Pendekezo thabiti la Jinsi ya Kukomesha mauaji ya Albino

Kwa kweli ndugu zangu wana JF hali kwa ndugu zetu Albino ni mbaya na inasikitisha,hebu angalia unyama huu hapa: MICHUZI

Thanks Balantanda;

Nimeona zile picha, hakika hakuna cha kufananisha katika maisha niliyoishi. Nakumbuka mwaka 1996 nikiwa MUCHS niliingia muchwari nikakuta hali mbaya ya vibaka wameiva, pia nilishuhudia ya bomu la ubalozi, na ndugu kadhaa na watu baki majeruhi... LAKINI HII HAISEMEKI

ROHO YANGU INAUMIA SANA NA SIJUI TUNAKWENDA WAPI

Halafu najaribu kukumbuka kale ka-graphic alikoonyesha M.M.M. Mwanakijiji alipokua akimpinga Pinda ndio kabisaa.... Hizi burger na coucil houses zinatufanya tujione ndio zaidi

I wish ningekua bado Silver Spring au Lewsham
 
umesikia bei inayodaiwa kuwa ni ya viungo vya maalbino kwenye sakata la Mchg. wa Pentekose... ?

Unajua ni kiasi gani kimetengwa na Jeshi la Polisi nchi nzima katika kuzawadia watakaotoa taarifa za wanaokula njama hizi na kutekeleza?
 
Naamini kila mtu mwenye akili timamu, kutoka ndani hata nje ya Tanzania lazima anaguswa kwa namna ya kipekee kabisa na Mauaji ya Albino ambayo yamekuwa yakiendela kwa miaka kadhaa sasa. Matukio haya yanatia uchungu zaidi pale yanapohusisha kundi la watu wanyonge, kundi la watu wenye mahitaji maalumu ambao walihitaji uangalizi na ulinzi wa hali ya juu.

Watanzania wenzangu na WanaJF wenzetu Albino ni watu wanaohitaji zaidi uangalizi upendo wa kila mmoja wetu, kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu kuanza kwa matukio haya wengi tumekuwa tumeweka matumaini yetu kwenye kauli nyingi za kisiasa na za kiutawala kutoka kwa viongozi wetu na kuamini mauaji haya yatamalizwa na vyombo vyetu vya usalama vyenye ustadi wa hali ya juu.

Ndugu zangu, Mambo hayapo kama tulivyofikiria, Hali ya vyombo vyetu vya usalama kila mmoja anaitambua, sio jambo la kulizungumzia, Kauli za viongozi wetu wa nchi hazina sapoti ya kimantiki kwenye utendaji,

Zaidi ya miaka 8 sasa albino wanaishi kama tembo wa serengeti hawajui wapi watanyofolewa kiungo gani, hawajui muda gani watapoteza uhai, hawaoni nia ya dhati ikiwa kwenye utekelezaji wa maadhimio ya kuwalinda.

Back to the point, Je! ni sawa kuendelea kuitupia madongo serikali, kwamba imeshindwa kuzuia mauaji ya albino? tuendelee kulaumu, na kuumia kuona wenzetu wanapoteza maisha?

Hapana, tunaenda kwenye uchaguzi na tunajua matukio haya yatazidi kuwa mengi, we have to take Action kama raia, kama wafanyakazi na wakulima we have to take a very strong and Effective action which will assure that,

kwanza hakuna Albino mwingine atakayekufa, lakini pia mizizi ya mauaji haya inangolewa, na kila aliyehusika awe mwanakijiji, awe mganga, awe mwanasiasa, wote wanawajibishwa. JamiiForums imeshafanya mengi kwenye maendeleo ya hii nchi, but now we have to move to the next buttle to serve our brothers life.

Mimi nimewaza njia moja tunayoweza kuitumia kama community, lakini naamini hapa kuna watafakuri kuntu wenye uwezo wa kutoa njia tunayoweza kuunganisha nguvu za pamoja kumaliza ushetani huu na kuufanya uwe historia kwenye nchi yetu.

Mapendekezo: Tutengeneze kikosi cha watu hata watano kutoka hapa jukwaani kiende kikafanye upelelezi wa kina juu ya matukio haya. Naamini maGreatthinker kama watu8, maundumula, the boss. wanaweza kabisa kufanya upelelezi wa Ki-FBI na kutuletea majina ya kuanzia, nani anaua, nani anatumwa kuua na nani ni mteja wa mwisho wa mauaji haya.

Hapa jukwaani tuchangishane hela za kutosha ili kufinance zoezi zima.

Wana JF jaribuni kupendekeza njia zingine hapa ambazo tunaweza kuzitumia kumaliza hili tatizo tuache unafki wa kutangaza tunaumia bila kuchukua hatua yoyote, Wakati wenzetu wanakufa na sisi tumekaa kimya bila kuchukua hatua yoyote wote tunakuwa wauaji, kama hujashiriki kuzuia basi ni mshiriki wa kutekeleza full stop.

Tukae kimya, leo zamu ya albino kesho utaambiwa zamu ya watu wenye vipara, wajomba zetu baba zetu hawatapona, mtondogoo watasema wenye mvi, mimi na wewe hatutapona.

