Pendekezo kwa Jeshi la Polisi, Viongozi na Wanajamii wengine

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Miaka ya hivi karibuni Tanzania tumeibuka na msamiati mpya ambao sio rasmi wa neno "watu wasiojulikana"

Nasema sio rasmi kwasababu kwenye kamusi yetu hilo neno halipo na duniani hakuna watu wasiojulikana. Kila mtu anatambulika kwa jinsia, utaifa, na wakati mwingine hata kwa rangi ya ngozi yake

Pendekezo langu tusiendelee kutumia hili neno panapotokea tukio baya la kushambulia, kuumiza, kuua, kuiba ama kupola linalofanywa na watu.

Badala yake kama mtendwa au shuhuda atakuwa amebahatika kuwaona anaweza kutaja jinsia ya watu walifanya tukio, kwa kusema "nimeshambuliwa na wanaume watatu, wanne, nk" na akiwa vizuri anaweza hata kutoa makadirio ya umri, muonekano nk

Kama hawatakuwa wameonekana kabisa jeshi la Polisi au viongozi watakao toa taarifa ya tukio hilo ni vizuri wakatumia neno kama "watu wenye nia ovu, nk

Kwanini napendekeza kutotumia "watu wasiojulikana"?

Hili neno nikama limewapa heshima fulani hao wahalifu kwasababu mtu yeyeto akifanya jambo baya na asiweze kujulikana mwisho wa siku anaishia kujigamba na kujiona anaweza kufanya lolote na asijulikane.

Hayo ni mawazo yangu, unaweza kushauri ya kwako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom