Pendekezo la 1: Tanga, Bagamoyo, Mafia na Pangani ziwe sehemu ya Zanzibar!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
PENDEKEZO LA 1:TANGA, MAFIA, BAGAMOYO NA PANGANI ZIWE SEHEMU YA ZANZIBAR!

Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni pendekezo la kwanza kati ya mapendekezo kadhaa ambayo nitayatoa katika kusaidia kuleta fikra mpya katika mijadala mbalimbali ya kitaifa ambayo lengo lake ni kutupa uwanja mkubwa zaidi wa kuweza kufanyia maamuzi. Miaka 46 imepita tangu Muungano pekee wa nchi mbili za Kiafrika uasisiwe na hivyo kujenga katika bara la Afrika nchi pekee ambayo mipaka yake haikurithishwa na wakoloni! Tanzania tunayoishi leo hii ni tunda na zao la Watanzania wenyewe.

Pamoja na matatizo yote yaliyopo Muungano wetu unapaswa kutetewa, kulindwa na kudumishwa si kwa sababu ya woga, si kwa sababu hauwezi kuvunjika, na si kwa sababu hautakuwa na matatizo huko mbeleni. Tunapaswa kuulinda, kuudumisha na kuuboresha kwa sababu moja tunaupenda kwani ndio nchi pekee tuliyoijenga kwa ajili yetu sisi na watoto wetu.

Ninaamini kabisa kuwa siku watawala wetu watatoka kwenye ufinyu wa fikra wanaouonesha siku kwa siku wataweza hatimaye kuja na mapendekezo ya kuuboresha Muungano wetu na kuufanya uwe kwa faida ya kila Mtanzania na kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na ambayo utatuzi wake unahitaji dakika chache tu za fikara. Pendekezo hili, halijawahi kutolewa na mtawala yeyote, hawawezi kulitoa kwani hawana uwezo wa kifalsafa kulitetea! Hawawezi kulikumbatia kwa uharaka kwa sababu wamefungwa na siasa zao za utengano hadi wanatia aibu. Hili hata hivyo, haliwezi kuwazuia Watanzania wengine kutoa mawazo yao na kuyasogeza mbele kama pendekezo ili kila Mtanzania ajue kuwa hatuhitaji wazungu watuletee mapendekezo yao ili tuyakumbatie kama yameletwa na wajumbe wa Mungu! Hili ni pendekezo la kuthubutu, la nguvu, la mkakati, la kisiasa, la kiutu, na la kiumoja kuliko mapendekezo mengine yote yaliyowahi kutolewa kuhusu kudumisha Muungano au kuondoa “kero za Muungano”.

READ AT YOUR OWN INTELLECTUAL PERIL!
View attachment PENDEKEZO LA 1.doc
 
Mchungaji; kizazi kipya hakina budi kuja na mapendekezo yake yenyewe nje ya siasa za utengano! NI lazima tufikirie nje ya kijisanduku kidogo walichotuachia na kuanza kufikiria na kwenda kule ambako hakuna aliyewahi kwenda!
 
tanga, mafia, bagamoyo na pangani ziwe sehemu ya zanzibar!

mmh.....tunatengeneza bomu sasa......likilipuka...mzee mwanakijiji mimi simo!!!!
kufanya hivi ni kuuvunja kwa style yake pasipo makali,hawa watu pamoja...balaaah
 
Ni mawazo mazuri MMKJ. Hongera kwa kufikiria hilo maana vinginevyo tutabaki tunauzunguka mbuyu tu kila siku, wakati kuna mtu alituasa kimbembe ni kujaribu kuukumbatia.
 
PENDEKEZO LA 1:TANGA, MAFIA, BAGAMOYO NA PANGANI ZIWE SEHEMU YA ZANZIBAR!

Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni pendekezo la kwanza kati ya mapendekezo kadhaa ambayo nitayatoa katika kusaidia kuleta fikra mpya katika mijadala mbalimbali ya kitaifa ambayo lengo lake ni kutupa uwanja mkubwa zaidi wa kuweza kufanyia maamuzi. Miaka 46 imepita tangu Muungano pekee wa nchi mbili za Kiafrika uasisiwe na hivyo kujenga katika bara la Afrika nchi pekee ambayo mipaka yake haikurithishwa na wakoloni! Tanzania tunayoishi leo hii ni tunda na zao la Watanzania wenyewe.

Pamoja na matatizo yote yaliyopo Muungano wetu unapaswa kutetewa, kulindwa na kudumishwa si kwa sababu ya woga, si kwa sababu hauwezi kuvunjika, na si kwa sababu hautakuwa na matatizo huko mbeleni. Tunapaswa kuulinda, kuudumisha na kuuboresha kwa sababu moja tunaupenda kwani ndio nchi pekee tuliyoijenga kwa ajili yetu sisi na watoto wetu.

Ninaamini kabisa kuwa siku watawala wetu watatoka kwenye ufinyu wa fikra wanaouonesha siku kwa siku wataweza hatimaye kuja na mapendekezo ya kuuboresha Muungano wetu na kuufanya uwe kwa faida ya kila Mtanzania na kuondoa manung'uniko yasiyo ya lazima na ambayo utatuzi wake unahitaji dakika chache tu za fikara. Pendekezo hili, halijawahi kutolewa na mtawala yeyote, hawawezi kulitoa kwani hawana uwezo wa kifalsafa kulitetea! Hawawezi kulikumbatia kwa uharaka kwa sababu wamefungwa na siasa zao za utengano hadi wanatia aibu. Hili hata hivyo, haliwezi kuwazuia Watanzania wengine kutoa mawazo yao na kuyasogeza mbele kama pendekezo ili kila Mtanzania ajue kuwa hatuhitaji wazungu watuletee mapendekezo yao ili tuyakumbatie kama yameletwa na wajumbe wa Mungu! Hili ni pendekezo la kuthubutu, la nguvu, la mkakati, la kisiasa, la kiutu, na la kiumoja kuliko mapendekezo mengine yote yaliyowahi kutolewa kuhusu kudumisha Muungano au kuondoa "kero za Muungano".

READ AT YOUR OWN INTELLECTUAL PERIL!
View attachment 9855

mzee mwanakijiji naona kilimo kimekuvuruga akili sasa, unahitaji kupumzika utulize akili kwanza kabla ya kutoa mapendekezo yako.
 
mzee mwanakijiji naona kilimo kimekuvuruga akili sasa, unahitaji kupumzika utulize akili kwanza kabla ya kutoa mapendekezo yako.

unatakiwa utoe sababu kwanini pendekezo hili ni baya, halina msingi, halifai au ni pendekezo la mwendawazimu.. so far hakuna ambaye anaweza kuonesha kuwa ni pendekezo baya! I dare say NONE! Kama yupo na amesoma nilichoandika na anyoshe kidole atoe sababu zake. Kama wewe unaweza thubutu tu.
 
Vikishaungana viwe chini ya uongozi wa nani? Itakuwa vile vile tu "shamba la bwana kheri na mbuzi wa bwana kheri".
 
Mwanakijiji kwa Wazanzibari hili sio pendekezo geni - Ukanda wa Maili 10 katika Pwani ya Tanzania Bara ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar!

Swali: Hivi watu wanaoishi kwenye huo Ukanda wanajichukulia kuwa wao ni Wazanzibari - je, walikuwa wanajiona hivyo toka zamani?
 
I am from Tanga and I respectfully disagree with you mkuu. I am bias in this issue and I do not want my home region as part of Zanzibar. My great grandfather was a Tanganyikan and I would rather be that first then become a Zanzibari.
 
Mwanakijiji kwa Wazanzibari hili sio pendekezo geni - Ukanda wa Maili 10 katika Pwani ya Tanzania Bara ilikuwa ni sehemu ya Zanzibar!

Swali: Hivi watu wanaoishi kwenye huo Ukanda wanajichukulia kuwa wao ni Wazanzibari - je, walikuwa wanajiona hivyo toka zamani?

Companero.. ndio my subliminal message hapa; watu wanaposema "Wazanzibari" wanataka kumaanisha nini kwa sababu historically na kwa muda mrefu "Zanzibar" Haikumaanisha Unguja na Pemba kama vile Azania haikumaanisha bara ya Afrika ya Mashariki tu. Kujiona Wazanzibari kivipi, Sultani alikuwa na makazi yake pale Pangani pia pembeni ya Mto Pangani! na alikuwa na wawakilishi hadi Bagamoyo na Tanga huko.

Kuna mtu kauliza itakuwa chini ya uongozi wa nani; nimeandika hapo.

Mwanafalsafa.. hata mimi niko biased sana na Tanga.. lakini ukweli ni kwamba, mji wetu utarudishiwa utukufu wake wa zamani; kumbuka sizungumzii "mkoa wa Tanga" wote.. nazungumzia Tanga mjini na Pangani.
 
Talking about solving a problem which is not there in the first place..This is funny enough.
 
hebu fafanua kwanini?
wanaongea lugha moja hawa,jeshi kubwa hili la ubishi,ung'ang'anizi, sijaona,waking'anga' lao lazima liwe...........wakikaa pamoja watajitia wanaweza nawataanza kelele kuwa wanaonewa, watatpigania kuuvunja wao,mwarabu nae atawasaidia maana ni mtoto wa shangazi yao,bibi yao,mjomba wao.kasheshe itakuwa kubwa,kadhi.....oic.....tutauvunja tuu kupisha upuuzi wao.kasheshe itaanza wakishafanikiwa,kila mtu atataka kuongoza.......
upo hapo??
 
Pendekezo hili halifai kwa mazingira na wakati tulionao sasa. Nililisoma pendekezo hili kwenye TD ya juzi. Nikalirudia leo humu sijaona hoja nzito ya kunifanya nikubaliane nawe Mwanakijiji. Tukianza kutengeneza upya mipaka yetu hatutaishia hapo. Haya mambo ni sawa na kula nyama ya mtu. Najua wewe muumini mzuri wa Mwalimu. Umenielewa. Wala usije ukadhani Pemba na Unguja ni "NCHI" moja.
 
mai wasu..........!!!!!!!!

bagamoyo iende zanzibar???

mzee mwanakijiji hivi umepata mbole ya ruzuku mzee, kama umepata elekeza nguvu zako huko kwenye kilimo.

hili pendekezo lako ni next to imposibo!
 
Back
Top Bottom