Pendekezo thabiti la Jinsi ya Kukomesha mauaji ya Albino

Mkuu@Kobe umeongea jambo la maana sana especially ulipoigusia OFM, wao wako busy kufukunyua watu wanaopeana raha zao madanguroni huko ambazo kwa kiasi kikubwa hazigharimu uhai wa binadamu wasio na hatia kama ilivyo kwa haya mauaji ya Albino baada ya yale ya vikongwe kupungua.

Kitendo cha OFM kukaa kimya kinatupa mashaka juu ya credibility ya wamiliki na wahariri, hawayaoni haya? au wananufaika vipi na haya matukio mbona hawayasemei?

Inawezekana kuna Siri kubwa manake haiingii akilini kabisa ishu kubwa kama hii kuchuliwa kiwepesi mamna hiyo tunapata aibu sana ugenini tunaulizwa sana kuhusu Albino kwanini tunafanya mauaji dhidi yao. Dah kwa kweli ni aibu sana viongozi kutwa kucha kuimba Amani Amani nchi haina Amani kwa RAIA wengine.
 
Tumwogope mwenyezi Mungu. Kitendo cha kutoa uhai wa mtu mwingine! Kisa ni imani za kishirikina ni jambo baya sana tena la aibu kwa taifa letu Tanzania. Hawa ndugu zetu Albino ni binadamu kama sisi na wana haki zote kama wengine. Leo hii imefika wakati wanashindwa kuwa na uhuru wa kutembea na kufanya shughuli zao kama watu wengine kwa kuhofia kutekwa na kukatwa viungo vyao. Jamani! Aibu gani inalikumba taifa letu. Viongozi wapo wapi kukemea swala hili. Tuelimishe jamii kuhusu hizi imani potofu za kishirikina. #AlbinoNiNduguZetuTuwalinde
 
nashangaa sana kwamba serikali haijui hivyo viungo huwa vinaishia wapi some times nashindwa kuamini..
somtimes najiuliza hii ni biashara ya watu wenye interijensia ya hali ya juu sanaaaa au ni wa aina gani but somtimes najijibu kuwa utamaduni wa mtz sio wa kiintelijensia kihivyo mpaka mtu awe trained...japo wapo makabila au watu wachache naturaly
maana busyness imekuwa km tu ya madawa ya kulevya the chain of the involved is performing every day but very difficult to be exposed..saingine nahisi serikali haijalitolea umakin vya kutosha
 
Ewe M/Mungu mwingi Wa rehema,uliyejaa huruma na upendo,wewe uliye muumbaji Wa wote,tunakuomba uwalinde ndugu zetu wenye ulemavu Wa ngozi, dhidi ya wauwaji simama uwatetee wewe uliye mtetezi Wa wanyonge,uweza na nguvu zako ni kuu kuliko za wachawi na waganga wanaotumia viungo vyao kishirikiana, waliende ee muumbaji wetu,sikia kilio chao na machozi yao uyatazame Kwa huruma zako nyingi,na kila aliyehusika au anayeji shughulisha na mauaji haya hata kama wanatumia ushirikina wasikamatwe,, wakakutane na Mkono wako wenye nguvu kuliko za hao waganga,waweke wazi na mamlaka zinazohusika zikatimize wajibu wao ipasavyo,tunakuomba M/Mungu usikie maombi yetu Kwa utukufu wako,Amina.!,,,kila anayeunga mkono maombi haya aseme ''Amina'(maana yake...NAIWE HIVYO.)
 
Ni vigumu kuamini kama vita hii imeshindikana. Yaani hawa wauaji imeshindikana kukamatwa, halafu kila baada ya muda utasikia mmoja katekwa na kuuawa . Hivi inaingia akilini kabisa kwamba imeshindikana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vijana wa kanda ya ziwa ujasiri wanaojivunia ndio huo wa kuwawinda binaadamu wenzao maalbino na kuwamaliza bibi zao wenye macho mekundu....
 
