Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo nia askofu wangu, lkn mvuto na weledi wake haupo tena nafikiri ni umri umekwenda. Ni vzr angekaa kimya kulinda heshima yake.
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Ndugu, mie ni mkatoliki tena wa jimbo la dsm, elewa kuwa pengo sio msemaji wa kanisa katoliki, na wala sio mkuu wa maaskofu wa Tz.
 
Huyu askofu hebu apambane na ya kanisani kwake haya ya katiba awaachie wanaoelewa umuhimu na uzito wake
 
ahsante kwa elimu nzuri. nmeeelewa huyu katumwa na nani kujib la mkubwa wake


HUYU NDIYE RAIS WA NCHI 2020

Na, Thadei Ole Mushi

Kuna watu bado wanaamini kuwa propaganda inafanya kazi kwenye siasa zetu za Tanzania. Propaganda zilikiwa zinafanya kazi kuanzia Kipindi cha Mkapa Kurudi Nyuma ila kwa sasa propaganda hazifanyi kazi sana.

Ni maeneo machache sana na kwa aina fulani ya watu ambao bado aina hii ya siasa inafanya kazi.

Hata vyama vyetu vya siasa vingi vimefuta vitengo vyao vya propaganda na kuanzisha kitengo cha uenezi ambavyo kwa baadhi ya vyama wameweka idara za utafiti. Kwa maana hiyo tumeingia kwenye siasa za utafiti maana yake tumeingia kwenye siasa Za Kusema ukweli.

Sio kwamba wanasiasa wanapenda kufanya siasa za aina hii hapana bali wapiga kura ndio waliowalazimisha kuingia kwenye siasa za aina hii. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wasomi Tanzania na kukua kwa Technolojia ya habari na mawasiliano moja kwa moja imebadili aina ya wapiga kura huwezi kuwadanganya tena kwa Propaganda.

USHINDI WA RAIS 2020 HUU HAPA

Sensa ya mwaka 2012 inatuambia kwa statistics kwamba idadi kubwa ya watu waliopo Tanzania ni watoto na vijana. Watoto ni asilimia 44 huku vijana wakiliwa asilimia 35. Ikumbukwe kuwa watoto ni vijana wa kesho.

Hadi kufikia mwaka 2012 takwimu za sensa zilikuwa zinaeleza kuwa kwa kila watu 10 wa Tanzania, wanne ni vijana ambao umri wao ni kati ya miaka 15 na 35. Hao sita wengine waliobakia ni watoto na watu wazima.

Takwimu hizi zinaoana na wale waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura mwaka 2015 ambapo vijana kati miaka 18-35 waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 12,894,576 sawa na asilimia 57 ya wapiga kura wote. Japokuwa kwa takwimu hizi zinatuonyesha kuwa kuna vijana wengi sana ambao hawakujiandikisha kupiga kura kutokana na sababu mbalimbali.

Kama vijana wote watajiandikisha kupiga Kura 2020 basi idadi ya wapigakura inaweza kuwa asilimia 70 na zaidi ni vijana huku asilimia hizi zikionekana kuongezeka kutokana na kundi kubwa la watoto wanaoingia kundi la vijana.

TAFSIRI YAKE NI NINI?

Tafsiri yake ni moja tu kuwa atakayefanya siasa na kundi hili ndiye atakaye kuwa na wapiga kura wengi 2020.

Utafiti wa juzi wa Twaweza umeonyesha mwelekeo mzuri wa kukubalika kwa vyama vya upinzani kutoka kwenye kundi hili. Hivyo hili ndio kundi linalopaswa kupiganiwa na kila chama ili Kujihakikishia ushindi wa 2020.

Kundi hili Kubwa ni wamachinga, vijana waliomaliza vyuo na waliopo vyuoni huku wengine wakiwa madarasa ya juu ya shule za sekondari. Kwa CCM wajiangalie wamewagusa kundi hili kiasi gani na ni kwa nini hawaongei lugha moja na wao ili watatue changamoto zao ili wanufaike na kura hizi.

Hata kwa wenzetu Kenya angalieni kwenye Kampeni ndio kundi linaloonekana sana kwenye kampeni tofauti na wazee. Kwa maana hiyo ni kundi lililoamua kufanya siasa na hata ukiangalia matokeo ya Uraisi wa Kenya na Tanzania kura za wagombea Urais hazitofautiani sana. Lolote kwenye Siasa linawezekana.

Hitaji la kundi hili ni moja tu, nalo ni Ajira.

2. BUNGE.

Wabunge wengi wanapigania maisha yao kwa sasa kuliko wanavyopigania maisha ya wananchi wao. Yaani wabunge wengi akili zao hazijatulia kuwasaidia wananchi wao bali wanawaza kesho yao. Kwa Tafsiri rahisi ni kwamba Wabunge pamoja na wananchi wao kila mtu "anapambana na hali yake"

Kuna viashiria vingi sana vya kwamba wabunge wetu mfukoni mwao hakuna fedha hivyo anawaza kwanza maslahi yake kabla ya maslahi ya Umma.

Wakati Lisu anasafirishwa kwenda Kenya yule Mbunge aliyewakopeshea ndege kwa mali Kauli aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakati wanatafuta ndege ile hakuna Mbunge hata mmoja aliyekuwa na Dola elfu moja. Sio kwamba walikuwa hawana mfukoni la hasha hata ukienda kwenye account zao utakuta mambo ni yale yale.... ndio maana ndege ikakopwa kwa mali Kauli.

Wabunge kushindwa kutoa sitting allowance yao ya Siku moja yote na kuishia kutoa nusu ni kiashiria Kingine cha hali ya mifuko yao.

Jana Spika kaomba Bunge liongezewe budget kwa manaana hiyo Mhimili huu una njaa kali kuliko huku mtaani. Kuna wanaohoji siku za vikao vya bunge na siku za utendaji wa kamati kupunguzwa, nafikiri hii ni Prediction tosha ya mawazo yao.

NINI KITATOKEA?

Wabunge wengi watashindwa kukamilisha ahadi zao. Wakishindwa maana yake wagombea wapya watakao jitokeza 2020 wana nafasi kubwa sana ya kushinda uchaguzi kutokana na ambao walikuwepo kushindwa kukamilisha ahadi zao.

Kila chama kinatakiwa kifanye tathmini ya wabunge wao wameshafanya nini mpaka sasa na kama hakuna kitu waanze kuandaa watu wapya.

Eneo hili litawaathiri zaidi CCM kwa kuwa wabunge wa CCM hawanaga utamaduni wa kukubali kushindwa kwenye kura za Maoni ni mpaka wapigwe mieleka kama Stephen M. Wasira hifadhini maneno haya.

3. CCM

CCM itoke sasa ndani iingie kwenye Uwanja wa Siasa. Swala la kutegemea tena wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kufanya siasa badala yao ni kuhatarisha uhai wa chama.

Jukumu la kwanza la wakuu wetu wa wilaya na mikoa ni ulinzi na Usalama wa maeneo yao jukumu la kupambana na vyama vya siasa linatakiwa liachiwe vyama vya siasa wenyewe.

Kitendo cha kuuachia mhimili huu wa dola kufanya siasa ni kuviingiza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwenye siasa.

Mkuu wa Mkoa au Wilaya akishindwa kwa hoja na vyama vya siasa unafikiri akili yake itamsukuma kufanya nini zaidi ya kuagiza flan akamatwe na flan akamatwe?

CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kukabiliana na upinzani na kama kutaonekana kuna viashiria vya uvunjifu wa amani ndio hawa wakuu wa mikoa na wilaya wajitokeze kuweka mambo sawa.

Hili litasaidia kuviondoa vyombo vyetu kwenye siasa. Kama ni mfuatiliaji wa habari za Tanzania hawa Ma-RPC wetu hawakauki kwenye vyombo vya habari na wote wanatoa matamko ya kuwadhibiti wanasiasa utafikiri nchi ipo kwenye vita

Thadei Ole Mushi,
Kada wa CCM damu,
19/09/2017.

Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake


Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
 
Yeye ametoa maoni yake yeye kama yeye wala hujasema huo ndiyo msimamo wa kanisa.
Mkuu, alikuwa hatoi msimamo wake ila alichokuwa akikifanya ni kutoa msimamo wa KANISA KATOLIKI kuhusiana na 'MAONI BINAFSI' ya Askofu Niwemugizi.
 
Huyu askofu hebu apambane na ya kanisani kwake haya ya katiba awaachie wanaoelewa umuhimu na uzito wake
Yeah mkuu. Huyu sasa kama mwanasiasa. Katiba ndio msingi wa taifa hata mzee Ibrahim Kaduma jana kasikika akisisitiza jambo hili.
 
ifike wakati watanzania tuone na kutaka kwa lazima utawala bora wa sheria nchimi mwetu. Pia kila mtu kwa nafasi take atambue na kuzingatia hilo. (for the greater good of the nation)
Baraka ya....
 
Kama uko nje ya Kanisa Katoliki siyo mtu muhimu lkn kwa Wakatoliki bilioni 1.23 ni Mkuu wao na maamuzi yake yanaathiri maisha yao, hivyo usiunderestimate nguvu yake, kwa mfano mimi Bibi yangu Kijijini anasali kila siku kama Kardinali akisema kitu hawezi kuhoji wala kumpinga, kwa mfano Kardinali akimwambia achague CCM atafanya hivyo kwake yeye ni mtumishi wa Mungu sasa watu kama Bibi yangu wako wengine Tanzania!
Bado sana wewe
 
Padri Mcharo,

Mkubwa Tumia Ustaarabu unapoongea kuhusu dini za watu sio kama vile unazungumzia siasa
tabia yetu sisi binadamu huwa tuna focus kwenye makosa siku zote na hatuangalii yale mema yanayofanyika em tutumieni upeo WA fikra yakinifu tulizonazo
 
Kwahiyo Baba Askofu anausaliti/kuukana rasmi Waraka wa Kanisa Katoliki wa mwaka 2009?! Kwenye waraka ule, Sehemu ya Kwanza ya Vipaumbele Katika Sera ilihusu Hadhi ya Utu wa Mwanadamu. Sehemu ya Pili ilihusu Marekebisho ya Katiba. Sehemu hiyo ilisema:

2) Marekebisho ya Katiba

Katiba inaeleza Mkataba Msingi wa Kijamii wa watu kuhusiana na namna ya kujipanga katika maisha yao ya pamoja. Katiba ni zaidi ya hati ya kisheria. Ni dira ya kimaadili na maelezo ya kifalsafa ya tunu na kanuni watu wanazotaka kuzizingatia katika maisha yao ili kuwahakikishia amani, haki na vile vile kuheshimiana na kuvumiliana katika kuwa na maoni tofauti. Hakuna chama cha kisiasa wala serikali ya wakati huu wanaoweza kihalali kutumia Katiba kwa faida zao za kisiasa.

Katiba inamilikiwa na watu na ni ya watu katika anuwai (diversity) na katika upokeaji wa watu wenye tofauti mbalimbali (plurality). Kwa kuwa taifa ni kitu kinachoishi ni jambo la kiasili na la muhimu hivyo ni sharti kuruhusu mapitio ya vipindi kwa vipindi yafanyike ili kuwapa watu fursa kueleza maoni yao. Haifai kuachia kundi moja kushinikiza au pande/kundi/chama chenye maslahi (kijamii, kiuchumi au kidini) kuchochea mabadiliko. Tangu Tume ya Nyalali imetoa ripoti yake (1991), ombi la marekebisho ya Katiba halijapokelewa kwa namna na kiwango cha kuridhisha. Kuhusiana na suala hili tungependa masuala haya yapewe kipaumbele:
- Tamko dhahiri juu ya tunu msingi za maadili ya kitaifa ambayo yapasa yazingatiwe katika mchakato wa kurekebisha Katiba.
- Pana haja ya kuunda Baraza la Mapitio ya Katiba. Katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kuna njia kadhaa za kuwezesha suala kutekelezwa: Mahakama ya Kikatiba, Chamba ya pili katika Bunge, Mkutano wa Katiba.
Tunapendekeza paundwe baraza la wazee, wanaoteuliwa na sekta za kijami, ama wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo hiki kingechaguliwa na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake kulingana na Katiba yenyewe. Kiwe huru, na kisibanwe na serikali.


I like this country....
 
Ya Pengo naye ni maoni yake binafsi kama ya Niyomugizi.
Kila mtu ana maoni yae binasi hata Warioba na wengine.
Maoni ya Watanzani hupatikana kutoka kura ya maoni
Wakuu, nionavo mie tatizo si akisemacho Pengo ila ni wale waliomuhoji kutaka afafanue kauli ya Askofu Niwemugizi. Ladba walitumwa ila ingekuwa jambo la busara kupata ufafanuzi wake yeye mwenyewe Askofu Niwemugizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom