Pendekezo: Madaraka Nyerere awe mgombea urais wa CCM

REBEL

Senior Member
Dec 15, 2010
166
64
Kutokana na uroho wa madaraka wa viongozi wa CCM ni bora chama hicho kikongwe kichague mgombea wake ambaye hana kashfa wala uroho wa madaraka.Pia ,kwasababu jina la Nyerere ni jina kubwa vichwani mwa watanzania kama ilivyo Ghandi India au Mandela,Martin Luther King itakuwa rahisi kuliuza jina la Madaraka Nyerere.
Baada ya kuona picha za habari za kimataifa Korea Kaskazini Kim Jong il nimeona wazo langu lina uzito na linaweza kukirudishia heshima CCM ya zamani.Maana chama cha majamba cha leo kimejaa watu matajiri,wabinafsi na wapenda ngono ambao jamii haiwataki.

Lakini tukileta mtu freash(Madaraka Nyerere) ambaye hana kashfa yoyote kutoka Butiama, mhandisi ambaye kaacha fahari zote na kukaa kijijini Butiama kutumikia watu wake.Nadhani anaweza kuleta changamoto ya ushindani wa urais wa 2015 dhidi ya mtu makini kama Dr.Wilbrood Slaa na nguvu ya Chadema.

Mwenye maoni kuhusu Madaraka Nyerere anakaribishwa.
 
tatizo si nani agombee CCM, tatizo ni chama chenyewe, hata kama akigombea Madaraka bado CCM itakuwa ile ile, atachukuwa mawaziri wale wale, washauri wale wale SERA ZILE ZILE.

Kama Madaraka anafaa, agombee kupitia chama kingine tofauti na CCM, Kwanza apate angalau miaka miwili ya kukijenga chama hicho kitambulike na kukubalika na wananchi mpaka vijijini ( mind you, this should not be CDM)

WE NEED CHANGES, AND ONLY CHANGES WILL COME OUT OFF CCM
 
CCM hata iweke malaika kuwa mgombea haiwezi kufufuka, ohhh marehemu CCM!!!!!!!!!


mnatuahidi hivyo hivyo hapa kila wakati lakini baada ya chaguzi huwa mnakuja na mabegi ya sababu kwanini ccm magamba wamewashinda ikiwemo ile sababu maarufu "wamechakachua",Yani kutwa mnachakachuliwa nyie tu,wapinzani tuache maneno tujipange kikweli ka sivyo kila siku tutakua tunapeana moyo kwamba tulishinda lakini tumechakachuliwa,tukae tujiulize hivi ccm wanatushindaje?
 
huyu madaraka ndo mdudu gani tena siku ccm ikitaka kukatikatika wamuweke mtu kama huyo
 
Hii sio nchi inayotawaliwa 'kifalme' eti tuanze kurithishana. Pia kumbuka tunaongozwa na watu sio majina. Achana na mawazo mgando hayo. Kajipange tena. Uje na mambo ya maana, sio maneno ya vigengeni.
 
Tukifikia hapo,kuchagua m2,eti kwa sababu baba ni NYERERE,Tutaipeleka TZ yetu kubaya!
CCM ni sikio la kufa!
 
Hii sio nchi inayotawaliwa 'kifalme' eti tuanze kurithishana. Pia kumbuka tunaongozwa na watu sio majina. Achana na mawazo mgando hayo. Kajipange tena. Uje na mambo ya maana, sio maneno ya vigengeni.

Swadakta, hapo umenena ndugu yangu. Jamaa hana hoja hapa, tunachagua majina au watu wenye uwezo. Huyo anaesema hana kashfa ni kwa kuwa hatujui madhambi yake.
 
Alipochaguliwa Kikwete alikuwa amelifanyia nini taifa letu?

Alikuwa Waziri wa Fedha, alikuwa Waziri Nishati na Madini, alikuwa Ministry of foreign affairs.

Madaraka kashika cheo gani mpaka apewe urais
 
Back
Top Bottom