Pendekezo ukusanyaji maoni ya katiba upate live coverage ya tv na radio

demolisher

Member
Apr 11, 2011
37
100
Ninapendekeza kwa Mwenyekiti wa tume ya katiba na jamii pana ya waTanzania ukusanyaji maoni upate live coverage ya TV na Radio. Hii itasaidia watanzania kuona na kusikia kila kitakachokuwa kinaendelea. Hili litasaidia kuondoa shaka na kutimiliza msemo maarufu wa kisheria: "Haitoshi tu haki kutendeka bali na idhihirike bayana imetendeka". Kama pendekezo hili likikataliwa ni kiashiria tosha kuwapo dhamira ya kuchakachua maoni ya wa-TZ. Mwishoni waibuke eti waTZ wanapenda raisi ateue tume, wabunge wawe mawaziri n.k
 
Hii ndiyo kazi ya TBC (Radio na TV). Wafanye kazi ya kutuletea maoni ya watanzania live. Hii itawafanya wajumbe wa tume wasifanye ya kwao kwani wakifanya ya kwao watanzania watakuwa wameishajua ni nini wanataka. Hivyo tume itaona aibu kwa kuwa kila kitu kitakiwa hadharani.
 
Back
Top Bottom