Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,743
- Thread starter
- #81
Bukyanandi hakuna mtu anakataa uwezo S-400 lakini msituambie haipitiki or is like iron dome Fulani,kwanza niliwahi kumsikia one General akisema dawa ya good defence system is overwhelm with cheap cruise missiles kabla hujailipua yenyewe,imagine 100 cruise missiles per minute targeting your system utashusha ngapi na ngapi zitakulipua? is more theory na wala sina uhakika lakini it does make sense
Ni kweli KOBA 100 cruise missiles/artillery shells per minute ni very overwhelming kwa Defence system moja lakini KOBA kumbuka kwamba S-400 hakai peke yake kwenye site Warusi ni wajanja sana wanaweka vile vile Pantsir ili isaidie kuongeza layer nyingine kukinga Air defence Unit (S-400) kwa mashambulizi ya kutoka angani hasa hasa ya masafa mafupi, Pantsir -S1 ni highly mobile na ina-track na kupiga ikiwa inatembea - rate of fire na ku-load kwake inatisha sana mkuu.
Ni i kweli vile vile kwamba Wamerika wanajaribu kubuni mfumo wa ku-overwhelm lS-400 kwa kutumia cheap cruise missiles au mfumo wa wasps/bees in form of tiny drones nyingi kwa mpigo kama mashambulizi ya nyuki - Merikani imekwisha fanyia majaribio mbinu hizo lakini wakagonga kisiki cha kuipumbaza Pantsir S-1/2 mpaka sasa bado wanapiga mbongo zao jinsi ya ku-deal/contain Pantsir-S1 kwanza, nilisoma sehemu Warusi wakisema itachukua Merikani miaka ishirini ku-defeat systems za S-400 sasa sijui kuna ukweli gani katika madai hayo.
Labda niongeza kwamba kisayansi uwezi kurusha 100 cruise missiles per minute kutoka sehemu moja hii inatokana kwamba cruise missile inafyatuliwa kwanza kama roketi kwa kutumia solid fuel wanafanya hivo ili gas turbine engine(jet engine) ipate enough compressed air kutokana na kasi ya booster ya roketi - hewa hiyo ikifika kwenye combustor inachanganywa na kerosene halafu inawashwa na sparkplug muwasho huo unakuwa continous kama stove au Petromax inavyo fanya kazi, itazima tu kama mafuta yamekwisha au hewa haitoshi, it takes about 15 seconds au twenty kama sikosei cruise missile kufikia hatua ya jet engine ku-kick in, jet engine ikisha
waka booster ya roketi inazima na kutemwa,missile ikifikia hatua hiyo inapaa/safiri kama jetfighter kwa kukunjuwa winglets automatically.
Ukiangalia vizuri cruise missiles ufayatuliwa moja baada ya nyingine kunakuwa na time lag 4 a reason wanafanya hivyo ili booster inapo temwa debris zisije zikaingia kwenye compressor za jet engine, cruise missiles zinafuata same flight path/curve zinakuja kusambaa huko mbeleni huko ndiko zinafuatisha ramani za target ambayo imekuwa digitised na kuwa uploaded kwenye memory zake.