PENDEKEZO LA KIGEZO KIPYA CHA KUZISHINDANISHA SHULE-MATOKEO YA NECTA

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Naomba kupendekeza kigezo kipya cha kuzishindanisha shule kutokana na ufaulu wa mitihani ya NECTA. Kigezo kinachotumika sasa cha kuangalia GPA pekee kina mapungufu yafuatayo: Hakizingatii kwa ukamilifu factor ya idadi ya watahiniwa. Haiwezekani mtu aliyebeba mzigo wa zaidi ya kilo 100 (idadi hiyo ya wanafunzi) utegemee ashindane kwa mbio na mtu aliyebeba mzigo wa kilo 40 (idadi hiyo ya wanafunzi).
Pendekezo langu ni kuwa GPA itumike sambamba na idadi ya watahiniwa kwa ukamilifu wake. Kigezo hiki ndicho hutumika kuwashindanisha wanafunzi kwa wanafunzi. Wanashindanishwa kwa pointi na kwa idadi sawa ya masomo. Kwa O- level hushindanishwa kwa masomo 7 na kwa A-level hushindanishwa kwa masomo 3.
Kwa upande wa shule waamue idadi ya chini ya wanafunzi watakaotumika kushindanisha shule zenye watahiniwa wengi, na zile zenye watahiniwa kidogo. Kwa sasa idadi ya chini ya watahiniwa wanaofanya shule ishindanishwe na shule zenye watahiniwa wengi watahiniwa 40.
Pendekezo langu ni kuwa GPA ya watahiniwa 40 wenye matokeo bora zaidi kwa shule ndiyo itumike kama kigezo cha kushindanisha ufaulu wa shule na shule, kama yanavyotumika masomo 7 tu yenye ufaulu mzuri zaidi kwa mwanafunzi wa O-level na masomo 3 tu kwa mwanafunzi wa A-level yanayotumika kumpatia pointi na kisha divisheni. hata kama amefanya masomo zaidi ya hayo. Kwa kigezo hiki, hata shule kama ya Majengo iliyopo Moshi mjini yenye watahiniwa zaidi ya 700 itaweza kushindana na Kismiri yenye watahiniwa 60 tu!!!
Karibuni kwa mjadala huru!!
 
Haiwezekani shule yenye div I: 145 iwe chini ya shule yenye div I: 58
 
Back
Top Bottom