Pengo aionya CCM: 'Usafi' wa Nyerere si wa chama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pengo aionya CCM: 'Usafi' wa Nyerere si wa chama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 14, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  • ASEMA ‘USAFI’ WA NYERERE SI WA CHAMA

  na Hellen Ngoromera

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinari Pengo, amewaonya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuingilia mambo ya imani ya Kanisa Katoliki katika mchakato wa kutangazwa Mwalimu Julius Nyerere kuwa Mwenyeheri.


  Akizungumza baada ya ibada ya kuwaombea wafiadini iliyofanyika katika kituo cha Hija Pugu, jijini Dar es Salaam, Pengo alisema viongozi wa CCM wanaodhani kuwa Mwalimu Nyerere akitangazwa kuwa Mwenyeheri kutakifanya chama hicho kionekane kitakatifu mbele ya jamii wanajidanganya.

  “Iwe ni kwa Mwalimu, iwe kwa Sista Mbawala, tuondoe wazo lolote la kusema Sista Mbawala akitangazwa Mwenyeheri sisi Wangoni tunatukuka. Hiyo hapana, huo si utukufu wa Wangoni ni utukufu wa Kanisa.


  “Tusianze kusema Mwalimu akiwa mwenyeheri manake sisi CCM tumetangazwa watakatifu. Hii si shughuli ya kisiasa, wala akitangazwa usiseme sisi familia ya Nyerere tuko kwenye heri. Wapi! Nani kakwambia wote mko wenye heri? Nayataja haya mambo kwa sababu yanajitokeza sana,” alisema.


  Bila kutaja jina la kiongozi yeyote wa CCM, na mahali alipotamka maneno hayo, Kardinali Pengo alisema kuwa ni jambo lisilopendeza kwa chama hicho kuingilia mchakato huo na kwamba hali hiyo inakwamisha kumalizika mapema kwa suala hilo.


  Pengo aliongeza kuwa endapo CCM itajivunia kwamba Nyerere ni Mwenyeheri wa CCM vyama vingine vitakuwa na sababu ya kutangaza kwamba chama hicho hakina heri yoyote ndani yake na kwa hiyo kitaleta ugumu kwa mwalimu kufanikisha jambo hilo.


  Alisema badala yake cha muhimu kinachotakiwa kufanywa na Watanzania ni kumwomba Mwenyezi Mungu kuwezesha mchakato huo kufanyika kwa mafanikio.


  “Tunaloweza kulifanya ni kumwomba Mwenyezi kufikia mafanikio wa yale tunayotamani kufikiwa kwa sababu yeye ndiye anayeweza kuliwezesha hilo na si nguvu wala mbinu zetu za kibinadamu,” alisema Mwadhama Pengo.

  Aliwataka Watanzania na waumini wa kanisa hilo kuacha michakato hiyo iende kwa mpangilio wa kanisa bila kuingiliwa na wanasiasa ama mtu yeyote.

  Alihoji: “Tusianze kusema aah Mwalimu hawezi kutangazwa Mwenyeheri bila maombi yangu, bila nguvu zangu sijui za kitu gani…wewe nani?”

  Alieleza kuwa mara nyingi shughuli zozote za michakato ya aina hiyo huingiliwa, jambo ambalo badala ya kusaidia huleta uzito kwa kanisa.

  Alimshukuru Askofu wa Shirika la Wamisionari Wabenedictine wa Mtakatifu Ottilie, Abate Anastas Rasier, ambaye ndiye aliyetoa mahubiri katika ibada hiyo kwa jitihada wanazoendelea kuzifanya.


  Alisema cha muhimu ni suala hilo kuendelea kwa mpangilio na msimamo wa Kanisa Katoliki.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. P

  PACHOTO JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  mwenyeheri? alikuwa mwanasiasa au mwanadini aliyeuangamiza uislam tanzania kisawasawa
   
 3. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Acha udini ndugu povu la nini kwa yasiyo kuhusu?Waache wakatoriki wafanye mambo yao kwa imani yao ilimradi hayaingilii uhuru wako na sisi wengine,na pia hawavunji sheria ya nchi.Hii ni kama Waislamu walivyoruhusiwa kuanzisha mahakama yao ya kadhi bila kubugudhi wengine.
   
 4. P

  PACHOTO JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  suala sio udini, ninachokifahamu nyerere alikuwa mwanasiasa, hivi kwenye siasa kuna uenyeheri? au ndio mambo yaleyale ya COBA( CATHOLIC OLD BOYS ASOCIATION)
   
 5. N

  NIMEKIMBIA CCM Senior Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pachoto njoo katoliki,2kubatize then 2kufundishe maana ya kutangazwa mwenye heri na ha2a zinazotakiwa kufuata,huwa catholic hawakurupuki,lasivo utaishia kulaumu wakati wenye imani n wengne
  "NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA NA WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA"sina haja ya kuelezea ni kansa lp hlo ila ntakuambia maneno hayo aliambiwa petro na yesu mwenyewe na petro ndo kiongoz wa rc,any way Mungu atakuokoa kwa wakati wake,
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Pengo ana lake jambo. Kwanini asijipambanuena kuweka bayana na kuchagua jimbo la kugombea kama anataka siasa?

  Ameshafahamika na hana jipya zaidi ya kumpa support Padre kuwa rais ili aongoze nchi kwa remote control.

  Na vipi kashfa yake ya kuuza madawa ya kulevya ameimalizaje?

   
 7. w

  wail Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere hana usafi hata mmoja isipokuwa kuuwa viongozi waliokuwa against na yeye
   
 8. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na usafi wa Nyerere si usafi wa Viongozi wa Kanisa katokiki au kanisa lenyewe ieleweke hivyo pia.
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Haya yote ni matunda ya Nyerere sasa huo usafi wake sijui upo wapi, Pengo bana
   
 10. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  sio lazima uchangie kama huna cha kuchangia, unaweza ukasoma tu na usitie neno...
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145

  Pengo kumbe anajihusisha na biashara ya mihadarati.....!sasa anapata wapi ujasiri wa kuikemea ccm?kumbe ndio mana alitudanganya kipindi kile kwamba ameoteshwa ya kwamba kikwete ni chaguo la mungu,kumbe alikua anatumika na mafisadi!
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Miafrika bana ndivyo ilivyo!

  Wewe kama nani humu JF kupangia watu? Nakushauri fungua forum yako upangie watu waandike unachopenda wewe, JF ni huru kila mtu ana haki ya kuchangia chochote kama anafuata sheria na kanuni za JF.

  Kweli leo ndio nimeamini wewe ni Mkuu wa chuo cha wehu!
   
 13. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Siamini ktk imani na taratibu za kikatoliki lakini unaweza kujibiwa hivi; KAMA KWELI aliua, Musa, Joshua, Daud na wengineo wote waliua... au uongo?! mtume muhamad je hakuua??? Ubaya au uzuri wa hili suala ni kuwa Sisi wengine wooote tusio wakatoliki hatuwezi kuwazuia wakatoliki kufanya kile wanachotaka kukifanya! Kwa sababu hakihitaji ruhusa wala msaada wa mtu mwingine yeyote nje ya wakatoliki wenyewe..
   
 14. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama Kawawa, Mwinyi na Jakaya hawana dini kaa kimya ndugu. Nyerere alikuwa mkristu wa madhehebu ya kikatoliki. Na kwa mila zetu, mkatoliki mwenzetu anayefuata dini vema hadi kifo chake, tunamtangaza mwenye heri na tunaamini hivyo. Kama sio mkatoliki, hayakuhusu mambo haya na ndicho Pengo alichotaka CCM iache kujihusisha na utakatifu wa Nyerere kwa sababu sio utakatifu wa kisiasa bali wa kidini.
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo mlidanganywa?! Unataka kusema kikwete ni chaguo la shetani??? Farao mwenyewe alikuwa chaguo la Mungu (aliwekwa kwa kusudi maalum) sembuse kikwete?
   
 16. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mkatoliki kama siyo mkatoliki ni Muislam ondoka kwenye hii hoja ila siku Wakitangaza waislam kumtangaza Nyerere kwa lolote lile pinga hili suala kwa nguvu zako zoote maana linakuhusu!!!
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  Deal with issues dont deal with personalities
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mshindwe kwenda shule mkikazania juuzuu mseme aliwaangamiza?
   
 19. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  1. Jimbo gani tena wakati tayari ni mkuu wa jimbo kuu la Dar es salaam? Unamjua au unamsikia Pengo? Ndiye mtanzania pekee mwenye kufahamika wazi kuwa na uraia wa nchi mbili na hakuna anayemsumbua (badala yake mnamsumbua mtu mdogo kama Nyalandu). Ni sawa na mbunge katika baraza la Vatican so hahitaji ushauri wa barux2 kutafuta jimbo. Duniani ana heshima kubwa zaidi ya rais wako JK au Shein. Anaendesha mradi mkubwa wa elimu na afya kisiwani Mafia na kuwahudumia maelfu ya waislamu na hata serikali imekiri bila Pengo hali ya kisiwa cha Mafia ingekuwa ngumu. Sasa wewe ***** unaropoka nini?

  2. Mtu yeyote mwenye akili timamu alimuunga mkono Dr Slaa uchaguzi uliopita. Sasa tusiongelee uliopita bali tuongelee uchaguzi ujao. Kama Pengo angelikuwa mchadema asingelipinga maandamano ya chama hicho. Hili ameliongea juzi juzi (x-mas) kuwa haki isidaiwe kwa maandamano.

  3. Kama anauza dawa za kulevya unashindwa nini kwenda kumkamata? Mbona yule askofu wa kilokole tayari yuko jela? Acha upupu bana!
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Suala la kumtangaza Mwl Nyerere mwenye heri ni suala la waKatoliki kwangu mimi amabaye si mkatoliki halina mashiko kwasababu Imani yangu inatofautiana na ukatoliki sana.Napata taabu sana kwasababu kuna watu wasiofuata Imani ya kikatoliki wanajaribu kuingilia Imani zisizowahusu.

  Mwl Nyerere akiitwa mwenye heri,Mtakatifu,Mtume,Nabii na nk kama wewe si mkatoliki pili pili usoila inakuwashia nini ?.Haya ni masuala ya Imani wapo watu wanaabudu Ng'ombe,wengine Sanamu,wengine wanaabudu watu tatizo liko wapi nni kakulazimisha kuamini au kuabudu Ukatoliki.
   
Loading...