Pendekezo: Maandamano dhidi ya bunge

Injinia

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
849
26
Napendekeza kufanyike maandamano ya mshikamano wa wananchi kuonesha kutokuwa na imani na bunge na uongozi wa serikali. Any takers?

Manake mimi yamenifika utosini.
 
Wabongo si wazalendo wa nchi yetu hata kidogo, wenzetu wako na uchungu sana na nchi zao, kuna nchi pale mashariki ya kati, kama sikosei ni Syria, Mkate uliongezwa bei kwa senti 20 tu watu walitafutana, maandamano ya kufamtu, viongozi wanakosa kura, wwengine wanatimuliwa kazi, sisi hapa kila kitu kinafanywa against US wananchi tunabaki kunung'unikia kichinichini tuu, TUANDAMANE WAKUU, nchi zote zenye demokrasia ya kweli hasa ulaya na marekani ukisoma historia yao walisha chinjana sana kwa mambo ya kipuuzi kama haya, mpaka kustarabika kafara ishatolewa sana tuu.
 
Tunaweza kukubaliana humu ila siku ya maandamano tukakutana watu wawili tukaishia kupiga story na kutafuta cafe ya jirani kupotezea muda.

Hapa ni kujiapiza kuwaelimisha wananchi ili waelewa mambo yalivyo na wajue how potential they are. Maandamano kwa wazalendo wa kibongo wenye heshima ya uoga ni sawa na kumshawishi osama anyoe ndevu zake.

Yanayotokea bungeni ni sarakasi hakuna usiriaz wa kuisaidia nchi. Kuna uchizi unaendelea mahala fulani nchi hii
 
Napendekeza kufanyike maandamano ya mshikamano wa wananchi kuonesha kutokuwa na imani na bunge na uongozi wa serikali. Any takers?

Manake mimi yamenifika utosini.

Mimi nitakuwepo kwenye maandamano na bango langu kubwa la kumuambia Mbunge wangu Mwakyembe aache toka jana kujivunia kuwa"yeye ni mpambanaji"na aache usanii!

Hawa waliokuwa wanajiita wapambanaji wamenifedhehesha sana na kwa kweli sasa imejidhihirisha wabunge wote wa CCM wapo kwa maslahi ya matumbo yao wala sio maslahi ya UMMA!

Nasisitiza tena wote ni wasanii,wapambanaji my foot!!
 
napendekeza yafanyike haraka nayasiongozwe na chama chocho kile cha siasa
 
Back
Top Bottom