Pendekezo: wazazi wa watoto omba omba wachukuliwe hatua kali za kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo: wazazi wa watoto omba omba wachukuliwe hatua kali za kisheria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Mar 15, 2010.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2010
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Yaani bila ya aibu, haya, wala soni, unakuta mijimama na mijibaba imebweteka kwenye kivuli, huku mingine ikiuchapa usingizi, wakati watoto wao (wengi wao chini ya miaka 7) wakihaha kwenye jua kali katikati ya barabara kuomba omba.

  Huku ni kuwadhalilisha watoto. Kama kweli hao wazazi wanahitaji misaada kwa nini wao wenyewe wasichakarike kugongagonga madirisha ya magari? Au ndio wamegundua kuwa watu uwaonea huruma zaidi watoto?

  Wizara inayohusika na watoto inapaswa kutoa onyo kali kwa wazazi hawa ili waache hii tabia. Wasiposikia, wapelekwe kwenye mikono ya sheria.
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu, wizara yenyewe unayosema mi naona inahandaika zaidi kutafutia wanawake ubunge wa viti maalum uongezwe.......... wamesahau kuwa wanayo dhaman aya kuokoa watoto hawa... na kwa kweli mi naona ndiyo jykumu la maana zaidi hata ya huo usawa bungeni na kwenye maeneo mengine....................... kuna nguvukazi kubwa sana na wataalamu wengi sana taifa linapoteza kwa kutowaingiza hao watoto shuleni eti kwa vile wazazi wao hawana uwezo............

  elimu ya msingi kwa mfanao sasa ni bure, japo kuna vijigharama vya unifmu nk........... lakni hili lingechukuliwa kama kichocheo na wadau wote kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kunza shle anaanza shule................... binafsi ningependa hata kuona hao wanaowapa watoto visenti kwenye madirisha ya magari wanaacha kufanya hivyo ili kuondoa incentive ya watoto kujipanga kutwa nzima mabarabarani kuomba magari pesa......... na wengine wanajifanya kukusaidia kufuta kioo vumbi ili uwape pesa................ hao wote ni ombaomba na walitakiwa kuwa shuleni na sio baranarani................... binafsi huwa naniuma sana............ na waziri mwenye dhamana hawezi kukwepa lawama kwa hili........... alipaswa kumshauri na kumsaidia rais kuhakikisha nammaliza suala la watoto hawa na kupeleka wote shuleni hata kwa msaada wa vyombo vya dola kama italazimu na kuwachukulia hatua kali wazazi wanaohusika na uhujumu huu wa nguvukazi na wataalamu wetu wa siku za usoni...............

  kila mdau awajibike............ mimi na wewe tuachekuanza sasa kuwapa hela............ na tuwabane wanasiasa serikalini na wawakilishi wetu kwenye vyombo vya maamuzi wachukue hatua................... tuanza sasa!!!!!!!!!................... tusiishie kulalamika tu..................... na kusema tunakereka............... tuanza kuchukua hatua na inawezekana...................
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ukweli mtupu Quemu nimevuta pumzi ndeefu sana wakati nikifikilia nini cha kufanya ..
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tatizo lipo kwenye Malango yao ya wazaliwa wa kwanza! Hawa watu tabia hii ya uvivu ipo damuni mwao.
  Na wizara husika imelala usingizi hapo tusitegemee chochote kufanyika.Toka mwzno kabisa aliyekuwa anajishughulisha na ombaomba ni Makamba lakini wenyewe hata kuunga mkono sijawahi wasikia.
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hata makamba mi naona alikuwa kaijshughulisha kisiasa zaidi............ sikuwahi kuona akija na approach ya kisayansi ya kumaliza kabisa tatizo hili............. kumbuka pia makamba alikuwa RC tu na hili ni tatizo la nchi nzima............... hapa wanaopaswa kuchukua hatua ya mbele kabisa ni wizara................ unfortunatelly wizara yenyewe imeelemewa na masuala ya usawa wa kijnsia imeesahau masuala ya watoto.................. nashanga wizara hii imekuwa na mawaziri wanawake siku zote................. lakini kusema kweli sijaona umakni wa wanawake hawa kwa suala la watoto............ kuanzia enzi za akina mary nagu/asha migiro na watangulizo wao mpaka leo akina mama sitta............ sijaona waziri aliyeshughulikia suala hili serious.............
   
Loading...