Pendekezo la kamati la kuunda kitengo cha kushughulikia rushwa

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,465
2,000
Pendekezo la kamati la kuunda kitengo cha kushughulikia rushwa kubwa halikubaliki.

tunayo takukuru, chombo hiki kinatakiwa kufanya kazi hiyo na kama kimeshindwa ni swala la kujiuliza kwa nini? kama ni tataizo la mtandao tuvunje mtandao, kama ni tatizo la uwajibikaji tuwajibishe wahusika, kama ni tatizo la uzembe tuondoe wazembe wote.

tunachotaka ni system kufanya kazi, asiyetimiza wajibu wake tunamuwajibisha kwa kutokutimiza wajibu.

tuko katika mchakato wa katiba mpya kama tatizo ni mfumo wetu ni wa kulindana unatupeleka kurudi utumwani miaka ijayo kwa wajukuu wetu kukuta tumeibiwa kila kitu tumewapa wageni kwa kuwahonga ndugu wenzetu na wakabaki kutumikishwa tu ni wakati sasa wa kukataa hayo kwa vizazi vyetu na maisha magumu kwa kila mtanzania.

dawa ni kuwajibishana.

aliyepewa dhamana anafanya kosa anayemsimamia amuwajibishe, ukishindwa kumuwajibisha uliyetakiwa kumuwajibisha na wewe umekuwa mshirika na aliyeko juu yako anawajibisha nyote alifanya kosa na aliyeshindwa kuchukua hatua.

mwisho ni wajibu wetu sisi wananchi kuwajibisha serikali kama inashindwa kusimamia mali zetu. hapa tunahitaji kutuliza akili zetu serikali ikichukua hatua tunawapongeza, atakayetuchezea tunawajibisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom