehicles, formations, or artillery systems vulnerable to attack.
 
Wamezoea Drone kuja moja moja so easy kuidukuwa hizi za Irani zinakuja Tano Tano au zaidi kwa wakati mmoja hivyo ata kama wanafanikiwa kuipiga moja au Mbili tatu au zaidi lazima zipige Target .

Tatizo ndo linaanzia hapo-pia Zinaruka Below radar Detection na pia zinatembea very slow below military Drone Specifications (nchi nyingi zikiwemo Israel wapo Lab kudesign system ya kupambana nazo ila mpaka sasa bado kichapo kinaendelea.

Kwenye katuni zaTommy and Jery kuna episode moja Mwenye Nyumba alinunua robotic Cat (mecano) apambane na Jerry- Jerry alitumia hii trick ya kutuma vipanya vya Chuma zaidi ya Viwili kwa wakati mmoja .

Mziki wake ulikuwa sio mdogo Mecano alizibitiwa na Mwenye nyumba ilimbidi amrudishe Tom kuendelea na kazi ya kumdhibiti Jery
 
Sikiri mbona unakuwa Kama timu NATO, kurejea (repost)thread ulokwisha ileta humu jamvini siku chache zilizopita? Nakukubali but bring new updates
Hapana Mkuu, taarifa hii sijaileta humu...hii ni mupyaa, na imechapishwa jana tu October 25.

Taarifa niloileta huko nyuma (October 14) ni hii hapa:

 
Hapana Mkuu, taarifa hii sijaileta humu...hii ni mupyaa, na imechapishwa jana tu October 25.

Taarifa niloileta huko nyuma ni hii hapa:

Alafu hizi Drone zikienda zimeenda- zikisha piga Target zenyewe pia zinageuka bomu zinaongeza Ukubwa wa kichapo kilichotokana na mabomu yaliyibebwa nayo ambayo uzito wake ni kuanzia 5 to 50 Kgs .
 
Sikiri mbona unakuwa Kama timu NATO, kurejea (repost)thread ulokwisha ileta humu jamvini siku chache zilizopita? Nakukubali but bring new updates
Nahisi hii ameileta kwa kua Afisa kutoka "pentagon" nae kakili uwezo wa hizo drone za Iran.
Kama Wataalamu kutoka pentagon nao wameongea,basi hii ni habari mpya.
Nadhani mwenyewe unaujua uzito wa Pentagon.
 
T14 Armata naona ofisi yenu ya Pentagon imetoa neno kuhusu zile droni zinazonasibishwa na Muajemi🤣🤣😇😇

Kizuri chajitangaza, hakihitaji kupigiwa promo.

Vile vidroni vya Marekani vilivyopelekwa Ukraine vilipigiwa promo mno na Western media zote. Ikadaiwa kuwa ni superweapons, game changers. Naona sasa hivi hata havitajwi tena.

Sasa 'kizuri' kimeingia kimyakimya kwenye safu za vita, kinajitangaza chenyewe...
 
Kwa hiyo wamekubali kufata matakwa ya Urusi au watazivumilia na kuendelea na mapambano? USA/NATO wana uwepesi sana kuongea na kukiri udhaifu au ushindi, ni kutazama matendo yao tu ndipo kutakupa picha ya nia yao halisi.
 
Nahisi hii ameileta kwa kua Afisa kutoka "pentagon" nae kakili uwezo wa hizo drone za Iran.
Kama Wataalamu kutoka pentagon nao wameongea,basi hii ni habari mpya.
Nadhani mwenyewe unaujua uzito wa Pentagon.

Mkuu,ukiona Pentagon inakiri adharani basi wenye akili wanajua ngoma imeanza kuwa nzito - hutasikia tena ngonjera za HIMARS na Switchblade kuwa ni game changer!!
 
T14 Armata naona ofisi yenu ya Pentagon imetoa neno kuhusu zile droni zinazonasibishwa na Muajemi🤣🤣😇😇

Kizuri chajitangaza, hakihitaji kupigiwa promo.

Vile vidroni vya Marekani vilivyopelekwa Ukraine vilipigiwa promo mno na Western media zote. Ikadaiwa kuwa ni superweapons, game changers. Naona sasa hivi hata havitajwi tena.

Sasa 'kizuri' kimeingia kimyakimya kwenye safu za vita, kinajitangaza chenyewe...
Hapa ni 2011 Marekani ikiwa na drones za kwenye ndege. B-52 inabeba drones na kuzitawanya, nyinyi bado mnashangilia drones za kubebwa na maroli
IMG_20221026_115421.jpg


China wamezijaza maelfu na maelfu ila Russia eti superpower ila hana
 
Alafu hizi Drone zikienda zimeenda- zikisha piga Target zenyewe pia zinageuka bomu zinaongeza Ukubwa wa kichapo kilichotokana na mabomu yaliyibebwa nayo ambayo uzito wake ni kuanzia 5 to 50 Kgs .
Sio mchezo kwa lugha nyepesi tunaweza tukaziita Dronebomu Yani zikimaliza kurusha mabomu iliyobeba bomu la mwisho ni Drone yenyewe

Ila Iran anasema sio zake Sasa sijui kwa nini wanaendelea kulazimisha kuwa ni za Iran
 
Hapa ni 2011 Marekani ikiwa na drones za kwenye ndege. B-52 inabeba drones na kuzitawanya, nyinyi bado mnashangilia drones za kubebwa na maroliView attachment 2398247

China wamezijaza maelfu na maelfu ila Russia eti superpower ila hana
Unazungumzia drones zipi za Marekani? Hizi zilizopelekwa toka May (karibu miezi sita imepita sasa) tukiaminishwa kuwa ni 'game changer' lakini zikachakazwa vibaya na hadi leo hii hazitajwi tena popote?!

Marekani hajawahi kuwa na zana bora zenye kuweza kufua dafu kwenye ushindani huru...na ndio maana huwa akipeleka zana zake sehemu hataki zana za maadui zake zipelekwe...atavuliwa nguo.

Sasa hivi yuko analialia tu na kupiga mayowe kwa nini Iran apeleke droni zinazochoma zanavita za Marekani + NATO zilizopelekwa Ukraine.

Mwambie aache kujilizaliza, yeye si alipeleka game changers, zimeenda wapi?! Apeleke game changers nyingineee.

SmartSelect_20221026-120102_Chrome.jpg
 
Siku zote bidhaa mbovu hupigiwa promo kubwa ili zikubalike...wakati kizuri hujiuza chenyewe

Droni za Marekani zikipigiwa chapuo mwezi wa nne kuwa zitageuza hali ya mambo Ukraine...Leo hii (miezi 7 sasa imepita) hazitajwi tena, na zimefeli vibaya kwenye kukabiliana na adui mwenye zana madhubuti (Urusi).

Hizo droni wazipeleke Iraq na Afghanistan, huko ndio huwa zafanya vyema.

SmartSelect_20221026-120246_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom