Pendekezo la Waziri Mkuu PINDA kwamba CHADEMA iache matumizi ya nguvu ya umma halikubaliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo la Waziri Mkuu PINDA kwamba CHADEMA iache matumizi ya nguvu ya umma halikubaliki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 11, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CHADEMA isikubali pendekezo la Waziri Mkuu la kuitaka iache maandamano. Lazima ikubalike/ieleweke kwamba maandamano ndiyo njia pekee ya kuleta ukombozi hivyo badala ya kuacha zoezi hilo, napendekeza nguvu iongezwe katika maandamano (nguvu ya umma) ikiwezekana maandamano yaende pamoja na kuharibu miundombinu ya barabara, kuwafuata mafisadi na kuwapa kibano mpaka serikali ishike adabu.

  Nawasilisha.
   
 2. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  hapo kuharibu miundo mbinu sipo!!ila maandamano nayakubali,maana ni njia ya kufikisha ujumbe!
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Daffi na mafisadi si tuwape kibano warejeshe mali zetu?
   
 4. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mandamano ndiyo njia pekee ya kupambana na serikali legelege ya mkoloni mweusi CCM,hi ni serikali iliyokosa mwelekeo inayokandamiza wananchi.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kuharibu miundombinu ndio kuwabana mafisadi?
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Wanaopelekewa ujumbe unawafikia? Ingekuwa poa kama maandamano yanafanyika mwanza, mkuu wa mkoa wa mwanza ayapokee, asome jumbe mbali mbali na kuahidi kupeleka kunakohusika na awape waandamanaji "time frame" ya kuyafanyia kazi. Kinyume chake sijui kama maji ya kuwasha ndiyo husoma ujumbe toka kwa mabango ya waandamanaji au mabomu ya machozi ni kubufe cha "forwarding message" kwa walengwa
   
 7. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  maandamano yaendelee mpaka utawala utakaposhindwa na nguvu ya umma na kutawala kwa matashi ya umma. utawala ukishaanza hivyo, lazima mafisadi watatiwa hatiani. mafisadi wanalindwa na watawala. Utamaduni wa maandamano ya kupinga utawala usiotekeleza matakwa ya umma unafaa sana kujengwa miongoni mwa watanzania iwe ccm au cdm au chama chochote cha siasa madarakani. hatuhitaji kufanya uharibifu wowote kubadili mfumo wa utawala tz
   
 8. mkatofa

  mkatofa Member

  #8
  Nov 11, 2011
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutakacho fanya nikuongeza kasi ya kuwafundisha vijana jinsi ya kuandamana ,kamwe hatuwezi kumsikiliza pindi
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Wabomoe barabara kwa maslahi ya nani? Kama tunaipenda CDM tusiipotoshe! Labda kitu kimoja cha kuzingatia ni kuwa wanasiasa wengi wa bara la afrika wapo kwa maslahi binafsi zaidi kuliko yale ya wananchi/taifa. Umewasikia 'wabunge wetu' huko dodoma wanataka kuongezewa posho?
   
 10. m

  mchaichai JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 650
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maandamano nasema yaendelee tena kwa nguvu zote maana ndiyo njia iliyobaki kwa Tanzania maana hawa watawala wanafikiri siku hizi ni Busness as usual tu...watu wamebadilika siku hizi..na iwapo serikali inaona yanakera na solution ya yanayolalamikiwa ni mazungumzo kwa nini wakiombwa bila maandamano hawakubali? au wanafanya research ya kutaka kujua kama vijana wa siku hizi siyo kama zamani? kama ni utafiti basi majibu nafikiri wameyapata..kama mtu anaishi bila future kwa sababu ya unyanyasaji wa haki kuna haja gani ya kuogopa kufa kwa bunduki na maji ya kuwasha wakati hata ukiyaogopa bado siyo dawa ya huyo mtu asife? serikali itambue kwamba tabia nchi na kukosekana kwa dhamira ya dhati ya serikali kuwezesha wananchi kupitia raslimali za nchi ndicho kichocheo cha hasira za wananchi na wanaona kwamba nafuu wafe kuliko kuwa na maumivu ya roho maisha yao yote kwa kuona wananufaika wachache tu...tena mbaya zaidi wachache hao hawana hata huruma hata kidogo kwa masikini wanawaowa kwa magari yao, wanawapiga risasi makusudi, wanawanyang"anya mashamba yao waziwazi, sheria kwa masikini zinapindishwa..wanadanganywa kwa kauli za kisiasa tu bila vitendo..Mfano maisha bora kwa kila Mtanzania..Kilimo kwanza (kilimo cha mdomoni na kwenye makaratasi tu), elimu mbovu kwa masikini, matabaka katika huduma za jamii, kazi za kujuana ni mengi jamani yaani napenda kumwambia Waziri tunakerwa na mengi siyo ya Umeya wa Arusha tu!
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani huyu pinda sijui hata alitokeaga wapi..hakuna jitu ongo na nafiki kama hili zeee.
   
 12. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa hili la kuharibu miundombinu nafikiri una lako jambo. Unajifanya unaunga mkono hoja ya maandamano ila hapo hapo unachomekea hoja ya uharibifu wa barabara ili CDM ionekane inahamasisha uharibifu wa mali.
   
 13. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mbona wao wanatumia nguvu ya dola kama.mahakama,polis,majeshi na usalama wa taifa.kuna umuhimu wa kuwa na mawaziri wasiotokana na vyama vya siasa.kwani kwa kuchelewesha kutoa haki na kutatua mgogoro wa arusha kunakofanywa na serikali ndio kuliko sababisha machafuko.itambulike kuwa Pinda ni kada na mtiifu kwa c.c.m hana jipya.nguvu ya ndio silaha iliyobaki,na ndio maana c.c.m na serikali wanatetemeka n kujinyea kwa umma ndio mwisho yote.CHADEMA IMARA ITAJENGWA NA NGUVU YA UMMA.na sio mafisadi wachache kama ilivyo c.c.m.
   
 14. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #14
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Nguvu Ya Dola (CCM) v/s Nguvu Ya Umma (CHADEMA na wapenda nchi wote).

  Lazima waogope maana wanajua wao ni minority
   
 15. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Maandamano ni lazima yaendelee na yaboreshwe, ila kuharibu miundombinu hapana!?

  Huyu Pinda ni mwoga, mnafiki na hajiamini kabisa yaani sio hata wa kumsikiliza, yeye kila wakati ni kutafuta huruma ya wananchi, yaani watanzania tunahali mbaya sana yaani kuongozwa na watu wasiofikiri! ni balaa ambalo hatutakaa tulisahahu labda Dr wa Ukweli Slaa aingie ikulu.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,679
  Likes Received: 82,531
  Trophy Points: 280
  Pinda- Chadema badilikeni, acheni maandamano
  Imeandikwa na Na Waandishi Wetu, Arusha na Dodoma; Tarehe: 10th November 2011
  Habarileo

  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amekitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiache uanaharakati na maandamano ya mara kwa mara kama kinataka nchi isonge mbele.

  Pinda alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge katika mkutano wa tano wa bunge unaoendelea, Dodoma, akisema Chadema inahitaji kuteremka chini na kuangalia maslahi ya nchi kwa mapana zaidi.

  Alielezea kukerwa na mtindo inaoutumia wa kufanya maandamano kila kukicha na kaulimbiu yao ya ‘Peoples power (Nguvu ya umma)’ kwamba hazioneshi dhamira ya kweli ya kuleta amani.

  Alisema ipo haja kwa Chadema kubadilika, ili kuipa imani Serikali kukiona kuwa ni chama makini na kinachohitaji kumaliza mgogoro uliopo.

  Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) aliyesema kuwa mgogoro wa vyama vya CCM na Chadema wa umeya wa Arusha umevuka mipaka na kusambaa nchi nzima na kuwa wa kitaifa.

  “Hivi sasa (mgogoro huo) umevuka mipaka ya kivyama na umekuwa wa kitaifa na kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi na kwa kuwa (Pinda) ulilitambua hilo na ukaandika barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na baada ya kupokea majibu ya CCM je, upo tayari kutoa maelekezo mengine ama ushauri mwingine ili upande wa pili ujue hatima ya suala hili na ijue hatua za kuchukua?” Alihoji Mnyika.

  Pinda alijibu; “Ndugu Mnyika usilikuze jambo hili kama limesambaa nchi nzima, si kweli, lakini kikubwa ninachokiona katika mazingira ninayoyaona, wenzangu wa Chadema mnayoyafanya kinachohitajika ni dhamira ya kweli kwa pande zote mbili, kwa namna mambo yenu mnavyoyafanya huoni dhamira ya kweli.

  “Kila siku maandamano kila mahali sisi tulioko serikalini tunapata tabu sana, tunataka kufanya kazi nyingine ambazo zinahitajika, lakini muda wote unakaa unafikiria maandamano.

  “Mteremke chini kidogo, tuanze kuona maslahi mapana ya nchi, tuone ni mambo gani ya msingi yanahitajika, kwa pamoja twende mbele,” alisema.

  Alisema tabia ya uanaharakati ya Chadema inanipa taabu sana, lakini kama umakini utakuwapo, haoni tatizo watu kukaa na kuzungumza suala hilo, “katika hali ninayoiona mimi ‘peoples power’ kila kukicha si nzuri, haiwezekani.”

  Kuhusu mgogoro wa umeya wa Arusha, Pinda alisema kama Chadema inaona haja ya kukaa kwa mazungumzo iandike na kuelezea maeneo inayoyaona yanahitaji kujadiliwa.

  Awali Pinda alieleza kuwa aliingilia mgogoro huo kwa kumwelekeza Msajili akutane na vyama hivyo, kuona maeneo ya kuzungumza akiamini tatizo litapatiwa ufumbuzi lakini CCM ilijibu kwa barua kwamba haioni cha kuzungumza.

  Akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM), aliyetaka kufahamu kwa nini Serikali imemzuia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutoka rumande na kuathiri utalii, alisema Mbunge huyo hakuzuiwa bali mwenyewe alikataa dhamana.

  Alisema wanatarajia Novemba 14 kesi hiyo itakapotajwa, Mbunge huyo anaweza kuachiwa na kuongeza kuwa utalii haujaathirika kutokana na vurugu hizo, lakini akawataka wananchi kuzingatia amani ili utalii huo usiathirike.

   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu ni muongo tu au mpotoshaji. Mwenyekiti wa Chadema alishapendekeza mazungumzo yafanyike lakini yeye na CCM yake wamekaa kimya. Sasa kulalama tu bungeni kuwa teremkeni chini kutasaidia nini?
   
 18. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #18
  Nov 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu, kama ulivyomuita ni MSANII mwingine huyo!
  Ye ndio amekuwa wa kutafuna maneno yake kwenye suala aliloliingia kichwakichwa hadi akaitwa muongo!

  Kweli huyu mzee ni muongo muongo, cheki alivyosimulia suala la umeya na suala la Lema!
  Ni kinyume na ukweli na hatua alizopitia, makubaliano yake na Mbowe.... Ameyazungumziaje?
  Hakimu kukaidi barua ya wakili, amelizungumziaje?

  Kama waziri mkuu, amekazana kulaumu ndani ya bunge badala ya kuchukua hatua kama serikali...
  Hakika ni msanii mwingine huyu.

  Masikini nchi yangu, kwa kuwa na watu (rais na waziri mkuu wake na baraza zima) wa namna hii...!
  Miaka 50 ya uhuru
   
 19. B

  Bundajo JF-Expert Member

  #19
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pinda anamwogopa sana Luhanjo
   
 20. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #20
  Nov 11, 2011
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Hivi pinda anaexperience na tatizo lipi kati ya haya? Kupanda kwa gharama za maisha kulikosbabishwa na mfumuko wa bei na shilingi yetu kuporomoka, foleni barabarani, urasimu kwenye kila jambo hasa huduma za jamii, huduma mbovu sana za hospitali.

  Huko kigamboni wananchi wanaporwa ardhi na baada ya kupimwa viwanja vinagawiwa kwa vigogo au watu ambao surname zao zimekaa kiccm ccm, wanafunzi wa vyuo vikuu hawajapewa pesa waliyokopeshwa takribani mwezi na zaidi sasa, mgao wa umeme, kuibiwa sight mirror na vibaka wasio na huruma kwa vile wasipoiba hawali kabisa, kuombwa sh 100 na omba omba pale fire au ferry upande wa kigamboni.

  Kweli madaraka matamu maana naona mtoto wa mkulima amekuwa mtoto wa sultani. Chadema ndio waotufaa kwa sasa maana wako karibu zaidi na nawananchi kuliko nyie mnatupita na ving'ora!
   
Loading...