Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

esitena tetena

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
1,747
1,082
pengo.jpg

Mwadhama Kadinali, Polycarp Pengo amesema kwamba kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge mkoani Kagera, Severine Niwemugizi kwamba Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni binafsi siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Pengo alisisitiza hilo wakati akitoa ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo siyo msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna taratibu zetu za kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka.

Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ilivyoanza kufanya.

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba mpya. Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka.

“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba,” alisisitiza Kadinali Pengo.

Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Marek Solczynski hakutofautiana na kauli ya Kadinali Pengo kwa kusema pamoja na kwamba Askofu Niwemugizi ana haki ya kutoa maoni yake lakini tatizo linakuja pale watu wakaposhindwa kung’amua kuwa ni maoni binafsi au ni ya kanisa.

Amesisitiza kwamba kanisa lina taratibu zake za kutoa maoni kwa masuala ya kijamii na kwa Serikali. “Hayo ni maoni yake binafsi na wala yasihusishwe na kanisa katoliki,” alisema Balozi Askofu Merek.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbeke cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongini mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo walisema, pamoja na mjadala mkubwa ulioibuka na baadhi ya wanasiasa kususia mchakato wa kukamilisha Katiba mpya, wataalamu wa sheria wanasema Katiba inayopendekezwa ilikuwa ni bora kuliko ya sasa ikiwemo kuruhusu wagombea kuhoji mahakamani matokeo mbalimbali ikiwemo ya urais.

“Hata mimi ukiniuliza leo tuache kufanya mageuzi ya msingi katika jamii ili kuwa na uchumi imara au tuanze kushughulika na Katiba mpya, nitakwambia tuachane na Katiba.

“Nakumbuka ile Katiba Inayopendekezwa ilikuwa na masuala makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo kipengele cha kupinga matokeo ya urais lakini kwa kuwa kuna watu walikuwa na maslahi yao binafsi, wakatoka nje ya Bunge na kukwamisha mchakato ule sioni uharaka wa leo tuache mengine yote turejee kwenye mchakato huu,” alisema Wakili wa Mahakama Kuu, James Nandonde.

Chanzo: Mwananchi

Kwa kauli ya Niwemugizi soma zaidi hapa;

Kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki, askofu Pengo sio msemaji wa kanisa. Msemaji ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.
pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.
chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.
Ingekuwa Heri kama huyu mzee angepumzika kwa sababu amefikia umri wa kuanza kurudi utotoni.Pumzika mzee Pengo sio wakati wako huu.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anawadanganya watu kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa mwanza,pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo
Mkuu raisi wa baraza la maaskofu ni wa Iringa, Ngalalekumtwa alichukua kutoka kwa huyo wa Mwanza Dr. Ruweichi na msaidizi ni Niwemugizi wa jimbo la Rulenge kama sijakosea!
 
Kwa ufupi

Kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara

Dar es Salaam. Mwadhama Kadinali, Polycarp Pengo amesema kwamba kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge mkoani Kagera, Severine Niwemugizi kwamba Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni binafsi siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Pengo alisisitiza hilo wakati akitoa ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo siyo msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimao wa kanisa kwa sababu sisi tuna taratibu zetu za kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka.

Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ilivyoanza kufanya.

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba mpya. Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka.

“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba,” alisisitiza Kadinali Pengo.

Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Marek Solczynski hakutofautiana na kauli ya Kadinali Pengo kwa kusema pamoja na kwamba Askofu Niwemugizi ana haki ya kutoa maoni yake lakini tatizo linakuja pale watu wakaposhindwa kung’amua kuwa ni maoni binafsi au ni ya kanisa.

Amesisitiza kwamba kanisa lina taratibu zake za kutoa maoni kwa masuala ya kijamii na kwa Serikali. “Hayo ni maoni yake binafsi na wala yasihusishwe na kanisa katoliki,” alisema Balozi Askofu Merek.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbeke cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongini mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo walisema, pamoja na mjadala mkubwa ulioibuka na baadhi ya wanasiasa kususia mchakato wa kukamilisha Katiba mpya, wataalamu wa sheria wanasema Katiba inayopendekezwa ilikuwa ni bora kuliko ya sasa ikiwemo kuruhusu wagombea kuhoji mahakamani matokeo mbalimbali ikiwemo ya urais.

“Hata mimi ukiniuliza leo tuache kufanya mageuzi ya msingi katika jamii ili kuwa na uchumi imara au tuanze kushughulika na Katiba mpya, nitakwambia tuachane na Katiba.

