Unajua sikutegemea Polisi wetu wawe vihiyo namna hii. Maelezo yao jana hayana mantiki hata chembe. Kama viongozi wa Chadema walikuwa tayari mikononi mwa Polisi pale kituoni waliweza kuwasiliana vipi na vijana mitaani na kuwachochea wavamie kituo cha polisi ili kuwaokoa vongozi wao? Vile vile ilikuwaje basi Polisi wakavunja vioo vya magari barabarani kama tulivyoona kwenye luninga? Je na magari nao yalikuwa yakielekea kituo cha polisi kuwaokoa kina Mbowe? Yale yale ya 2005 wakati Mahita alisema CUF wameingiza contena na majambia!! Complete hogwash!!