Pendekezo: Tuunde umoja wa wakulima humu JamiiForums

igihumbi

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
441
350
Nimefikiri kitu kimoja baada ya kuona kuwepo watu wengi kutafuta partner/ mtu wa kushirikiana nae katika kilimo.

Kuna changamoto nyingi sana katika kushare biashara maana kila mtu anakuwa ana malengo yake wengi huwa wanaumia na kulia na wengine huwa washangilia kwa mafanikio.

Nimeona tufanye hivi; mnajiunga mnakuwa labda 5 mnaingia Morogoro kwenda kulima maharage mnakodi heka 10.

Zile heka kumi mtagawana kulingana na uhitaji wa mtu mwenyewe, kila mtu atagharamia kivyake. Hii ni kuchangia ujuzi na sio fedha kwa sababu mtakuwa mnalima karibu karibu.

Ukisema mmoja atoe pesa na mwingine atoe ujuzi mara nyingi mwisho wake sio mzuri. Lakini hii itakusaidia kukujengea kujiamini na uzoefu na ujuzi zaidi.

KWA MTAZAMO WANGU
tuunde kikundi ambacho tutakutana whatsapp ambapo tutajadili tulime nini na tukalime wapi na nikiasi gani cha heka kitahitajika, hii itamsaidia hata yule mwenye uwezo wachini kupata hata robo au nusu heka.

Endapo tutakuta na kufanikiwa kuunda hicho kikundi na kuingia shambani kuanzia kuandaa shamba, kupanda yaani hatua zote tufanye wenyewe ili kuongea ujuzi zaidi.

Pia itatuwezesha kupaza sauti kwa serikali kama kutakuwa tunahitaji msaada maana tutakua ni vijana wa mfano katika taifa. Naimani viongozi na mawaziri hasa wa kilimo watatupeleka mbali.
Lazima tujigawa katika kilimo kutakuwa na watu watakao lima maharage, mpunga, karanga, labda na ufuta hapo lazima taifa litutambue maana sisi ndio tutakua wakwanza na njia rahisi sana ya kupata mikopo ya kifedha na dhana za kilimo.
 
Wazo lako zuri...mkuu tatizo usawa unabana wawili kati ya hao watano wataweza kuafford gharama hizo za kilimo wengine wanaweza kushindwa...vile vile tunelelewa kwenye itikadi tofauti tofauti ya kimaisha....unajua hadi muda huu kuna ambao hawaamini kuwa kilimo kinaweza kuwatoa...ila sijakupinga
 
unajua tunachokosea wengi ni kutaka kuanza na vitu vikubwa mfano mtu anatakakuanza na heka 5 bila yeye kuangalia kuwezo wake,
ni vyema ukaanza na hata robo au nusu heka ili kupima uwezo wako na uelewa wako katika kilimo ukiona upo vizuri ndio ungie kwenye heka 1 na kuendelea.
 
Point
 
4feae7c518e342b1d819afc9963d63b0.jpg

e78899a44d8251509b66f506e6c647ac.jpg

Najitolea eneo hilo hapo njoo tushirikiane tunyeshe mfano
 
Back
Top Bottom