The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,908
- 2,889
Baadhi ya wabunge wa CCM wamependekeza itungwe sheria ili wanasiasa watakaohama chama cha siasa wanyimwe pensheni zao lakini pia wabunge hao wameenda mbali zaidi na kutaka itungwe sheria ya kuwabana watumishi waliotumikia nyadhifa za juu kabisa za kiserikali wasihame vyama mara baada ya kumaliza muda wao wa utumishi wa umma.
Serikali imesema leo kuwa mawaziri wakuu waliokihama Chama cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kulipwa pensheni zao kwa mujibu wa sheria ya nchi.
Mawaziri wakuu hao; Fredrick Sumaye na Edward Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema)na badaye Lowassa aligombea urais chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji endapo watu waliokuwa katika nyadhifa hizo wanaweza kuzuiwa kuchukua pensheni zao kwa kuhamia upinzani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema sheria haizuii kwa kuwa kuhama chama ni haki ya kikatiba.
Akinukuu Sheria ya mwaka 1999 pamoja na ile ya mwaka 2005 ya Utumishi wa Umma, Kairuki amesema waliokuwa viongozi katika nyadhifa hizo wana haki ya kuendelea kupata stahiki hizo kisheria.
Hata hivyo ameonya kuwa, wanapaswa kuheshimu sheria ya nchi inayowazuia kutoa siri za nchi wakati wakiwa katika nyadhifa zao.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema uchumi ukiimarika utaisaidia serikali kuwalipa wastaafu pensheni itakayokidhi mahitaji yao.
Chanzo: Mwananchi