Pengine ni agizo la kamati ya kampeni, Magufuli aiga tena 'Safari ya uhakika' ya Lowassa

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,651
2,627
Wanaukumbi.

Nimeamka mapema sana leo nikiwa na karedio kangu pembeni huku nachuma kahawa muda mfupi uliopita,sikujua kama nasikiliza RFA.

Ghafla nikawa nawaza bei na umuhimu wa kawaha miaka ile, kurejesha mawazo katika spika nikawa nasikia sauti ya mtu akiomba kura ya urais katika tangazo maalum bovu bovu hivi, nikajiuliza duh, mmasai siku hizi ana sauti kama ya Pombe?

Kuna maneno haya nimesikia,'mama ntilie, bodaboda, MABADILIKO YA KWELI, TWENDE NA SAFARI YA UHAKIKA' Kumbe ni sauti ya Magufuli.

Sasa yaonesha dhahiri CCM imezidiwa, na pengine mgombea ameshauriwa na kamati ya kampeni kuiga kila kitu cha Lowassa na Chadema kwa maana wanayojua wao.

Ukweli ulio mchungu ni kuwa Magufuli anazidi kujimaliza, kwani igaiga yake inampaisha Lowassa.

Kule Vunjo tayari ameshammaliza mgombea wa CCM
 
Bavicha at its best!

Huoni kama kujimaliza kwa magufuli ni sherehe kwako!

Kwa hiyo unataka asijimalize kisiasa?

Hutaki Lowassa ashinde Urais wa Tanzania?
 
Bavicha at its best!

Huoni kama kujimaliza kwa magufuli ni sherehe kwako!

Kwa hiyo unataka asijimalize kisiasa?

Hutaki Lowassa ashinde Urais wa Tanzania?

Mtanzania wa kweli anapenda kuwepo na upinzani wa kweli, sasa atafurahiaje Magufuli kujimaliza kabisa kisiasa?
Sasa yeye anaukosa urais anataka na wabunge nao wakose awape TLP? Huyo sasa ni adui wa CCM pia.
Tunataka CCM ijipatie hata wabunge 50 ili waipeleke puta serikali ya Ukawa isilale
 
Acha aendelee kuiga kila kitu, anazidi kudhihirishia wananchi kuwa yeye na ccm yake ni wasanii.
 
Kiukweli kabisa Magufuli kaharibu kabisa taswira ya kampeni za CCM, sehemu kubwa ya wanaCCM mwaka huu wanashindwa kuelewa ni nini cha kuamua.
 
Tattizo lake anaongea sana majukwaani hadi anakosa cha kusema anajikuta ameiga vya watu
 
Kuna video clip nimeona Magufuli anazungusha mikono ishara ya mabadiliko alivyokuwa Same anamnadi Ane kilango Malechela.
 
yeye anahisi kuwa anaconfuse wapiga kura ila badala yake anajiconfuse mwenyewe
 
Wanaukumbi.

Nimeamka mapema sana leo nikiwa na karedio kangu pembeni huku nachuma kahawa muda mfupi uliopita,sikujua kama nasikiliza RFA.

Ghafla nikawa nawaza bei na umuhimu wa kawaha miaka ile, kurejesha mawazo katika spika nikawa nasikia sauti ya mtu akiomba kura ya urais katika tangazo maalum bovu bovu hivi, nikajiuliza duh, mmasai siku hizi ana sauti kama ya Pombe?

Kuna maneno haya nimesikia,'mama ntilie, bodaboda, MABADILIKO YA KWELI, TWENDE NA SAFARI YA UHAKIKA' Kumbe ni sauti ya Magufuli.

Sasa yaonesha dhahiri CCM imezidiwa, na pengine mgombea ameshauriwa na kamati ya kampeni kuiga kila kitu cha Lowassa na Chadema kwa maana wanayojua wao.

Ukweli ulio mchungu ni kuwa Magufuli anazidi kujimaliza, kwani igaiga yake inampaisha Lowassa.

Kule Vunjo tayari ameshammaliza mgombea wa CCM

Hujaeleweka mjomba labda urudie
 
Kasuku ataelewa vizuri kama jana aliangalia Bongo Star Search.Maana mtangazaji alijitoa ufahamu na kusema"hapa kazi tu" na hapo ndipo balaa la wanamabadiliko lilipoukumba ukumbi kwa kelele za peopleeeeeeeeeessssssss na mabadilikoooooooooooooooooooo.Pia angewaona yamoto bendi walivyochuniwa na mashabiki mpaka wakaanza kutia huruma kisha baadae wakarudi tena hali ikawa mbaya mpaka alipoingia yule chiba ndio watu wakaingiwa huruma kidogo.
 
Magufuli alipopitishwa Dodoma mimi nilipledge kumpa kura na niliandika hata humu. Ila alinitibua na ilani yake ya milioni 50 kwa kila kijiji na tangu hapo sijataka hata kuisoma.
 
Yaani ukiitazama hiyo sehemu ni kama pumzi imekata...

Huyu si Magufuli tunayemfahamu...

Kuna video clip nimeona Magufuli anazungusha mikono ishara ya mabadiliko alivyokuwa Same anamnadi Ane kilango Malechela.
 
Ndio kawaida yao.... Bado kubadilisha jina na kuitwa ......... Ngoyai Lowassa
Mwisho wa siku atawaambia Watu "chagua CHADEMA" Kama yule mama kule Chalinze aliyesema "maendeleo ni ndani ya CHADEMA" kwenye kampeni za Ridhiwani...
 
Back
Top Bottom