Pendekezo: Utunzaji wa garden za Dar, wakabidhiwe Jeshi

babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,643
3,299
Ni takribani miaka miwili sasa tangu barabara ya Mwenge-Bagamoyo ikamilike. Kwa wale watumiaji wa njia hii watakuwa mashahidi kwa kipande cha garden kutoka Makongo mpaka kituo cha magari cha super kilivo tengenezwa kwa ustadi.

Kazi hiyo yote imefanywa chini ya usimamizi wa jeshi la wananchi wa Tanzania na binafsi imenivutia na kunisukuma kuangalia garden nyingine ndani ya jiji la Dar es Salaam zinafananaje. Hakika sijaona garden iliyohudumiwa na kuvutia kama iliyopo katika kipande cha barabara tokea Makongo hadi Super.

Kuna haja halmashauri ya jiji akaangalia jinsi ya kuingia mkataba na baadhi ya vikosi kwa ajili ya kupendezesha mji huu kupitia bustani.

Ni hayo tu nilionayo kwa sasa na nikipata muda nitaleta baadhi ya picha za eneo hilo la barabara kati ya Makongo na Super.

Nawasilisha.
 
Ni takribani miaka miwili sasa tangu barabara ya mwenge bagamoyo ikamilike.Kwa wale watumiaji wa njia hii watakuwa mashahidi kwa kipande cha garden kutoka makongo mpaka kituo cha magari cha super kilivo tengenezwa kwa ustadi.

Kazi hiyo yote imefanywa chini ya usimamizi wa jeshi la wananchi wa Tanzania,na binafsi imenivutia nakunisukuma kuangalia garden nyingine ndani ya jiji la Dar es salaam zinafananaje..hakika sijaona garden iliyohudumiwa na kuvuta kama iliyopo katika kipande cha barabara tokea makongo hadi super.

Kuna haja halmashauri ya jiji akaangalia jinsi ya kuingia mkataba na baadhi ya vikosi kwa ajili ya kupendezesha mji huu kupitia bustani.

Ni hayo tu nilionayo kwa sasa,na nikipata mda nitaleta baadhi ya picha za eneo hilo la barabara kati ya Makongo na Super.

Nawasilisha.
Ili tupate maendeleo haraka naona ni vema tukawatumia hawa wajeda . Hawanaga longolongo.
 
Exactly...bustani nzuri sana ile.Kikubwa ni kuwa wanajeshi wanajituma na wanaijali bustani yao.Asikudanganye mtu bustani ni matunzo.Nyingine ni ile ya TCRA nayo imetunzwa vizuri.
mkuu hizi zilizopo katikati ya mji zinatia kinyaa,kuna moja naona imeanza tengenezwa barabara ya sam nujoma,,wameanza vizuri sana.
 
Kwa hiuo umeona Jeshi ndio la kutunza Bustani? Kama umeshiba sana nenda Kanye ulale.
sawa mkuu,ndo uwezo wa kufikiri ulipoishia ,kama ulikuwa hujui jeshi lina miradi mingi,,mfano dodoma kuna kikosi cha ihumwa wana vitalu vya mito na wanafanya biashara ya kuuza miti....
 
Ni takribani miaka miwili sasa tangu barabara ya mwenge bagamoyo ikamilike.Kwa wale watumiaji wa njia hii watakuwa mashahidi kwa kipande cha garden kutoka makongo mpaka kituo cha magari cha super kilivo tengenezwa kwa ustadi.

Kazi hiyo yote imefanywa chini ya usimamizi wa jeshi la wananchi wa Tanzania,na binafsi imenivutia nakunisukuma kuangalia garden nyingine ndani ya jiji la Dar es salaam zinafananaje..hakika sijaona garden iliyohudumiwa na kuvuta kama iliyopo katika kipande cha barabara tokea makongo hadi super.

Kuna haja halmashauri ya jiji akaangalia jinsi ya kuingia mkataba na baadhi ya vikosi kwa ajili ya kupendezesha mji huu kupitia bustani.

Ni hayo tu nilionayo kwa sasa,na nikipata mda nitaleta baadhi ya picha za eneo hilo la barabara kati ya Makongo na Super.

Nawasilisha.
Yaani kweli JWTZ wakabidhiwe bustani? Watakuwa wanalipwa au inakuwaje? Ina maana hawana kazi za kuwatosha au? Kama wanatunza za kwao si ni kwa sababu ni maeneo yao? Unatafuta kichapo bila shaka.
 
Yaani kweli JWTZ wakabidhiwe bustani? Watakuwa wanalipwa au inakuwaje? Ina maana hawana kazi za kuwatosha au? Kama wanatunza za kwao si ni kwa sababu ni maeneo yao? Unatafuta kichapo bila shaka.
kwani kampuni zinazotunza bustani zinalipwa ama zinafanya kazi bure???

ukipata jibu hapo manna yake katika miradi ya jeshi huu pia unaeza ukawa ni moja wapo ya mradi....
 
kwani kampuni zinazotunza bustani zinalipwa ama zinafanya kazi bure???

ukipata jibu hapo manna yake katika miradi ya jeshi huu pia unaeza ukawa ni moja wapo ya mradi....
Sizungumzii kampuni nazingumzia jeshi ambalo ni taasisi ya serikali.
 
Iko siku utasema na vyoo vya Stand wasafishe wanajeshi...Jukumu la usafi ni la kila mtu pamoja na wewe..
 
Nadhani tukiwapa hawa nyanja nyingi za serikali tutafika mbali tofauti na hawa raia na mf.mzuri ni JK jinsi alivyotupa maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi hadi kuwa donner country
 
Ile Bustani kwa kweli ni nzuri sana,ila nasikitika kuwatangazia kuwa mradi wa BRT utaibomolea mbali.
 
Back
Top Bottom