Pendekezo: Viongozi wa vyama vyote na viongozi wa dini mkutane kujadili mada moja tu-haki katika uchaguzi huu. Baada ya hapo muwaombee wagombea wote

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
Waheshimiwa Viongozi wetu wa vyama na Wagombea,

Waheshimiwa viongozi wetu wa Dini zote,

Wadau wa uchaguzi.

Amani iwe kwenu.

Wapendwa viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa vinavyogombea urais mwaka huu, kwa unyenyekevu mkubwa ninaomba kutoa pendekezo kwenu, ikiwapendeza mkaufanyia kazi kabla ya Kampeni kuanza.

IKIWAPENDEZA, bila kuwa na muegamo wa kichama kwa upande wowote iwe kwa chama tawala au vyama vya upinzani, mkaitishe siku moja tu ya kuwapa wagombea hawa mada/somo likawe ni HAKI NA AMANI YA NCHI WAKATI WA UCHAGUZI. Mkawaombee wagombea wote kwa kutaja majina yao. Yaani mchakato mzima ukaanze na Mungu na ukakamilike na Mungu.

HAKI ni tunda la amani. HAKI hupaswa kuonekana kuwa inatendeka katika maisha yetu ya kila siku. HAKI inapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu. HAKI inapaswa itamalaki kwenye uchaguzi huu wa October 2020. Viongozi wetu wa Dini mna nafasi kubwa ya KUWEZESHA hilo kutokea.

Vyama vya siasa kupitia ule umoja wenu mnaweza kuratibu hili. Ama hata viongozi wa Dini wenyewe.

Nawasilisha

Potokaz
 
Back
Top Bottom