vunjo
JF-Expert Member
- Jun 2, 2011
- 1,323
- 2,607
Nilikuwa na wazo katika mkoa wetu Dar es Salaam nafikiri likikifanyika litapunguza msongamano wa magari kwa asilimia kubwa.
Nilikuwa nafikiria zikisajiliwa daladala za VIP ambazo zitakuwa na Air conditioning usafi wa hali ya juu zikapiga ruti mfano Tegeta- Posta kwa Tsh 3,000 na abiria wote level seat hakuna kusimamisha abiria.
Kwa asilimia kubwa watu wataacha magari binafsi nyumbani na kutumia usafiri huu kwani kwa kiasi kikubwa wataokoa gharama za matumizi ya mafuta pia zitawaepusha misongamano ya kubanana kwenye daladala na pia mtu kufika ofisini kwake akiwa bado nadhifu na bila uchovu wowote.
Usumbufu abiria wanaopata kwenye daladala za kawaida unafanya watu wengi kukopa kupata usafiri binafsi ambao ndio huongeza msongamano kwenye barabara zetu hizi.
Kwenye Mabasi ya mikoa yapo VIP na Treni pia kuna madaraja tofauti hata ndege kwa nini kwenye daladala isifanyike.