Pendekezo la kumaliza mvutano wa muundo wa tume huru ya uchaguzi-CCM, CHADEMA na ACT Wazalendo zingatieni sana

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
"Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu"
Mithali 18:18

Mara nyingi kumekuwa na kawaida kwa vyama vikuu vya pinzani na Chama kinachotawala kuvutana na kutokukubaliana kabla au baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, iwe Tanzania bara au Tanzania visiwani.

Mara zote hizi lawama zimeelekezwa kwa refa/msimamiaji wa uchaguzi kuwa anaegemea upande wa watawala, sababu inayofanya wanaamini hivyo ni ule muonekano wa tume inayosimamia uchaguzi.

Yaani M'kiti, makamishna wa tume wanateuliwa na Rais na hapo Rais huyo huyo au mwenzake wa Chama chake akaingia kwenye mashindano.

Ni Kama Simba inacheza na Yanga halafu refa achaguliwe na M'kiti wa club ya Yanga. Kwa akili ya kawaida Simba haiwezi kutoboa hata iweje. Na hapo mmoja wa wasaidizi wa refa awe Manara.

Tume ya Uchaguzi sio tu inaaswa kuwa huru Bali ionekane kuwa iko huru na hapo ndipo shida ilipo. Yaani vyama vinavyogombea visishawishiwe kuwa tume iko huru Bali kwa macho yao wenyewe waone na kuthibitisha kuwa tume hiyo iko huru.

Kivipi?

Sisi Kama wananchi wapenda Amani, tunashauri mabadiliko ya muundo wa Tume kabla ya Uchaguzi 2025.

Endapo mchakato wa katiba mpya hautaweza kukamilika kabla ya 2025 basi Kuna haja ya kuunda tume ili KUPITIA MAPUNGUFU YA TUME ILIYOPO NA KUUNDA TUME HURU MPYA itakayoshirikisha wadau wote muhimu, viongozi wa dini,vyama vya siasa, asasi zisizo za kiserikali, wabobezi wa Sheria.

Miongoni mwa wanaoweza kusaidia upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi ni hawa wafuata:-
1.Jenetali Ulimwengu
2.Mama Helen Kijo Bisimba
3.Prof Mwandosya
4. Askofu Benson Bagonza
5.Jaji Warioba
6. Mzee Butiku
7.Ismail Jusa
8.Tundu Lissu
9.
10.
11.
Orodha inaweza kuendelea
(Lissu na Jussa kama WANASHERIA nguli ingawa na WANASIASA pia)

Tulimalize hili na maisha yasonge mbele.

Nchi hii tuipendayo ni yetu sote, tuipende na tupendane bila kujali uCCM , U CHADEMA, u ACT,. u NCCR hata u CUF. SOTE NI WATANZANIA.
HAKUNA MWENYE HATI MILIKI ZAIDI YA MWINGINE. TUIJENGE!
 
Kikawaida tu ni kwamba MNUFAIKA wa sasa ni ngumu mno kukubaliana na hayo mapendekezo .

LABLA WANANCHI WENYEWE WAAMUE BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA VYAO ILI KUJIPATIA MAENDELEO.
 
Back
Top Bottom