Pendekezo la dhati kwa CCM

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,411
8,809
Wadau, heshima kwenu,

Wana-CCM wote, hivi Katiba ya CCM inasemaje kuhusu muda wa 'hand-over' ya UENYEKITI wa chama? Kama kuna loop-hole ya kikatiba inayoweza kuruhusu 'speed-up' ya kumkabidhi Rais Magufuli uenyekiti wa Chama, basi ni vyema wana-CCM wote mkalifikiria hili kwa haraka.

Kama mzalendo wa nchi yangu, binafsi nimeridhika na utendaji wa Rais wetu Dkt Magufuli, hakika ameanza na kasi nzuri inayomfurahisha mtanzania yeyote mzalendo. Huku 'site' tuna imani kubwa sana na Rais wetu. Ni tumaini letu kuwa kasi aliyoanza nayo haitakuwa 'nguvu za soda', bali kasi itaendelea na kuongezwa zaidi kwa ajili ya ustawi wa Taifa hili lililoendeshwa 'kimagumashi' na baadhi ya watangulizi wake.

Huku 'site' tunaona kila dalili ya Rais wetu kufungwa 'speed governor' na Chama chake. Tunaona kabisa kuwa kuna baadhi ya maeneo aidha anasitasita ama anashindwa kuyashughulikia ipasavyo kwa vile tu anapata influence fulani kutoka ndani ya chama chake cha CCM, chama ambacho (kwa mtazamo wangu) majority ya viongozi ni watu wa 'deal na magumashi'. Chama kinamfunga speed governor Rais ili mafisadi wafunike na kusawazisha maovu yao kukwepa mkono wa dola.

Hivyo basi, kama Katiba ya CCM inaruhusu, napendekeza kwamba chama kikabidhi haraka uenyekiti wa chama kwa Mheshimiwa Rais. Naamini kuwa endapo Rais akipewa 'full power' ndani ya chama chake as a Chairperson, atakuwa huru zaidi katika kusimamia na kuongoza nchi, kuliko ambavyo akiwa hana 'full power' ndani ya chama.

Please, wana-CCM wote hebu put this into consideration with urgent attention. Tusingojee mafisadi waendelee kuincontrol speed ya Mh Rais. Embu unganeni wote katika hili kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Mpeni haraka mh Rais 'rungu' la uenyekiti wa chama alafu sasa tuone the 'next episode' ya movie yetu.

Mh Magufuli akishapata UENYEKITI wa CCM Taifa, I guarantee you kuna watu hapa nchini wataanza kupumulia pua moja!

Rais Magufuli + Uenyekiti wa Chama = Ngoma inogile !

K.N.Y :
Ordinary citizens from 'site' .


-Kaveli-
 
Back
Top Bottom