Pendekezo la namna bora ya kupata wafanyakazi wa umma wenye ufanisi, uadilifu na uchapakazi

Quinn

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
473
1,180
Binafsi nina boreka sana ninapoenda kwenye ofisi za umma unakuta huduma mbovu inayotolewa na watumishi:

Serikali inabidi ibadilishe mikataba ya wafanyakazi wa utumishi wa umma iwe ya miaka mitano mitano.

Kila baada ya miaka mitano yule mfanyakazi anafanyiwa tathmini ya kina ili kumuwezesha kuongezewa mkataba wa miaka mitano tena.

Hii itafanya watumishi wengi kujituma, kuwajibika na kuwa wabunifu kwenye sehemu zao za kazi.

Itasaidia kupata watu walio na nguvu na uchapakazi katika kipindi chote cha utumishi kwan kwenye ofisi nyingine unakutana na wazee hata kompyuta hawez kutumia.

Njia hii ya mikataba mifupi itasaidia hata watumishi wanapofanya makosa ya kiutumishi inamuwezesha kumuondoa kabisa na sio kuhamishwa ambako anapeleka ugonjwa huo sehemu nyngne.

Je wewe una maoni gani?
 
Back
Top Bottom