Pendekeza njia gani tutumie kumaliza tatizo hili kabla mauaji zaidi hayajatokea.
 
Mapendekezo: Tutengeneze kikosi cha watu hata watano kutoka hapa jukwaani kiende kikafanye upelelezi wa kina juu ya matukio haya. Naamini maGreatthinker kama watu8, maundumula, the boss. wanaweza kabisa kufanya upelelezi wa Ki-FBI na kutuletea majina ya kuanzia, nani anaua, nani anatumwa kuua na nani ni mteja wa mwisho wa mauaji haya.

Hio sio kazi ya JF na wala sio dhumuni la JF....Hio ni kazi ya Vyombo vya usalama...kama una taarifa za kipelelezi peleka huko.
 
KWELI ndugu yangu tupige kelele sana swala la kuua ALBINO ani aibu sana.Hivyi Watanzania tumelogwa nani?Na kwa nini kasi ni kubwa sana kukaribia uchanguzi mkuu.Ndugu zangu hawa viongozi wetu wa kuoteshwa,mara kwenda kwa Nabii,mara nyota na majini kwa ulizi wa wagombea.Wagombea wenye dalili za kutumia nguvu za GIZA tuwakatae kwa nguvu kubwa.
 
Wazo nzuri sana na hili linatokea huko ukanda wa ziwa kuna kina Rock City na wengine wengi tu ukanda huo wafanye upembuzi yakinifu kuna kule kikosi cha OFM wako kushika watu ugoni ndio kazi yao kubwa kufumania sijui salon za massage na madanguro! Sasa naomba hizi nguvu ziende kusaka na kuchimbua haya mauaji ya ndugu zetu Albino.
 
Last edited by a moderator:
njia sahihi ni kuwaua wanaojihusisha na huu mchezo. Hakuna haja ya kwenda kwenye vyombo vya usalama! Akikamatwa na ikidhibitika, basi auawe.
 
Pendekeza njia gani tutumie kumaliza tatizo hili kabla mauaji zaidi hayajatokea.
Tunajua kila mtu anaguswa kwa namna moja au nyingine na mauji ya ndugu zetu albino ila suala la kuanza tengeneza vikosi JF nadhani unachemka kaka/Dada.

Kuna mamlaka nyingi husika za kulinda raia,kuna mashirika kibao yasiyo ya kiserikali yanayoshughulikia matatizo mbalimbali ya albino.

Cha msingi labda ungesema tupaze sauti na kulaani mauaji haya kitu ambacho tunakifanya tayari.

Mambo mengine tuwaachie mamlaka zinazohusika tuache kiherehere.
 
Hili ulilotoa sio pendekezo lenye ACTION kama ulivyotaka kumaanisha kwani hujasema baada ya kuwajua hao watu nini kifanyike!.
Binafsi hili jambo linaniuma sana especially ukiona jinsi binadamu anavyoweza geuzwa kuwa kama nyama iliyoko buchani kwa vile anavyocharangwa, kwa kweli inauma sana.

Tatizo kubwa ambalo naliona na ambalo tunaweza shiriki kama wana JF kulitokomeza ni ukimya na kusuasua kwa wanasheria wa hii nchi kwenye kutoa hukumu za kesi zinazowakabili wauaji waliokwisha kamatwa siku za nyuma.

Kwa takwimu zilizopo kwa zaidi ya miaka mitano ya mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), kati ya kesi zaidi ya 50 za waliokamatwa ni kesi tatu tu (3) ambazo zimeshatolewa hukumu!!!Hili ni tatizo na kosa kubwa sana linalofanywa na serikali yetu kwani wauaji huwa wanapima upepo, obvious wanapoona hakuna kinachoendelea wanajua hakuna tatizo hata kama wataendelea na mauaji.

Nini Kifanyike?

Kama wana JF tunataka ku-affect maisha ya hawa watu basi na tuandae mikakati ya kuishinikiza serikali kutoa hukumu haraka za kesi za wanaokamatwa na kuthibitika kuwa wanajihusisha na hili zoezi haramu. Tunaweza andaa MAANDAMANO ya amani kushinikiza hili.

Njia nyingine ni ya ku-sign "PERTITION" itakayosainiwa na watu wote (duniani) ya kushinikiza serikali kukomesha mauaji haya.

Mapendekezo: Tutengeneze kikosi cha watu hata watano kutoka hapa jukwaani kiende kikafanye upelelezi wa kina juu ya matukio haya.

Naamini maGreatthinker kama watu8, maundumula, the boss. wanaweza kabisa kufanya upelelezi wa Ki-FBI na kutuletea majina ya kuanzia, nani anaua, nani anatumwa kuua na nani ni mteja wa mwisho wa mauaji haya.
 
Tunajua kila mtu anaguswa kwa namna moja au nyingine na mauji ya ndugu zetu albino ila suala la kuanza tengeneza vikosi JF nadhani unachemka kaka/Dada.

Kuna mamlaka nyingi husika za kulinda raia,kuna mashirika kibao yasiyo ya kiserikali yanayoshughulikia matatizo mbalimbali ya albino.

Cha msingi labda ungesema tupaze sauti na kulaani mauaji haya kitu ambacho tunakifanya tayari.

Mambo mengine tuwaachie mamlaka zinazohusika tuache kiherehere.

Vyombo vya ulinzi huwa vinatuhimiza kuwa jukumu la kusimamia usalama ni la kwetu wote that is first, hivyo kuwaza njia za kuisaidia serikali yetu haiwezikuwa crimes.

Pili, Watu wanakufa kwa zaidi ya miaka kumi sasa, na wanaendelea kufa na kwa muujibu wa rekodi zinavyoonesha huu ndio msimu wa kupoteza ndugu zetu wengi zaidi, and we take no action!!.

Ingekuwa inatokea kwenye ukoo wako, ungeiachia polisi? Eeh!? Laiti ingekuwa ni watoto wako, mkeo, wazazi wako wanaelekea kupoteza maisha kwenye uchaguzi huu, ungesubiri kova aje kukulindia? ungeacha ndugu zako wakae Mtwara, wewe unaendelea kula Bata Dar?

Lazima sasa tukubaliane hata na situation zisizo eleweka kuwa jeshi la polisi linajitahidi sana lakini sasa kwa zaidi ya miaka 10 hali imezidi kuwa tete hivyo inabidi wananchi tuongezee nguvu.
 
Kwa nini haya mauaji ya albino ya ongezeke tunapoelekea kwenye hizi chaguzi za kisiasa?

Wito tuone sababu za kuushirikisha umoja wa mataifa kama uwezekano upo wapewe urai wa nchi ambayo/ambazo hazina historia ya uuaji wakati wa chaguzi zake.
 
Mawazo mazuri.................tatizo nchi hii inakatisha tamaa. Unaweza kuwa unaspy wauaji kumbe na wewe unawindwa. Hata ukiwafahamu ukariport unaambiwa ushahidi huna.
 
  • Thanks
Reactions: 999
njia sahihi ni kuwaua wanaojihusisha na huu mchezo. Hakuna haja ya kwenda kwenye vyombo vya usalama! Akikamatwa na ikidhibitika, basi auawe.

Baada ya kutoa taarifa vizuri, yaani mtandao mzima unakuwa umeshapatikana ndiyo anauawa
 
Watu 11 waliouwa albino wamehukumiwa kunyongwa tangu Kikwete awamu ya kwanza, condemn mmoja wapo ni Boje Mawe, lakini Kiwete hatii sahihi wanyongwe anabaki kuchekacheka tu. Hatua ya kwanza kikwete atie sahihi waliohukumiwa wanyongwe halafu hatua zingine zitafuta
 
Bila kukitoa hiki chama cha ccm madarakani itakuwa ni hadithi tu. Hivi kama mtu alimwaga ndumba mpaka bungeni na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa itakuja kuwa huyo albino? Tulichukua hatua gani? Juzi kwenye katiba watu yametangazwa maandamano watu walitoka. Tukingoja vibali itakula kwetu. Wenye jukumu naona kama limewashinda ama wananchi hawawapi ushirikiano kutokana na kujiweka upanda fulani
 
Siyo kwamba juhudi za kuubaini mtandao huu wa manyang'au hazijafanyika, dada Vick Ntetema wa BBC miaka kadhaa iliyopita alifanya kazi hiyo katika mazingira magumu sana, kazunguka sehemu mbalimbali ambako ndiko waliko wapiga ramli maarufu hasa wilaya za Magu na Busega alitoka na utafiti ambao kama serikali ingekuwa haina kigugumizi hili tatizo lingekuwa historia nafikiri wote tunaelewa kilichomtokea dada yetu hadi leo yuko kimya, kuna wakati fulani niliwahi kumsikia dk Patrick Bulugu wa shirika la UNDER THE SAME SUN akiweka wazi ugumu nakigugumizi cha serikali katika jambo hili nafikiri kama yuko humu JF atueleze kwani lengo ni kuhakikisha jamii hii ya binadamu wenzetu inaishi salama na kwa amani kama tunavyoishi wengine.
 
Wazo nzuri sana na hili linatokea huko ukanda wa ziwa kuna kina Rock City na wengine wengi tu ukanda huo wafanye upembuzi yakinifu kuna kule kikosi cha OFM wako kushika watu ugoni ndio kazi yao kubwa kufumania sijui salon za massage na madanguro! Sasa naomba hizi nguvu ziende kusaka na kuchimbua haya mauaji ya ndugu zetu Albino.

Mkuu Kobe umeongea jambo la maana sana especially ulipoigusia OFM, wao wako busy kufukunyua watu wanaopeana raha zao madanguroni huko ambazo kwa kiasi kikubwa hazigharimu uhai wa binadamu wasio na hatia kama ilivyo kwa haya mauaji ya Albino baada ya yale ya vikongwe kupungua.

Kitendo cha OFM kukaa kimya kinatupa mashaka juu ya credibility ya wamiliki na wahariri, hawayaoni haya? au wananufaika vipi na haya matukio mbona hawayasemei?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom