Uchaguzi 2020 Pendekezo la kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa 2020 to 2025

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,269
4,575
Kufuatia hali ya kutokuaminiana katika uendeshaji wa shuhuli za kisiasa ikiwemo chaguzi mbalimbali hapa nchini Tanzania, napendekeza badala ya kuitisha uchaguzi mkuu 2020 iundwe serikali ya umoja wa kitaifa itakayoshirikisha vyama vyote vyenye wabunge ili kufanya yafuatayo:-

(i) Pesa yote ya uchaguzi ielekezwe kugharamia na kusimamia mchakato wa katiba mpya itakayoweka mifumo ya uwajibikaji wa kitaasisi katika uendeshaji wa serikali na ugawanyaji wa madaraka

(ii) Kuweka mifumo thabiti na shirikishi ya uendeshaji wa serikali ikiwemo mchakato shirikishi wa kuwapata viongozi wakuu wa serikali na taasisi zake

(iii) Kuunda tume huru ya uchaguzi ambayo itaonekana kutoa haki sawa kwa washindani wote

(iv) Kuweka misingi ya kufanya uchaguzi mkuu wa 2025 chini ya tume huru ya uchaguzi.
 
Hatutaki Katiba nyingine, mbona wagumu kuelewa? Hamieni Kenya wana Katiba mpya na Karibik wanaaandika nyingine!
 
Hakika wewe huna unachomiliki na wala huna cha kupoteza ikitokea hali ya ghasia. Wenye cha kupoteza tunahitaji sana maridhiano ya kitaifa
 
Unasubiria vuguru ili upore mali za watu? Tunahitaji kuepusha hii hali ya kutokuaminiana maisha yaendelea kwa amani kama ilivyo jadi yetu sisi Watanzania.
Hatuhitaji vitisho vya kijinga kwa ajili ya wachumia tumbo, fanyeni kazi sio muda wa porojo. Porojo tumepiga sana tulichoambulia ni wizi mtupu, sasa tunataka maendeleo.
 
Kufuatia hali ya kutokuaminiana katika uendeshaji wa shuhuli za kisiasa ikiwemo chaguzi mbalimbali hapa nchini Tanzania, napendekeza badala ya kuitisha uchaguzi mkuu 2020 iundwe serikali ya umoja wa kitaifa itakayoshirikisha vyama vyote vyenye wabunge ili kufanya yafuatayo:-

(i) Pesa yote ya uchaguzi ielekezwe kugharamia na kusimamia mchakato wa katiba mpya itakayoweka mifumo ya uwajibikaji wa kitaasisi katika uendeshaji wa serikali na ugawanyaji wa madaraka

(ii) Kuweka mifumo thabiti na shirikishi ya uendeshaji wa serikali ikiwemo mchakato shirikishi wa kuwapata viongozi wakuu wa serikali na taasisi zake

(iii) Kuunda tume huru ya uchaguzi ambayo itaonekana kutoa haki sawa kwa washindani wote

(iv) Kuweka misingi ya kufanya uchaguzi mkuu wa 2025 chini ya tume huru ya uchaguzi.

That is daydreaming!! Forget about this and ask for forgiveness from the Creator.
 
Ccm hawawezi kukubali kwa namna yeyote katiba mpya ije wakati wanajua ndio mwisho wao dawa ni kuitisha maandamano yasiyo na mlengo wa chama cha kisiasa na kudai katiba.
 
Maandamano yana athari za kiuchumi kwenye biashara za watu na hata kuwavutia watalii kuja Tanzania. Mimi naamini katika maridhiano kuliko hii hali ya kutokuaminiana
 
Back
Top Bottom