Pendekezo: Tanzania iweke Balozi Uholanzi!

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
Barua ya kwazi kwako Ndugu JK rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Nchi tajiri sana Duniani ina mbunga kibaoo, maziwa yenye kutoa samaki hadi Sauper akaja kupatia jina huko,Nchi yenye watu wavumilivu sana na wanaopenda lakini Serikali muda wote ina waangusha lakini hawakati tamaa.

Nchi yenye kuongozwa na watemi na wenye kauli jeuri kama Kalamagi lakini ndugu rais yuko kimya , Nchi inayo sadikiwa kuwa na makaa ya mawe, gesi, mafuta, urenium,madini ya kutengeneza meli, madini kibao , maua nk .

Pamoja na mambo hayo hapo juu bado tunasoma na kusikia toka kwa wakuu walioko chini yako nikiwa na maana ya mawaziri nk kwamba bajeti yetu 50% inagharamiwa na wazungu .Mali tunazao , akili tunazo na uwezo wa kuzifanya mali zetu ziwe msingi imara wa kulambwa na kubembelezwa Duniani hakuna .

Serikalio ya Uholanzi iko kwenye Umoja wa EU lakini kama serikali imekuwa kati ya Nchi marafiki wakubwa sana wa Tanzania kwa hila hali . Wanamwaga mapesa , yao kwa mikopo na hata misaada sawa , wamekuja kuwekeza kwa wingi sana Tanzania na sasa wako watu wao ambao wanafanya biashara na hasa utalii bila ya vibali na hawalipi kodi .

Hili nitaliacha kwa sasa ila nitalisemea pengine .Waholanzi kwa siku za karibuni wamekuwa marafiki wa karibu kuanzia kutoa mafasi za masomo kwa Watanzania kwa ngazi za Masitatz(Masters) na diploma na hata PhD na mengine mengi lakini ndugu Rais hujawahin kufika kwao kujitambulisha .Sijui labda wewe mkuu una sababu yako lakini bado najiuliza sana .

Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na ukaribu wote bado hakuna Ubalozi wa Tanzania Uholanzi.Balozi wetu wa Ubeligiji sina uhakika kama kapata kibali sasa kuja hata kuwatembelea Watanzania wa Uholanzi maana nakumbuka kwaba hata ndugu Mkapa anaenda mwaka jana kuaga Uholanzi balozi alienda kwa special permit .Uone mambo haya na kwa miaka kama 2 sasa tangia awe balozi pale Ubeligiji.

Tuna mtu anaitwa Hakkenburg ni mdachi huyu ambaye kwa kweli ni business minded .Hana habari na watanzania na mambo yake hayaeleweki . Ndugu Mkapa alisema siku ile ya kuagana na Watanzania wa Uholanzi kwamba kwenye handouts zake atakueleza juu ya umuhimu wa kuwa na Ubalozi Uholanzi je umepata ujumbe ule ? Ama bado kuna kubana matumizi hata mahala pale ambapo tunapata faida ?

Ubalozi wa Tanzania ama ofisi ya Konshula Uholanzi iko ofisini kwa huu mwakilishi wa watanzania Mzungu.Hatumbagui lakini pia kwenye habari zake wapi pa kumpata mara ya mwisho niliona kwamba anapatikana The Hague lakini ukweli ni kwamba anapatikana kwenye kijipori fulani ukipita kwenye highway utaona bendera ya TZ imepauka haishuki wala kupanda ilisha panda basi , hakufikiki bila ya taxi ama personal vehicle . Ndugu rais tafadhali fikiria hili ili ulipatie jibu ka Nchi hapa kama kana kuwa msaada mkubwa namna hii kwa Tanzania kwa nini basi tusipate Ubalozi na kuhudumiwa na Mtanzania badala ya sasa ilivyo shida kubwa hata ya kumpata mwakilishi wetu ?

Naomba chonde chonde ulikuwa mkuu wa mambo ya nje unajua vyema kuliko mimi sasa litupie macho hili .

Mimi Mtanzania mwenzio

Mugishagwe Mwana wa Majimoto
 
Mugishagwe
Huyu jamaa Hakkenburg nimewahi kukutana naye na alinieleza mambo ambayo sikuamini kwamba mzungu anaweza kuijua na kuihambua TZ namna hii na ana dharau hadi mwisho kwa Watanzania na serikali yetu .
 
Mzee Es huu ujumbe umesha mpa Rais au Waziri wa Mambo ya ugenini ?Hebu nipe majibu au Fillga umewapa huu ujumbe wako ? Au nyie mnao kuja kutukana humu hii issue mmeifikisha huko kwa RO na wenzake jamani ?
 
rais hakurupuki kufungua ubalozi, una gharama nyingi.

Halafu bado kiwango cha ushirikiano baina ya uhalonzi na tanzania sio kikubwa cha kujustify ushirikiano wa balozi kuwepo pale,beside balozi wetu wa belgium anatuwakilisha vizuri tu pale.

Sio kwamba ni mbali kiasi hicho na sio kweli kwamba balozi alihitaji special permit kwenda kumuona rais mkapa akiagana na viongozi, huku ni kutwist the truth.

Nilikuwa Amsterdam in july just after the world cup sikupata matatizo yeyote kusafiri kwenda ubelgiji manake mwendo wa treni ni only one hour 33 minutes na ni very comfortable.

Na balozi wetu Mlay alinieleza kuwa watanzania wengi wapo Uholanzi lakini nao pia hawapati tabu kupewa msaada tokea ubelgiji, in fact baadhi ya watanzania waliopo ujerumani kwenye ubalozi wetu mwingine kule huwa wanashughulikia masuala yao belgium kwa vile ni strategically located.

Kwa hiyo wakati bado ukifika hata mimi ntaomba iwe hivyo.

Kwa sasa kwenye bajeti ya safari hii tanzania inafungua ubalozi brazil na malaysia kwa sababu maalum:

Brazil watatufaidisha sana na elimu ya kilimo wale wame-excell katika kulima na kuuza mazao yanaostahamili ukame kama vile mihogo-alisema hivyo waziri wetu Cyrill Chami.

Malaysia ndio kwenye cheap technology kule ndio super highway ya mitambo ya kisasa ya information technology hivyo tunahitaji kuwa nao karibu, kwa muda mrefu walikuwa wakioperate na tanzania kutokea zimbabwe sasa wamefungua ubalozi wao Tanzania na sisi likewise tunajiunga hawa watatusaidia sana manake wametuacha sana kisayansi na kiuchumi ingawa tulikuwa nao sambamba katika level ya uchumi mwaka 1961.

Uholanzi patasubiri.
 
Katika kusafiri hapo nilikuwa nacounter argue hoja yako ya special permit nchi hizi zinaoperate schengen visa ukipata visa ya nchi moja unaweza kusafiri nchi nnyingine kumi na tatu sasa balozi hahitaji permit mradi anasafiria pasi yake basi hahitaji chochote beside hakuna border control between these countries.
 
Tafiti
"Malaysia ndio kwenye cheap technology kule ndio super highway ya mitambo ya kisasa ya information technology hivyo tunahitaji kuwa nao karibu"

1. Hapo umeniacha mbali Tafiti. AS cheap as IPTL, or any other technology, please enlight me! There are IT kings like India, China, etc cheaper than Malaysia, or even Australia of which all the hitech products are most produced in East Asia majority in China.

2. Go to the records, in case of cooperation Holland contributed a lot, frankly speaking I do not see how Malaysia can be important as you're saying. Maybe the issue here is as you're saying is too expensive to open embassies.

By the way what about those consulates worldwide which are being used by private business people; in the name of Consular General; who is in the payroll!!!!!!!!!
 
tafiti

Nimelazimika kuondoa mawazo yangu kukuamini juu ya hoja zako na vielelezo vyako juu ya RO baada ya kuja na uzushi hapa .Sijui kama kweli unajua unachokisema and you have missed a very huge point hapa .

Mimi Mugishagwe I need no special permit kama niko Holland kwa visa ya Schengen.Nakwenda kote kasoro UK ambako hawana mahusiano ya namna hii kwenye travel doc .Balozi Mlay anahitaji special permit kuja kukutana na Watanzania ama kuhudhuria mkutano wowote kama credencials zake hajaziweka kwa Queen wa Uholanzi na kupewa kibali maalumu cha kuingia Nchi hii kama Balozi .Hii ndiyo niliyo semea mengine uliyo yaelezea kweli nimesikitika unabisha hata usilo lijua .

Mwaka jana Mzee Mkapa alienda kutoa Mhadhara ISS na akatumia mafasi hiyo kuaga Watanzania walimweleza hili tatizo na Mlay alikiri kutofika Holland kuongea na Watanzania kwa sababu Utambulisho na kupata ruhusa kama Balozi wa Nchi hizi .

Mkapa alisema atamweleza Rais mpya juu ya hili mbele ya Hakkenburg ambaye ni mwakilishi wetu pale Hotelini unacho bisha sasa sikijui .Again issue ya kupata huduma toka Brussels wakati hata Mlay kakueleza Holland ina Watanania wengi sijui sasa unasemaje. Anaweza kuwa Brussels kwa sababu ya EU lakini watanzania wako hapo wengi sana in Holland.

Umesema Ubalozi wa Brussels ku save watu wa Ujerumani kwamba ni kitu gani ? Ama kweli wewe naona ni mtu wa ajabu sana .Uliza kwa nini watu walitoka Germany kwenda kupata Huduma pale Brussels . It is because Karume gave the shit .Karume na watu wake hawakuwahi kumjali mtanzania . Kuna siku aliitwa kenye mkutano wa Watanzania pale Stuttigart akaulizwa maswali ya msingi mojawapo ya majibu yalikuwa hivi.Pilipili ya shamba usiyo ila inakuwashia nini ? Kwamba watanzania wale kuku na matatizo ya Tanzania waachiwe walioko huko lakini baadaye akaja Dar kugombea nafasi ateuliwe kugombea Urais .

tafiti sitakuelewa tena hata ukija na ushahidi mwingine maana kumbe huna ushahidi bali unajenda story ku win watu hapa .

Kwenye hili umekosea sana na kuna data kibao .Sasa kama unasema hakuna shida ubalozi kwa nini basi na Ujerumani wasiondoe aka save huyu Mlay pekee huko ?Nimekushangaa sana mengine ya Malasia ndiyo kipeo umbele sitasema maana watu watanishangaa . Ona juzi Rais kafukuza makampuni 2 mojawapo ni Malasia sasa tunaenda kujifunza nini ?

Ila nimekuogopa sana na hasa baada ya kuingia kwenye anga zangu sasa naijua hili vyema.
 
Ndio bwana Mugishagwe,

Siko familiar na situation ya uholanzi, ila kama kuna strong case ya kufungua ubalozi nitaisapoti. Waholanzi wana ubalozi pale Dar? Kama wanao itaongezea umuhimu nasi kuwa na wa kwetu nchini kwao.

Umetaja suala la huyo consular, kuna haja ya hizi consulate kuangaliwa. Kuna jamaa yetu alipata matatizo akiwa Singapore(around 2002), wa-singapore wakamwambia aende kumuona consular wa Tanzania.. akawaambia, hakuna consulate ya Tanzania in Singapore. Jamaa wakamwambia ipo na kumpa address. Akaitafuta na kufika mahali kweli akakuta kuna bendera ya Tanzania na kuna mhindi yuko na biashara zake hapo, na wala masuala ya Tanzania hayamo katika ratiba zake za kila siku. Infact alimshangaa jamaa kapajua vipi pale!

Eeeh, nliwahi kumuona huyo balozi Karume .. Man, the guy is very arrogant and boasty! He doesn't have any respect. man, it is as if he is constantly auditioning for a movie role that requires arrogance. Sitoshangaa kuwa wa-Tz wa ujerumani kuukwepa ubalozi wao. I was suprised to see him transferred to Italy instead of being sent back home, considering the fact he has been out of the country too long. Probably kaka aake hamtaki arudi kule ZNZ, maana lazima atamtibua tu.
 
Bwana Mugishagwe

Naam nimeona message yako ya awali, naamini maelezo niliyotoa ndio aliyoyasema mama migiro na manaibu wake na nina mahusiano ya kitaaluma na malaysia kutokana na kuwa na colleagues wengi waliosoma pale Kuala Lumpur wote wamekiri hivyo.

Mmetoa mifano ya China na India ambapo kote tuna mabalozi na wawakilishi wetu!

Kuhusu Holland:

Sikujua kama unaishi hapo nitakutumia message prior to my next trip huko tukutane japo kwa moja moto moja baridi. Hupenda kukutana na watanzania wenzangu kila nifanyapo trip nje.

Naam nilikuwa na balozi mlay in july na tuliongea kwa kirefu kuhusu nadharia ya economic diplomacy na akanipa kadi yake ambayo ilikuwa inaonyesha kwamba yeye ni accredited balozi wa tanzania hapo uholanzi.

Halafu bwana anaeshughulikia passport Mr Zoka [aliniambia kafundishwa na mahiga in 1975 pale UD] yeye alishawahi kufika na mama SS KAMBA [yule mzungu anaedeal na masjala pale ubalozini belgium] wote hawa huwa wanakuja sana holand kudeal na daily issues zikiibuka na wanafanya kazi bila utata, sina hakika wewe bado ni mzalendo wa tanzania meaning unahold passport gani lakini na-assume ni mbongo kwa vile umesema unatumia schengen permit basi utaona kabisa kwamba jamaa walishafika hapo kuwapa watanzania passport.

Nasikitika katika intl relations watu huwa wanachanganya mahusiano ya ubalozi baina ya nchi na nchi na majukumu ya ubalozi kwa wananchi wake waliopo katika nchi husika. hivi ni vitu tusivichanganye, ubalozi unaweza unaweza kufunguliwa kwa vile kuna community kubwa ya watanzania lakini hiyo haiwezi kuwa key reason.

Tuelewe nchi yetu bado ni maskini sana ndio kwanza tuna balozi fully functioning 31 tu zinazohudumia nchi zote za dunia sasa holland kijiografia na mahusiano na nchi yetu bado hakuna justifications kabisa kwa kweli kuwa na ubalozi.

Kuhusu watz wa ujermani kwenda hapo belgium it could be many reasons na hizo za balozi inawezekana kabisa yule jamaa Karume hatabiriki lakini pia ukaribu wa kijiografia ni sababu mojawapo.

Kudrive kutoka cologne kwenda brussels ni masaa mawili wakati ukidrive kutoka cologne kwenda berlin ni masaa saba! sasa hapo hata mimi ningeenda brussels.

nadhani nimejibu, nashukuru kwa changamoto na samahani kama pale mwanzo sikueleweka vizuri
 
hii ya singapore ni very interesting kwa kweli manake sikujua kama ipo hivyo.

sijajua vigezo lakini nitaulizia nipate maelezo vizuri nijue mambo huwa yanakwendaje.

adios
 
tafiti
pamoja na kujirudi kwako lakini bado tunasema kuna haja ya kuwa na Ubalozi hapa . Wewe unaongelea mambo ya PP wewe bwana unaonekana kukosa points za .Zoka hajawahi kuja Holland kutoa passport kwa taarifa yako .Mimi niko tayari kumsuta wewe ukiwepo .Hakuna ofisa wa Ubalozi alisha wahi kuja Holland kisa kuwaatia watanzania passport huu ni uongo kubwa .Watu wakati wa lile zoezi walienda Brussesels tena kwa appointment.

Nakumbuka Mushigawe alipata shida sana PP baada ya kuanza mauzauza na Ubalozi moto ukawaka hadi kwa Mkurugenzi wa Uhamiaji na alikuja Holland akajieleza na kuomba samahani mbele ya rais .Ukisema hakuna justification kwa Ubalozi sijui unaelewa kiais gani Holland wanaipiga jeki Tanzania kwa kila hali .

Kuendelea kukataa ukweli ndiko kunapelekea mwakilishi wetu kujikita kwenye vitendo vya rushwa kuanzia Hazina yetu hadi mbuga za wanyama kuwa na makampuni nk . Kuna uchafu mwingi sana .Uliza ofisi ya huyu jamaa iko utapelekwa porini kabisa wakati kwenye mtandao wanaonyesha iko The Hague .Hii ndiyo Tanzania mzungu yule ukiongea naye ni kashfa kwa Tanzania na watanzania na anasema yeye ni Mfanya biashara na kweli anafanya .Haya JK anayajua vyema maana alikuwa Boss wake . Hapa kuna mengi mimi naishia ila tafiti uache tabia ya kusema mambo bila ya kuyajua na hata usemeje kweli hili naungana na Mzee Muggy kwanza hulijui n huwezi kusema lolote ukaeleweka watu wanao kaa na walio kaa Uholanzi wa mengi ya kusema .
 
tafiti
Naomba kafanye tena utafiti uje upya ila swala kwamba Tanzania ni masikini na tunafanya mambo kwa hatua nakataa kwamba Tanzania si masikini na we spend more that hao wanao tunjazia bajeti yetu .We are not poor huu wimbo uacheni kabisa .Kama unasema sisi ni masikini naomba usee kivipi.
 
Mzee Muggy,

Habari za hapo zote JK anazijua fika kwani alishapewa siku nyingi lakini akaamua kushughulikia la Mahalu tu, sasa unajua yeye ni rais wa nchi aliyechaguliwa na wananchi kwa njia ya demokrasia kwa hiyo siku zote tunampa, the benefit of the doubt kwa mambo mengi yanayohitaji marekebisho, na hilo la Uholanzi ambalo nilillalia macho na wewe unajua vizuri nalo ni miongoni mwao,

Lakini anapopita mistari tunamkumbusha!, kama vile kumchagua RO!
 
Jambo hili baada ya tafiti kufika hapa na data za ajabu limenifanya nisimwamini kabisa kwa mambo yake na RO.Sikutegemea kwamba mtu anaweza kibisha kitu ambacho hakijui.Huyu jamaa Hakkenburg ndiye kaanzisha mradi mbaya kabisa wa kuweka sticker kwa wageni waingiao Nchini nk . Miradi hii ina mizizi ya harufu hafu kuanzia hazina .Mengi yanajulikana hapa sijui tafiti hili unalijua kwamba ni huyu mzungu ali engineer hii move na kafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno ?Unajua kwamba ni yeye kwa kutumia nafasi yake kajiingiza hadi Tanapa na sasa ana makampuni ya Utalii Tanzania anapenda na hata majuzi mwanae alio na wamekujaa wamekaa mbungani kwa gharama zetu kwa wiki 3 yeyey na famila yake nzima ?tafiti bwana umenimaliza sana na kwa maana hiyo ndiyo tunasema Ubalozi ni muhimu Holland kuliko Malasia
 
Mzee Es kama JK anazijua zote kimya cha nini kila mara kwa muda wote huu ? Tuelewe ama tuamini maneno ya huyu Konsula kwamba ameiweka serikali mkononi na kuendelea kusema your government is very corrupt .Hadi yeye Hakkenburg kusema anashiriki kuandaa muongozo wa miaka 5 wa seikali ya JK na utendaji wake wa kazi . Hii ni dharau kubwa mno kwa mzungu kuingia na kuwema mizizi hadi kwenye hazina yetu .

Mzungu huyu kuwa makampuni ya Utalii kwa jina la mwakilishi wa Watanzania ambao hana hata mawasiliano nao .

tafiti nangoja uje na hoja zako za utafiti
 
tafiti unangojewa hapa uje a data zako ama umeingia mitini wewe kazi ni mada ya RO ? Maana ulianza ubishi wa ajabu kweny hili ukapewa vipande uko wapi ? Ukweli wako kwenye hili utakujengea heshima tukuamini zaidi lakini ulianza na uongo mkubwa njoo utoe utafiti wako mzee
 
utaupata bila shaka, narecheck my facts nitarejea, hakimbii mtu manake mimi sishindani kwa pumzi natumia hoja halafu siku zote nipo shule hata barabarani manake hekima ni haki ya mtu wa busara, kwa hiyo kwa sasa naamini kesi yangu ni imara na sahihi la kama ni potofu nita-admit humu munipe ukweli

kwa sasa naona mmekaa mkao wa kusuta suta hivi badala ya kukaa kimjadala!
 
tafiti tufunge hii mada ama unakuja ma utafiti wako ndugu sema tujue moja kama umenawa na data za ko basi tuifunge na JK aelezwe kwamba bado watu wanataka kujua kwa nini Konsula mzungu ana mkono mzito ndani ya hazina yetu .
 
Back
Top Bottom