Pendekezo langu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo langu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ras, Nov 9, 2010.

 1. Ras

  Ras Senior Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF NAWASALIMU NA KUWAPONGEZA KWA KUFANIKISHA UCHAGUZI KWA AMANI ingawa najua kuna waliofurahia sana matokeo na kuna walioumia, binafsi nimeumia sababu nilipenda mabadiliko lakini maisha lazima yaendelee.

  Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala (threads) mbalimbali zinazoanzishwa ktk jukwaa hili na lile la Uchaguzi 2010. Nimegundua kuwa watu wengi hawakubaliani na mfumo mzima wa tume ya uchaguzi na wangependa iundwe kama tume huru kwa maana kuwaisimuhusishe rais wala serikali husika. Nadhani hili ni jambo la busara na halihitaji degree kuona ubaya wa tume ya mfumo kama huu wa tume yetu. Naamini kuwa wanajf wote ni wasomi, na kama kweli mna mapenzi mema na nchi yetu tufanye mambo kisomi, hebu tuanzishe vuguvugu kuanzia sasa ya kutaka madaliko ktk kuundwa tume ya uchaguzi kwa kutaka iundwe tume huru popote pale ulipo, jaribu kuwafumbua macho watu kuhusu hili mfano, makazini, shambani (vijijini) n.k. Inasikitisha sbb vijijini kuna ndugu zetu ambao wanaangamia ktk umaskini wa kutisha, hawana elimu! wanahitaji kuamshwa! Nasema hivi kwa sababu HAKIKA KAMA KWELI CCM WANACHAKACHUA KURA KWA KUPITIA CHOMBO HIKI HATA WATANZANIA WAFANYAJE KATU HAWAWEZI KUTOKA MADARAKANI HAWA WATU na watalindwa na UN kwa kivuli cha demokrasia. Kwa kuanza mapema kudai haya mabadiliko ndiyo itakuwa ukombozi wa nchi yetu yenye Mali asili na Neema nyingi ila uongozi mbovu uliojaa ubinafsi.Tukifanikiwa ktk hili twaweza hamia kwenye Katiba maana nayo ina mapungufu mengi tu. Hatimaye uchaguzi ujao tutavuna matunda mema.
  Mungu ibariki Tanzania, naomba kuwasilisha.
   
Loading...