“Nakumbuka ile Katiba Inayopendekezwa ilikuwa na masuala makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo kipengele cha kupinga matokeo ya urais lakini kwa kuwa kuna watu walikuwa na maslahi yao binafsi, wakatoka nje ya Bunge na kukwamisha mchakato ule sioni uharaka wa leo tuache mengine yote turejee kwenye mchakato huu,” alisema Wakili wa Mahakama Kuu, James Nandonde.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa Katoliki, askofu Pengo sio msemaji wa kanisa Msemaji ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa mwanza,pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Pengo anautumia mwanya wa Watanzania wengi kutojua kua yeye ni askofu tu kama walivyo maaskofu wengine akiwa hapa tanzania.utadhani yeye ndo msemaji wa wakatoliki Tanzania.na ikumbukwe hata askofu niwemuganyizi hakusema kua ule wa katiba mpya ndo msimamo wa Wakatoliki Tanzania kojikombakombaaa tu.
 
Nathubutu kusema Askofu wangu Pengo uzee unamwingia vibaya...hata hekima ile ya kawaida ambayo angeweza kuwa nayo kijana form four failure kwake imeshaondoka{natubu kunena haya juu ya mpakwa mafuta}ila ukweli lazima usemwe!!!sijui amehongwa au ninini sijui,labda nae anautafuta ukuu wa wilaya?!au ukatibu mkuu!inasikitisha.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa mwanza,pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Exactly!
 
Kwa ufupi

Kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara

Dar es Salaam. Mwadhama Kadinali, Polycarp Pengo amesema kwamba kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge mkoani Kagera, Severine Niwemugizi kwamba Katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi ni maoni binafsi siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Pengo alisisitiza hilo wakati akitoa ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo siyo msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimao wa kanisa kwa sababu sisi tuna taratibu zetu za kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Alifafanua zaidi kwamba kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa kanisa au jimbo anakotoka.

Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ilivyoanza kufanya.

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba mpya. Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka.

“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba,” alisisitiza Kadinali Pengo.

Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Marek Solczynski hakutofautiana na kauli ya Kadinali Pengo kwa kusema pamoja na kwamba Askofu Niwemugizi ana haki ya kutoa maoni yake lakini tatizo linakuja pale watu wakaposhindwa kung’amua kuwa ni maoni binafsi au ni ya kanisa.

Amesisitiza kwamba kanisa lina taratibu zake za kutoa maoni kwa masuala ya kijamii na kwa Serikali. “Hayo ni maoni yake binafsi na wala yasihusishwe na kanisa katoliki,” alisema Balozi Askofu Merek.

Hivi karibuni Askofu Niwemugizi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kipaumbeke cha kwanza cha Watanzania ni Katiba mpya na kuongeza yeye binafsi ni miongini mwa watu walioipinga Katiba Inayopendekezwa.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo walisema, pamoja na mjadala mkubwa ulioibuka na baadhi ya wanasiasa kususia mchakato wa kukamilisha Katiba mpya, wataalamu wa sheria wanasema Katiba inayopendekezwa ilikuwa ni bora kuliko ya sasa ikiwemo kuruhusu wagombea kuhoji mahakamani matokeo mbalimbali ikiwemo ya urais.

“Hata mimi ukiniuliza leo tuache kufanya mageuzi ya msingi katika jamii ili kuwa na uchumi imara au tuanze kushughulika na Katiba mpya, nitakwambia tuachane na Katiba.

“Nakumbuka ile Katiba Inayopendekezwa ilikuwa na masuala makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo kipengele cha kupinga matokeo ya urais lakini kwa kuwa kuna watu walikuwa na maslahi yao binafsi, wakatoka nje ya Bunge na kukwamisha mchakato ule sioni uharaka wa leo tuache mengine yote turejee kwenye mchakato huu,” alisema Wakili wa Mahakama Kuu, James Nandonde.
Askofu Pengo ni irrevant kwa jamii ya sasa iliyojaa vijana wengi, hapaswi hata kuongea.

Muda wake wa kukaa na vijana umeisha, aende kwenye Nyumba za mapumziko ya mapadri waliozeeka au akaombe chumba Vatican.

Hizo seminari zina ada kubwa kweli kweli wakati wanaoziendesha ni watoa sadaka, hata hospitali ya Bugando, tangu wakabidhiwe gharama zimekuwa Mara mbili, hana moral authority kuongelea elimu na afya.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom