Domy
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 4,700
- 1,086
Ndugu Wanabodi.
Nimefuatilia vyombo mbalimbali vya habari siku ya leo,habari kuu ikiwa ni kufukuliwa kwa mabaki ya aliyekuwa kiongozi kipenzi cha wapalestina Hayati Yasser Arafati kutokana na malalamiko kwamba aliuwawa kwa sumu hivyo umefukuliwa ili kufanya uchunguzi upya kubaini kama kweli alipewa sumu ambayo ni mionzi ili wahusika wachukuliwe hatua.
Sasa pendekezo langu ni kwamba,hapa Tanzania kumekuwa na manung'uniko ya Muda mrefu Tangu kufariki kwa Baba wa Taifa hili ambaye pia alikuwa ni rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania Mwl Julius K.Nyerere kwamba hakufa kwa mapenzi ya MUNGU bali alipewa sumu akiwa uingereza au kabla ya kwenda uingereza alikofia hata kufikia hatua kwa baadhi ya wanasiasa kurushiana maneno makavu jukwaani.
Sasa ili kuondoa utata huo ni kwa nini mabaki ya mwili huo yasifukuliwe ili uchunguzi ufanyike upya na kama ni kweli Mwl Nyerere alipewa sumu hatua zichukuliwe kwa faida ya Tanzania na familia yake? Ni mtazamo tu au wadau mnasemaje kuhusiana na hili? Najua uzi utawapa kigugumizi mods lakini naomba mnitendee haki.