Pengo kapofushwa na nani,kwa nini hakuyaona haya?!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,760
102,109
Mtu mkubwa na mwenye heshima nzito ya kiuongozi na kiimani anapozungumzia mustakabali wa nchi hutakiwi kuzungumzua juu juu.Unatakiwa kuzungumza kwa mapana na kwa utulivu wa hali ya juu kwa kuwa wewe ni mtu unayetiliwa maanani zaidi kuliko kina siye

Nimemsoma na kumsikiliza Kardinali Pengo akiifagilia serikali ya Magufuli,na kwamba kwa awamu hii masikini wamepumua na kwamba hata mtu wa kawaida anaweza kutumia usafiri wa ndege za ATCL.

Nimesikitika sana.........lakini nimepata somo kwamba ni marufuku kumuamini mtu yeyote isipokuwa Mungu aliyee juu ya yote

Mpaka mwaka 2016 unaisha Watanzania bado hatujatulia,mambo mengi ya kuudhi na kushangaza yametokea mwaka huu. Orodha ya mambo Haya ni ndefu sana nitaorodhesha baadhi.Nachoshangaa ni kwa nini kiongozi huyu mkubwa wa dini hakuyaona kama ni maswala yanayowakwaza wanakondoo

1.Maumivu ya wahanga wa tetemeko kukosa misaada tegemewa
2.Idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo kukosa mikopo
3.Kubinywa kwa demokrasia ya vyama kinyume na katiba
4.Kutokuwa na uelekeo wa kupata katiba ya wananchi
5.Kubinywa kwa Uhuru wa kujieleza
6.Kupotea kwa Kijana Ben Saanane
7.Ukiukwaji wa haki za Binadamu waliosemekana ni wahamiaji haramu waliozikwa kwenye sandarusi
8.Kutokuheshimiwa kwa Bajeti iliyopitishwa na Bunge.
9.Wabunge wa CCM kuhusishwa na rushwa ya 10m kula mmoja
10.Msakabali wa Zanzibar na chuki za kisiasa
11.Mazingira mabaya kwa atumishi wa Serikali
12.Haki za watumishi walisitishiwa ajira zao
13.Matumizi mabaya ya jeshi la Polisi.
14.nk nk nk
 
Mkuu sasa wewe ulitegemea Pengo ataikashifu serikali? Anaisifia tu maana hawezi ukata mkono umlishao
 
mkuu tambua kwamba watumishi wa Mungu si Malaika. Ni Binadamu na Binadamu Uwa na Mapungufu yake.

Napia Ana Uhuru wa Kushabikia Upande wowote katiba ina Mruhusu.

Hivyo Maoni yake ya Unafuu wake wa Kupanda Bombadia Uheshimiwe Tusimhukumu Mawazo Yake.
 
Anataka Rugemalila akatupie tena mkombozi bank.
Chezea noti wewe!!!
Ukadinali woote kautoileti pepa.
 
Serikali iliona mbali sana ikaamua kupakata ofisi za imani kuu hapa Tz yaani Baa kwata yetu na Rich church yao (RC).
 
Mzee keshatembelewa mara mbili yule, Acheni Chongo aite kengeza;
Pengo aite mwanya!
 
Viongozi wa dini wanaposhindwa kusema ukweli na kuanza kuwa waongo ujue dola imeingia ndani ya dini!!!
 
In short Pengo alikuwa ametoka kusoma hayo maoni kwenye gazeti la Uhuru na yeye akaamua kuyasema maneno hayohayo mbele ya Rais.
 
Pengo ni mwana ccm mtiifu....lazima aifagilie serikali pia ndie mshauri wa JumaPondamali......FJ
 
Tusisahau fact kwamba Pengo ni mwanadamu na ana mitazamo yake pia. Kwa namna moja au nyingine matamshi yake hayajitoshelezi kumuhusisha na serikali, ni kama katika mijadala ya hivi karibuni ambayo ilidaiwa kulenga serikali lakini wahusika wakakana suala hilo, sioni sababu ya kumuweka Pengo katika mtazamo wa kisiasa zaidi bali katika mtazamo wa mienendo yake binafsi ya kimaisha. He is who he is, ana haki ya kujieleza kile anachojiskia na anacho amini ili mradi haingilii uhuru wa watu wengine. My perception is not of political view rather it's based in personal freedom of expression and speech.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom