Pengo la Lissu, Mnyika na Zitto halijazibwa bungeni! Hizi tozo za kizalendo zisingepita bila marekebisho makubwa!

Kiukweli kilio cha wananchi huko mitaani kuhusu maumivu ya tozo za kizalendo au mshikamani kimekuwa kikubwa mno.

Wananchi wanawakumbuka Tundu Lissu, J J Mnyika na Zitto Kabwe na kusema hivi " vidume" vingekuwepo bungeni ama tozo hizi zisingepita au zingepita baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa sana.

Wewe mdau unasemaje?
Hakuna cha huyu wala yule! Hakuna cha CCM wala CHADEMA! Wote mabwege tu! Miaka yote ya CHADEMA kukuwa wakiwa bungeni na kuwa chama kikuu cha upinzani, mbona hawajawahi kulaani wao kutolipa kodi?

Shida siyo kukataa tozo au kupunguza tozo hizo, kwa nini wao hawalipi kodi halali ya kipato chao? sasa leo unaanza kuonesha eti Lissu ni wa maana sana! Lini aliomba wabunge walipe kodi? Wote ni wapigaji na ndo maana Bunge la Katiba, Lissu alimuingiza dada yake. Leo hii yuko wapi ktk siasa? Si aliingia kupiga pesa tu!
 
Back
Top Bottom