Shepherd
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 2,416
- 1,643
Kufuatia kuwepo tetesi, na uwezekano wakuja,na kuboreshwa kwa utaratibu wa kuchukua mafao pale mtu anapokoma ajira yake,Ingependeza sana watunga sera wetu na wapitisha mswada wetu, au kwa lugha nyingiwe Wawakilishi wetu,kwa wale ambao awajafikisha miaka 55 wanapostaafu au kufurushwa katika nafasi zao za ubunge na kisiasa,basi wasipewe mafao yao badala yake wapewe FAO LA KUTOKUWA NA AJIRA mpaka watakapopata ajira mbadala.Wao watakuwa mfano na kielelezo kizuri cha sheria na miswada wanayoipitisha.FAO LA KUTOKUWA NA AJIRA litawasaidia wasiteseke wakati wakitafuta ajira mbadala au wakingojea kufikiwa umri wa miaka 55.Kwa dhati pendekezo hili liingizwe kwenye hansard ya mchakato huwo kama aupo,tunawapenda sana wawakilishi wetu ambao wengine tunawaona baada ya miaka mitano ya ubunge wao majimboni.