Pendekezo kwa Wizara ya Afya na Serikali ya JK

BabaH

Senior Member
Jan 25, 2008
103
8
Ndugu Watanzania napenda kutoa maoni yangu ambayo kwa namna moja au nyingine, nimekuwa nikiumia sana tena sana kwa mambo ambayo yanatokea Tanzania

Katika Hospitali zetu tumekuwa na matatatizo kibao ambayo yanasababisha vifo vya kujitakia na vya kizembe, nasema haya kwa sababu nyingi tu


1. Hatuna Hospitali za kutosha katika nchi yetu
2. Hospitali zilizopo zimejengwa sehemu ambazo wananchi hawakai, hii namaanisha kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanaishi vijijini ambapo Hospitali hakuna, na hawana uwezo wa kuja Mjini kwenye hizo mnazoziita hospitali

3. Madawa hakuna ya kutosha kwenye hizo hospitali zetu
4. Hatuna wataalamu wa kutosha kwenye hospitali zetu

Lakini ukumbukwe kwamba haya matatizo yote niliyoyaeleza hapo juu yanatatulika kama tutakuwa na nia ya dhati
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom