Pengine makusanyo haya ya sadaka na mavuno yanawasahaulisha Kardinali Pengo na Mapadre wengine.Tuwakumbushe kuwa waumini tupo ktk mtanziko wa kiuchumi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Kauli za wazee wa kanisa,hasa kanisa katoliki kwa siku za karibuni zimetushitua wengi.Kauli za maaskofu mpaka mapadre walio chini yao.Hawa wote kama viongozi wa kiroho wanaoongoza wananchi wenye itikadi na mlengo tofauti,Kauli zao zinatustua,hasa sisi ambao ni waumini wao.

Hata katika mazingira ambayo haki inaokana kutokutendeka,hawa wazee wanapongeza tu.Tunapolalamika hali ya maisha imekuwa ngumu,wao hawapo na sisi.Sisi waumini tumebaki peke yetu.

Weekend hii nilihudhuria "Makusanyo ya Mwaka wa Mavuno Jimbo la Dar es Salaam".Makusanyo ya dekania zote,toka kwenye parokia kamili na parokia tarajiwa.Tumevuna kwelikweli...na pesa hizi zinakwenda kulitegemeza jimbo.Makusanyo haya hayana kodi,maana ni mali ya kanisa.Hili pia linaweza kuwa moja ya jambo linalofanya hawa watu wa kanisa wajisahau na kuona huku mtaani waumini wao maisha ni raha mustarehe

Pengine mavuno haya yanawasahaulisha hawa viongozi wetu,basi kupitia jukwaa hili nataka kuwaambia hawa mababa kuwa maisha ni magumu sana,milo mitatu ni huku kwa waumini wao ni kwa kubahatisha,wanapopata nafasi ya kukutana na mfalme au wasaidizi wa mfalme,basi wasimamie ukweli,wasimame na waumini wao.Wasione soni katika kukemea rushwa,uonevu,mauaji,ukiukwaji wa demokrasia na kudumazwa kwa siasa za ushindani.Hivi kweli muitikio wa leo katika uchaguzi wa serikali kanisa hili la Khalifa wa Mtume Petro linaona ni sawa tu!!?

Sisi waumini tunapokusanya mamilioni haya na wakati mwingine mpaka kuvuka kiwango,hawa mababa zetu wa kiroho waadhani tuna maisha mazuri sana,labda tuna pesa na tunaridhika na mfumo wa uchumi unavyokwenda kwa sasa.Wanajisahau na kuwa upande wanaopaswa kuukosoa kwa hekima,wanafungamana nao na kutusahau sisi tunaohitaji sauti zao na kauli zao katika mimbari zitusemee.

Angalisema Pengo peke yake tusingeshangaa sana,lakini sasa mpaka maparoko wameanza siasa kwenye mahubiri,wanaanza kampeni,wanaona kila jambo ni shwari na maisha ni sawa sababu waumini tunatoa mavuno yanayopita kiwango tulichojiwekea.

Mfano huu ni wa mavuno kwa Jimbo la Dar es Salam tu,tumevua mamilioni,labda ndioyanawsahaulisha hawa mababa nawanahisi tuna maisha mazuri tu.

MAVUNO JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM.

DEKANI YA KIGAMBONI Tsh 263,226,750

1. KIGAMBONI 18,830,645
2. MBAGALA. 14,252,535
3. KIJICHI. 55,000,000


DEKANIA YA ST. JOSEPH Tsh 49397550/489,622,220

1. ST. JOSEPH. 216,250,210
2. UPANGA. 40,000,000/
3. MSIMBAZI. 61,300,00


DEKANIA YA GASPAR. Tsh 404,768,100/ 418,180,510

1. GASPAR. 53,164,300
2. TEGETA 12,673,700
3. BOKO. 31,000,500
4. SALASALA 20,126,550
5. T. MORE. 27,453,400
6. KUNGURU. 14, 968,000/

DEKANIA YA PETRO.
Tsh
532 670,575/ 489,823,712

1. PETRO. 153,51000
2. MIKOCHENI 32,000,000
3. MWEGE 70,272,500
4. SINZA. 48,260,000
5. MAGOMENI. 41,500,000

DEKANIA YA. UBUNGO. 278,816,650/ 300,301,000

1. UBUNGO 15,314,000
2. MANZESE. 43,000,000
3. MAKUBURI 27,338,000
4. C.KIKUU. 40,000,000

DEKANIA YA UKONGA 251,750,950 / 265,500 090

1. UKONGA 76,000,000
2. PUGU 35,275,000
3. KIWALANI 14,000,000
4. VITUKA 16,700 600
5. KITUNDA 36,523,770

DEKANIA YA SEGEREA. 270,176,700/ 254,827,050

1. SEGEREA. 43,631,700
2. TABATA. 102,213,850
3. KINYEREZI 16,800,000
4. KIPAWA. 30,452,300
5. KIMANGA. 15,000,000

DEKANIA YA KIBAHA. 145,532,050/ 161,976,300

1. KIBAHA 31,000,200
2. MLANDIZI 14,000,500
3. MKUZA. 14,000,000
4. KIBAMBA 23,390,500
5. KIBWEGERE. 28,000,000


DEKANIA YA KILIMAHEWA. 36,749, 100/ 37,309,850

1. KILIMAHEWA 5,573 700
2. MKURANGA 12,108 250
3. KIBITI 3,500,000

DEKANIA YA MBEZI LUIS. 257,613,300 /293,962,900

1. MB/LUIS 25,334,300
2. MAVURUNZA 68,100,250
3. TAGASTE. 27,000,000
4. TEGETA A 9,122,000

Makusanyo kama haya,ninadhani ndio yanawasahaulisha watu kama kina Pengo na Mapdre wengine,maana sasa wanafungamana na upande ambao bila shaka unawafanya waon udikteta ni bora kuliko utawala wa sheria.Kwenye kanisa ambalo ndani yake kuna watu weye fikra na itikadi mseto,viongozi wa kanisa mnapaswa kuchun sana ndimi zenu.


Juzi kati akiwa na RC Makonda,Muadhama P. Cardinal Pengo amewananga wanaoikosoa serikali ya awamu ya tano.Kwa tafsiri ya hotuba yake,ni kama Cardinal Pengo anasema kwake demokrasia si lolote kama tu watu wanaenda shule bure,wanajengewa barabara na hata kujengewa vituo vya afya.

Mwadhama ambaye kwa nafasi yake ni mmoja kati ya walio wachache wenye haki ya kikatiba pale Vatican kutuchagulia Papa ambaye ni khalifa wa mtume Petro na msimamizi wa kanisa katoliki lililo nyumba ya imani ya mabilioni ya watu duniani.

Pengo akavuka mipaka,akasema hata Hitler na Musolini walikuwa watu wema,maana udikteta wao ulileta maendeleo.Akasema kwa lugha ya kificho kuwa hata wale wayahudi dunia inayoambiwa waliuawawa na Hitler,si lolote ukilinganisha na maendeleo aliyoleta.Yaani kwa tafsiri ya juujuu,Pengo anasema hata Rais fulani akiuwa,akipoteza watu kwa njia ya watu wasiojulikana,akipiga watu risasi hadharani,akiminya demokrasia na kuharibu mifumo mizuri ya utawala wa kisheria,maadamu mtu huyo anatujengea shule na mabarabara,basi mtu huyo ni mwema,anafaa,na yote anayofanya katika kunywa damu za watu ni kama "kosa lenye heri".Pengo haamini katika utawala wa sheria,anaamini katika falsafa ya maguvu inayoleta "maendeleo".

Unaposika maneno haya toka kwa gwiji wa "Moral Theology" roho inakuuma sana,haya hayakupaswa kuwa maneno yanayotoka katika kinywa cha mtu aliyekaa darasani na kufungua kurasa za vitabu vya kina St.Thomas Acquinas ambao wameelezea kwa undani juu ya "Justice and Society".Pengo ni mwalimu na gwiji wa "Moral Theology",anapata wapi nguvu za kukana elimu yake kwa kuona "udikteta" ni bora kuliko utawala wa sheria??.Ninamkumbusha mwalimu wangu Cardinal Pengo kuwa "In civilized life,Law floats in a sea of ethics".Kwa gwiji wa moral Theology kama Pengo,huu si msemo mpya kwake.Leo Muadhama ni wa kuunga mkono udikteta dhidi ya utawala wa sheria?

Walatini wanasema "Legum servi sumus ut liberi esse possimus" i.e "We are slaves of law in order that we may be able to be free".Pengo awahimize marafiki zake wanaomtumia,na wawe watumwa wa sheria,maana utumwa wa sheria humuweka mtu kuwa huru.

Hatuwezi kusifia uvunjifu wa haki za binadamu,kudidimia kwa utawala wa sheria,kulegalega kwa haki ya kukusanyika na kupotea kwa misingi ya uchaguzi huru na wa haki eti kwa mbadala wa ujenzi wa majengo ya hospitali na baabara.

Mtakatifu Thomas Aquinas alisema "He who is not angry when there is just cause for anger is immoral. Why? Because anger looks to the good of justice. And if you can live amid injustice without anger, you are immoral as well as unjust"
 
Pengo hajawahi kuwa mnyenyekevu katika maisha yake. Pengo ni mjivuni na mjeuri, Pengo yupo tayari kwenda kinyume cha kanisa ili tu asikike na ajadiliwe yeye. Pengo ameamua yeye ndiyo awe mjadala badala ya kuibua mijadala.
Wapumbavu wachache ndani ya kanisa na baraza la Maaskofu (TEC) wamejikuta nao wanatamani kualikwa na kula mezani pa watawala, hivyo wameona nyayo za Pengo ndiyo sahihi kufuatwa ili na wao waalikwe mezani.

Kanisa linapaswa sana lijitafakari badala ya kubeba msalaba limeamua kumuachia msalaba huo Simeone Mkirene (Waumini)
 
Umeandika vizuri sana na data kabisa ambazo ni researched.

