Pendekezo/ Wazo: CCM anzisheni kampeni ya ‘tuzikomboe na tuzirejesha kura milioni 6 nyumbani, mwenye nazo karudi’.

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai kwangu binafsi, kwa familia yangu na kwa kila mtu kwa ujumla. Pia, naliombea taifa langu la Tanzania dhidi ya ukosefu wa Amani na mabaa ya asili. Pia, namuombea Rais wetu Mhe. John Magufuli na serikali kwa ujumla katika kutimiza majukumu yake ya kuliongoza taifa hili kwa mafanikio makubwa na uelekeo mzuri.

Nikijikita moja kwa moja kwenye mada baada ya hiyo shukrani na maombi mafupi. Napenda kuona kuwa mzee Lowassa amarejea tena kundini na akiwa na furaha tele na matumaini makubwa ya kuihakikishia CCM ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao. Kutuletea zawadi ya kura milioni 6 ambazo watanzania walimpgia wakati wa uchaguzi mkuu uliopita ni jambo la shukrani.

Shauku ya kila mtanzania hasa mwanaCCM ni kuona zile kura milioni 6 ambazo Lowassa alizoziingiza upande wa pili(UKAWA) mwaka 2015 ambazo ziliifanya CCM kutopata ushindi wa kishindo ila kwa zimekuwa ni ‘ investment’ nzuri kwa sababu zinarudi nyumbani na huo uwekezaji unatuhakikishia faida nzuri ya gawio na ndicho watanzania wanataka kuona kuwa ‘ is Lowassa an asset or liability to CCM ?

Kwa mtazamo wangu Lowassa ni ‘asset’ kwa CCM kwa sababu CCM haikupoteza kitu Lowasaa alipoondoka na hata alipoondoka ikaweza kushinda lakini kurejea kwake ni ‘ asset’ nzuri kwa sababu anatuletea mavuno makubwa ya kondeni alipoenda kukusanya na hivyo kuongeza idadi ya wapiga kura na wanachama wa CCM ambayo ndio ‘ Asset’ kwa chama cha siasa.

Hivyo, napenda kuchukua nafasi hii kutoa pendekezo langu juu ya kufanya ujio wa Lowassa CCM kuwa ‘asset’ kwa kuanzisha kampeni ya kitaifa kwa kila kitongoji, kijiji, kata, tarafa , wilaya , mkoa na kanda kushawishi na kuhimiza wle waliompigia kura lowassa mwaka 2015 kuzirejesha kura hizo nyumbani. Pia, kuwashawishi wajiunge na CCM kama walikuwa si wanaCCM au wanachama wa chochote cha siasa.

Kampeni hiyo iwe na lengo la kujenga chama na sio kumjenga mtu na Lowassa awe mstari wa mbele kwenye kampeni hiyo ya kiaifa akielezea umuhimu wa kuirejesha kura yake nyumbani kwa waliompigia kura . Kampeni ihusishe watu wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kushawishi watu kuzirudisha hizo kura milioni 6.

Ni ukweli usiopingika kwamba robo tatu ya kura za Lowassa mwaka 2015 ni za kwake na hiyo robo ndizo za ukawa, hivyo hizo kura million 6 zinatakiwa kurudi kwa mwenye nazo na waliompa hizo kura washawishiwe kuzirudisha.
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,113
2,000
Wewe ni kauzu kweli kweli...
Badala ya kuwashauri waanzishe kampeni kuwaletee watu maendeleo endelevu wewe bado unasubiri siasa za kukudanganya..!!
Watu wamekichoka hicho chama cha zamani..
Yaani hilo jinamizi limesababisha nchi ijiendeshe kwa kupiga kwaride la hatua 5 mbele na kurejea 15 nyuma..!!
Chama kilichoshindwa kuleta mapinduzi yoyote zaidi ya kuwapumbaza watanzania..!!
Aibu sana hii!!
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,303
2,000
Kwanza naomba uelewe kwamba watu waliwapigia kura UKAWA sio kwa sababu ya mtu mmoja bali ni kwa sababu ya kuwachoka CCM na utawala wao wa kiimla na bado msimamo wao ni huo huo. Kamwe msitarajie kuwa Lowasa ataondoka ma hizo kura milion 6. Mtasubiri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,189
2,000
Kwani hata hizo mil 8 walizipata? Si tuliambiwa ni goli la nkono vinginevyo EL ndiye angekuwa rais wa 5? Juzi si ndiyo ameitwa kwa maridhiano ili akubali hasara na aungane mwizi na yeye akakubali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
815
1,000
CCM ikiwa inafanya hivyo basi na upinzani (UKAWA) wuruhusiwe nao kuzunguka nchi nzima wakitaka kueleza umma sababu za kura milioni 6 zisivyotakiwa kuhama na aliyehama. Hapo ndio tutajua kura milioni 6 zilichagua tu mabadiliko au zilimchagua aliyehama.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,413
2,000
Mwaka 2015 watanzania walichagua mabadiliko na hawakumchagua Lowasa kwa sababu wengi tulikuwa tunamfahamu hakuwa mkamilifu. Mfano mzuri ni uchaguzi ujao, kama ungekua huru na wa haki; wapo watanzania wangekubali kulipigia kura jiwe dhidi ya mgombea kutoka ccm.

Kuna watu wameichoka tu ccm na siku zote tunaiombea ife na kupotea kabisa kwenye siasa za nchi hii , hivyo ni ngumu sana kupata kura za aina hii ya watu nikiwemo mimi.
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,995
2,000
Bora amerudi huko paliko tufikisha hapa kwanye siasa zisizofaa kwa binadam mwenye imani ya kumjua Mungu Muumba mwenye haki.

Ni jambo jema sana mana kwa sasa tunaweza kuwaambiwa:
Wapiga kura,
Waafrika na
Dunia nzima.
...Tunaweza Kuwaambia Marafiki zetu na wote wenye utu na uzalendo kuwa vita iliyopo mbele yetu ni ya kutafakari na kuchagua :
Kati ya Wema na uovu.
Kati ya dhulma na haki.
Kati ya utu na unyama.
Kati ya uzalendo wa kweli na uzalendo ubinafsi wa maslahi ya mishahara minono.
Kati ya maisha bora na kuwafukarisha watanzania.
Kati ya wizi wa kura na ulinzi wa kura.
Kati ya dharau na heshima.
Kati ya udikteta na demokrasia.
Kati ya mabavu na uongozi wa hekima .
Kati ya chuki na upendo.
Kati ya amani ya kweli na uchokozi.
Kati ya kujenga urafiki na kujenga uadui.
Ukweli na uongo.
Siasa safi na ugaidi wa kisiasa.
Kati ya Unyenyekevu na Kiburi.
Vita kati ya Upole na Vitisho.
Kati Kulinda uhai na Kuangamiza wenzetu kwa kutumia kodi za wote.
Mshikamano na kufarakana.
Utaifa na ubaguzi.
Kujidhili na kujikweza.
Katiba kandamizi(ya watawala) na katiba ya wananchi.
Uhuru na utumwa.

Kifupi dunia kuna vita mbili tu kati ya Mungu na shetani.
Ingieni kupitia mlango mwembamba.
Maana mlango uendao Motoni ni mpana nao waingiao humo ni wengi mana una mambo ya anasa na raha za dunia.
Ndio maana kwa sasa ni rahisi kabisa kiwaona wakubwa wakiwa walevi na wahuni wa kupindukia.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,113
2,000
Kwani hata hizo mil 8 walizipata? Si tuliambiwa ni goli la nkono vinginevyo EL ndiye angekuwa rais wa 5? Juzi si ndiyo ameitwa kwa maridhiano ili akubali hasara na aungane mwizi na yeye akakubali?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni watanzania wachache sana wataliona hili suala kwa jinsi unavyoliona..
Wengi wamepofuka.. ni vipofu na viziwi wa akili..!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom