Pengo: Ugumu wa maisha ungeanza kwa viongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo: Ugumu wa maisha ungeanza kwa viongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Aug 7, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,438
  Trophy Points: 280
  Ibrahim Yamola | Mwananchi | Agosti 07, 2012

  ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema ugumu wa maisha unaowakabili Watanzania sasa, ulipaswa kwanza kujionyesha kwa viongozi wa Serikali.

  Kardinali Pengo aliyasema hayo juzi katika kipindi maalumu kilichorushwa na Radio Tumaini, kuadhimisha miaka 68 tangu alipozaliwa Agosti 5 mwaka 1944.

  “Hali ngumu kwa Watanzania angalau kwa kiasi fulani ingeanzia kwa viongozi wetu, tukaona kuwa wameshiriki na sio hali ngumu huku wengine wanakula raha mstarehe kwa kula nyama choma kuanzia asubuhi hadi jioni”alisema Kardinali Pengo.

  “Watanzania wa kawaida hawana hata fedha ya kununulia Aspirini, maskini wanakufa, tofauti kabisa na ilivyo ka viongozi wetu wa sasa ambao hawana uzalendo,” alisisitiza.

  Kuhusu vurugu na migomo katika shule mbalimbali nchini, kiongozi huyo wa kidini alisema inachangiwa na watoto wa vigogo wailiokula na kushiba kutokana na utajiri wa wazazi wao.

  Aliwataka vijana wasiilalamikir Serikali na kuitaka iwasaidie kwa kuwapatia chakula na badala yake, wajitume katika shughuli za kilimo.

  “Tusianze kulia kuhusu maisha magumu na tusianze kulalamika na kumuambia Rais kwamba hatuna hata mchicha, sasa yeye azalishe wapi,na ndio maana tunaona Wachina wanakuja na kuzalisha na baadaye kutuuzia tukiwa ndani ya ardhi yetu” alisema Askofu Pengo.

  Pia alisema katika siku za hivi karibuni amekuwa hapati usingizi kila anapofikiria mustakabali wa amani ya nchi na mwelekeo wake hasa baada ya baadhi ya watu kuchomeana makanisa na kutukanana ovyo.A

  kizungumzia wazazi wake, Kardinali Pego alisema baba yake (Joseph ) alizaliwa Kaskazini mwa Zambia na mama yake Rozalia, ni Mtanzania.

  “Kwa kuzaliwa baba yangu ni Mzambia, lakini alipokuwa mdogo kabisa alivuka na kuingia Tanzania enzi hizo palikuwa hakuna mipaka kama ilivyo hivi sasa,” alisema Askofu Pengo.

  Alisema baadaye, wazazi hao walifunga ndoa na kufanikiwa kuwazaa watoto tisa, watano wakiwa wa kiume na wengine wanne wakiwa wa kike
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Polycarp Cardinal Pengo angeanza yeye kuishi kimasikini kama Mtanzania wa kawaida. Kwa kweli hakuna MTANZANIA anayestahili kulipwa hata mshahara wa milioni moja kwa mwezi kwenye ajira yoyote ya UMMA kuanzia Rais mwenyewe!
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Big up Pengo!watu wanagoma na kuandamana bse ugumu wa maisha uko upande mmoja tuu wa shilingi ie wananchi uku viongozi na familia zao wanakula good time!Imagine mtu ana deposit worth a trillion ivi atakuelewa ukimwambia kuna shida uyo!Si atacheka tuu
   
 4. m

  markj JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Na yeye basi aishi kama mtanzania wa kawaida! Mbona hata yeye anaishi maisha hata zaidi ya rais!
   
 5. m

  markj JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  NI KWELI KABISA! ila tatizo viongozi wa dini wa hii nchi walishayaona haya kitambo, sema wao ndo walikuwa wakiyafuga kwa kuwapigia chapuo hawa viongozi! mana hata wao hizi pesa zetu wanzila kwa namna moja ama nyingine pia!
   
Loading...