Pendekezo la Kidiplomasia: Diamond Platnumz Apewe Pasi ya Kibalozi (kama hana)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
1576852197080.png
Na. M. M. Mwanakijiji

Naomba kupendekeza kuwa huyu kijana apewe rasmi hati ya kusafiria ya Kibalozi (Diplomatic Passport). Nimekuwa nikifuatilia jinsi anavyoshirikiana na wasanii wengine ndani na nje ya nchi lakini pia jinsi gani anakubalika katika sehemu mbalimbali za Afrika. Nimefuatilia kwa karibu ziara yake inayoendelea huko Afrika ya Magharibi.

Ndugu zangu,

1. Hakuna Mtanzania ambaye si mtu wa serikali anayetangaza jina la Tanzania kama Diamond.

2. Kwa ndani ya miaka 10 hivi kijana huyo ameweza kutoka kuwa "the boy from Mbagala" to a "global phenom". Muda si mwingi, kijana huyu ataanza kupasua kwenye majukwaa makubwa ya nchi za Kimagharibi (siyo yale ya ukumbini tu). Kuna watu wenye majina ambao nao watataka kijana huyo awemo..

3. Kwa vile sasa ni mtu wa "kimataifa" Diamond aachane na haya malumbano ya kijiweni na siasa na "wadogo" zake. Ni lazia aanze kujionesha kuwa ni mtu wa namna yake.

Serikali itambue mchango wake - siyo tu katika kutoa ajira lakini pia katika uchumi. Hivyo:

1. Serikali impatie passport ya hadhi ya juu kabisa.
2. Anaposafiri nje ya nchi, Balozi zetu ziwe na taarifa na pale ambapo kuna balozi zetu basi anapoenda ni lazima apokelewe na kukutana na mabalozi wetu.
3. Apewe nafasi ya kubeba jumbe za kibalozi na hata kukutana na viongozi wa serikali huko anakokwenda na kubeba ujumbe kurudisha nyumbani.
4. Kwa jinsi anavyovutia vijana ni wakati makampuni ya Kitanzania (namaanisha hapa ya "Kitanzania" yashirikiane na serikali kumtumia Diamond katika kufungua biashara zao zaidi. Uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa tukijifungia ndani tu; ni lazima makampuni yetu yaanza kusambaa katika nchi za Kiafrika. Diamond kama jina na mjumbe anaweza sana kushawishi.
5. Ni vizuri kuhakikisha kuwa usalama wake anaposafiri. Hili watu wa serikali na kampuni ya Diamond wanahitaji kukaa chini kuona jinsi gani watahakikisha. Je, mnajua watu kama kina Jay Z, Beyonce, wanaposafiri kwenda nje ya nchi watu kama FBI wanajua na mara nyingi wanahusishwa kuhakikisha usalama wao?
6. Jeshi la Polisi lianzishe kitengo cha Ulinzi wa Watu Maalum (VIP Protection Unit) ambacho ni pembeni ya kile kinacholinda viongozi wa serikali. Kitengo hiki kitakuwa kinatoa ulinzi kwa watu wetu mashuhuri wanaposafiri nje ya nchi .. na kadhalika na kadhalika..

Ni mawazo mengine kem kem...
 
Huyo jamaaa tumwacheni Tu anawa-outclass watu vibaya mno , naishaur serikali impe support kimya kimya mana wakifanya public kuna watu Wana roho mbaya Sana watamharibia kijana wa watu , hasa clouds na genge lao
 
Mpira umetushinda, Michezo yote imetushinda mziki wetu pia ulikuwa na vipaji kibao uko nyuma ila tulishindwa ila Diamond kaonyesha uthubutu mkubwa nakuunga mkono mziki unaweza zaidi kututangaza kuliko kitu chochote kwa sasa.

kuna kipindi nilikuwa south nilikutana na jamaa mmoja baada ya kujitambulisha natoka tz alinambia kule anakotoka Diamond na Nyerere? nikamjibu ndio kuna jambo nilijifunza.
 
Una mawazo mazuri ya hapa na pale, lakini hicho kitengo unachopendekeza ni kama kutaka kwenda kuchukua pointi za mezani baada ya kuona mtu anafanikiwa, huku serikali haikuwa na mchango wowote kwa huyo mtu hapo alipofika. Wameshindwa kulinda watu wanatekwa na hawana majibu, saa hii unapendekeza wakawalinde watu waliofanikiwa kwa jitihada zao? Hicho kitengo kiwakamate walioshambulia Lisu, diamond kafanikiwa kwa jitihada zake.
 
Upo sahihi 100%.Jeshi la polisi liko outdated.Linatakiwa kuboreshwa na washirikiane na serikali TISS n.k kujenga diplomasia ya kiuchumi na kijamii.Lakin Jiwe bwana duh! Anaona ni mabeberu.Kwa jiwe hata Kenya ni mabeberu sasa sijui itakuwaje lakini vema fursa zikafunguliwa mfano masuala ya kielimu.Kujua wenzenu wanaelimika vipi,wanafanyaje ni muhimu maana naona balozi zetu zimeshindwa hata kujua hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una mawazo mazuri ya hapa na pale, lakini hicho kitengo unachopendekeza ni kama kutaka kwenda kuchukua pointi za mezani baada ya kuona mtu anafanikiwa, huku serikali haikuwa na mchango wowote kwa huyo mtu hapo alipofika. Wameshindwa kulinda watu wanatekwa na hawana majibu, saa hii unapendekeza wakawalinde watu waliofanikiwa kwa jitihada zao? Hicho kitengo kiwakamate walioshambulia Lisu, diamond kafanikiwa kwa jitihada zake.
Hivi unaweza vipi kusema hili bila kufikiria...?
 
Mpira umetushinda, Michezo yote imetushinda mziki wetu pia ulikuwa na vipaji kibao uko nyuma ila tulishindwa ila Diamond kaonyesha uthubutu mkubwa nakuunga mkono mziki unaweza zaidi kututangaza kuliko kitu chochote kwa sasa.

kuna kipindi nilikuwa south nilikutana na jamaa mmoja baada ya kujitambulisha natoka tz alinambia kule anakotoka Diamond na Nyerere? nikamjibu ndio kuna jambo nilijifunza.
Tunakumbuka jinsi Rais Mwinyi alipompokea Michael Jackson... muziki ni urafiki, muziki ni demokrasia.. na ni diplomasia..
 
Back
Top Bottom