Katibu mkuu wa CCM Kinana anatakiwa akemee kwa nguvu zote wanasiasa wa chama chake, haiwezekani kila mwaka wa uchaguzi ndio Albino wanauwawa na chama chenye wanasiasa wazee waliochoka na wanaopenda kushinda kwa hila huku wakiwa washirikina wakubwa wako CCM. Ni nyoka wenye makengeza wenye jicho kali sana la dhuluma na uonevu dhidi ya Albino. Wakati umefika sasa watanzania tuongee ukweli na kuwaumbua wanasiasa kwa kuwa ndio wanaoua Albino na kutumia viungo kama chanzo cha ushindi kwenye uchaguzi baada ya kushindwa kutimiza wajibu wao kisiasa
 
SERIKALI kupitia MAMLAKA YA UDHIBITI WA MAWASILIANO(TCRA) ilidai kwamba simu za mkononi zinatumiwa kufanya uhalifu! Uhalifu uliotajwa ni pamoja na kutukana, kutoa vitisho kwa watu mbalimbali, na kutoa taarifa za upotoshaji bila mhusika kufamika! Serikali ilidai simu zikisajiliwa, kazi yake ya "ulinzi wa amani" itakuwa imerahisishwa! Simu zilisajiliwa! Wamiliki walisajiliwa! Je, Serikali na TCRA wanaweza kutuambia Simu No +3588976578 na +3588108226 ni za nchi gani, mtandao gani na mmiliki wake ni nani!? Kama hawataweza basi ni dhahiri walishirikiana na CCM kumkashifu Dr Slaa na CHADEMA kwa ujumla kuelekea uchaguzi mkuu 2010! Je, kwa mazingira haya sisi wananchi wa kawaida tunaweza kuwa salama kutoa taarifa za wahusika wenye mamlaka katika nchi kuwa ni wahusika wakuu wa kuua walemavu wa ngozi(Albino) bila kudhuriwa!? Usalama wa watoa taarifa uko wapi ilhali wahusika ni watu ambao Serikali inawafahamu na kwa makusudi inawaita "watu wasiojulikana" ilihali wanafahamika na kujulikana!? Vita hii ni ngumu sana!!!
 
+358 code nmb ya finland.tuwaokoe ndugu zetu albino.

swissme

Waombeeni Ukimbizi Zanzibar, Zanziba haijawahi kutokea kesi ya kuuliwa Albino na wala haitotokea.
Baada ya Hapo lazima kuwe Pasportcontol kuingia Zanzibar
 
Kila Mkoa,wilaya,kata,kijiji Kisha Kitongoji Kibainishe Kina Albino Wangapi Na Wanapoishi.Pili,serikali Ya Mahala Husika Iimarishe Ulinzi Kwa Kaya Yenye Albino.

Wananchi Wahamasishwe Kutoa Taarifa Mara Moja Pindi Waonapo Sura Ngeni Kwenye Eneo Lao. KAMPENI KABAMBE ZIHAMISHIWE HUKO KWENYE MAUAJI.
 
Tumekuwa tukitegemea vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mahakama kumaliza hii fedheha inayokabili taifa letu. Kama taifa, tumekubali mambo mengi ya fedha lakini kwa hili la mauaji ya binadamu kama tembo wenye vipusa tukatae kwani ni laana kubwa kwa Mungu. Aidha haiwezekani kitu kama hiki kikatushinda. Tatizo, wahusika wanayachukulia mauaji haya kama makosa mengine ndani ya jamii. Nawasihi Watanzania tukubali kuwa vyombo vyetu vimeshindwa. Hivyo napendekeza mambo matatu. Kwanza, tushinikize kwa nguvu zetu zote nchi yetu itafute kutoka nje msaada wa kikachero kwa gharama yoyote. Pili, watuhumiwa watakaopatikana kutokana na msaada huu wa kikachero wabakie magerezani hadi mwisho wa kesi zao mahakamani. Tatu, wale wakaoshinda kesi katika mazingira tata, wawekwe kizuizini.
 
Mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hayakubaliki. Serikali imeshindwa kuzuia mauwaji ya watu hao. Je, serikali imeweza kuzuia mauwaji ya watu wasio na ulemavu wa ngozi? Kesi zinazohusu mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi zinachelewa kusikilizwa. Je, kesi za mauwaji ya watu wasio na ulemavu wa ngozi zinawahi kusikilizwa? StopAlibinoKillings. Je, mauwaji ya watu wasio na ulemavu wa ngozi ni halali? Tunasema IamAlbino. But we treat them differently i.e. they are albinos. Tunasema StopAlbinoKillings. Lakini tunaenda kwa waganga na babu wa Loliondo na kupigia kura wezi (it's the same phenomenon). We are a superstitious state. We are the killing of albinos. Tweets hazitatokomeza mauwaji. Tatizo litakwisha tukiacha unafiki. It's now fashionable to tweet #StopAlbinoKillings . We should instead demand for effective institutions, if we are to address root causes of albino killings and plethora of related evils.
 
Wana haki ya kuishi,
 

Attachments

  • 1424763627608.jpg
    1424763627608.jpg
    33.7 KB · Views: 126
Back
Top Bottom