ILA, umechelewa kujua kuwa Pengo alishakengeuka muda mrefu na pia akili yake inachoshwa na kina Makonda na Uzee pia.

Anaongea mpaka anatia huruma.

Kuanzia pale aliopata Mgao wa Escrow akazidi kujipendekeza kwa wenye dola ili atetewe.

Kardinali Pengo sio yule wa 1999 aliyemzika Mwl. Nyerere.
 
....wewe mtu sijui una matatizo gani, waumini wameamua kwa mapenzi yao kutoa kile walichonacho, wewe kwa mapenzi/ mtazamo wako ndio unaleta mambo ya siasa kwenye hili suala. Sijaona sababu ya msingi ya wewe kuanzisha hii mada, maparoko na Kadinali Pengo wana maamuzi yao, wao wanaamua ni wakati gani waongee jambo gani, sasa wewe mbona ndio unaingilia uhuru wao wa kutoa maoni kwa kutaka waongee kile unachopenda?, kama unaenda kutoa sadaka kanisani kwa shingo upande kwa sababu ya hali ngumu, acha kutoa, sababu Mungu hapendi kutoa sadaka huku umeukunja moyo!, wenzio wanatoa kwa mapenzi yao, wewe ndie unaepeleka siasa kanisani kwa kutaka wazungumze unachotaka wewe, na hiyo sadaka unayotoa my friend huku umekunja moyo kwa Mungu haikubaliki, bora uache tu.

....very funny, kumbe unajua kanisani kuna watu wenye itikadi mseto, then unataka wazungumze unachopenda wewe!, aisee...
 
Haya mambo yanafikirisha sana....
Mungu atusaidie sana. .. bado muda si mrefu kuna shukrani.....
Hela nyingi zinaenda ku fund lifestyle za hawa watu badala ya kuwasaidia masikini na wahitaji. ....

Utambuzi huu una atari kubwa sana kwa kanisa huko mbele...
Ulaya ilianza hivi hivi na sasa makanisa haya na watu
 
Haya mambo yanafikirisha sana....
Mungu atusaidie sana. .. bado muda si mrefu kuna shukrani.....
Hela nyingi zinaenda ku fund lifestyle za hawa watu badala ya kuwasaidia masikini na wahitaji. ....

Utambuzi huu una atari kubwa sana kwa kanisa huko mbele...
Ulaya ilianza hivi hivi na sasa makanisa haya na watu
.....inaonekana wengi humu hamna uelewa na haya mambo, jaribu tembelea Kanisa Katoliki kuna wazee wanalelewa, wenye ukoma na ulemavu mwingine wa viungo, usisikilize maneno ya mitaani ndugu kwamba sadaka inatumika kuwavisha na kuwalisha mapadri na maaskofu. Kuna makanisa na vigango huko ndani vijijini, kwa jumapili moja wanaweza kusanya elfu 20 sadak ambayo haitoshi kuendesha shughuli za kanisa, inabidi pesa itoke parokia za mijini kwenda kuhudumia za vijijini, tembeeni au ulizeni muambiwe.
 
.....inaonekana wengi humu hamna uelewa na haya mambo, jaribu tembelea Kanisa Katoliki kuna wazee wanalelewa, wenye ukoma na ulemavu mwingine wa viungo, usisikilize maneno ya mitaani ndugu kwamba sadaka inatumika kuwavisha na kuwalisha mapadri na maaskofu. Kuna makanisa na vigango huko ndani vijijini, kwa jumapili moja wanaweza kusanya elfu 20 sadak ambayo haitoshi kuendesha shughuli za kanisa, inabidi pesa itoke parokia za mijini kwenda kuhudumia za vijijini, tembeeni au ulizeni muambiwe.

Tena kama ndio hivyo inabidi watu wasitoe kabisa ili hao viongozi wajifunze.
 
Tena kama ndio hivyo inabidi watu wasitoe kabisa ili hao viongozi wajifunze.
Ni Bora wawape ili wachoke

 
Pengo hajawahi kuwa mnyenyekevu katika maisha yake. Pengo ni mjivuni na mjeuri, Pengo yupo tayari kwenda kunyume cha kanisa ili tu asikike yeye na ajadiliwe yeye. Pengo ameamua yeye ndiyo awe mjadala badala ya kuibua mijadala.
Wapumbavu wachache ndani ya kanisa na baraza la Maaskofu (TEC) wamejikuta nao wanatamani kualikwa na kula mezani pa watawala, hivyo wameona nyayo za Pengo ndiyo sahihi kufuatwa ili na wao waalikwe mezani.

Kanisa linapaswa sana lijitafakari badala ya kubeba msalaba limeamua kumuachia msalaba huo Simeone Mkirene (Waumini)
Kuna kila dalili Pengo anaweza akawa MCHAWI , kwao anakotoka uchawi ni jambo la kawaida sana , radi ya kutengeneza inauzwa hadi 1500/= , sasa ukichanganya na kauli zake ni uhakika kwamba huyu mzee ni kigagula .
 
Back
Top Bottom