Pendekezo Korofi: Wabunge na Madiwani Wakatazwe Kufanya Hili

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,872
Hivi nini kitatokea endapo Wabunge na Madiwani watakatazwa kisheria kutoa misaada binafsi kwenye majimbo au sehemu mbalimbali? Binafsi, naamini wabunge na madiwani - lakini hasa wabunge - wakatazwe kutoa misaada kutoka kwenye mifuko yao au 'marafiki zao' kwenye majimbo yao. Wasiruhusiwe kutoa misaada ya mabati wala mbao, baskeli wala kalamu! Wapigwe marufuku kisheria kutoa misaada ya magari wala majengo.

Hili liwe sehemu ya mambo ambayo Sheria ya Maadili ikataze mara moja na wanaovunja hili wapigwe faini (kutoka kwenye mishahara yao) na watakaorudia iwe sababu ya kufuta Ubunge wao!

Wamepokea misaada ya Pikipiki 16 toka kwa MBunge wa Isimani - William Lukuvi (faili)

DSC_0739.JPG

Mbunge wa Mpanda Vijijini naye alitoa misaada ya vifaa vya umeme

mwalimu.JPG

Mgimwa naye akitoa misaada jimboni kwake

blogger-image-988172815.jpg

Mbowe naye akitoa misaada

DSCF4448.JPG

Nini kitatokea wabunge wakipigwa marufuku kisheria kutoa misaada majimboni kwao?
 
Binafsi siungi mkono mbunge au diwani au mtu yeyote kutuma fedha mfukoni mwake zisizoratibiwa kirasmi kutoa kinachoitwa misaada ya maendeleo. Kwanza hii si endelevu halafu ina harufu za rushwa. Kwahiyo ikipigwa marufuku itakuwa bora. Mtu akitaka kuchangia apeleke katika mfumo rasmi ambao matumizi yake yataratibiwa kulingana na mpango wa maendeleo wa eneo husika.
 
Mara nyingi neno msaada linatumiwa vibaya, yaani mbunge kaamua kupeleka mabati katika moja ya vijiji vya jimbo lake, au kaamua kununua mifuko hamsini ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji fulani, huo sio msaada. Anachangia maendeleo ya wapiga kura wake, inafaa tutumie neno kuchangia maendeleo kuliko neno msaada. Nadhani hilo neno msaada halivutii masikioni, linabeba chembechembe za dharau ndani yake. Ni ushauri wangu.
 
Hivi nini kitatokea endapo Wabunge na Madiwani watakatazwa kisheria kutoa misaada binafsi kwenye majimbo au sehemu mbalimbali? Binafsi, naamini wabunge na madiwani - lakini hasa wabunge - wakatazwe kutoa misaada kutoka kwenye mifuko yao au 'marafiki zao' kwenye majimbo yao. Wasiruhusiwe kutoa misaada ya mabati wala mbao, baskeli wala kalamu! Wapigwe marufuku kisheria kutoa misaada ya magari wala majengo.

Hili liwe sehemu ya mambo ambayo Sheria ya Maadili ikataze mara moja na wanaovunja hili wapigwe faini (kutoka kwenye mishahara yao) na watakaorudia iwe sababu ya kufuta Ubunge wao!

Wamepokea misaada ya Pikipiki 16 toka kwa MBunge wa Isimani - William Lukuvi (faili)

DSC_0739.JPG

Mbunge wa Mpanda Vijijini naye alitoa misaada ya vifaa vya umeme

mwalimu.JPG

Mgimwa naye akitoa misaada jimboni kwake

blogger-image-988172815.jpg

Mbowe naye akitoa misaada

DSCF4448.JPG

Nini kitatokea wabunge wakipigwa marufuku kisheria kutoa misaada majimboni kwao?

Kuwe na utaratibu maalumu vikuisanywe vipelekwe. Kwanza sasa hivi hata shule/ Institutions zenyewe zitakuwa zinazidiwa na wageni na kuharibu hata muda wa kufundishwa. hata hawa wabunge mara ooh wameenda kuangalia vyoo, madarasa no. Lazima utaratibu ufuatwe la sivyo mwalimu Mkuu itakuwa kazi yake kupikea mara mawaziri, mara wabunge , mara madimwani, mara Meya. Utaratibu uandaliwe!!!
 
Hii hoja ya mzee mwanakijiji kwa kweli ni ya muhimu sana ukiangalia kwa jicho pevu,
itasaidia sana kufanya siasa safi na watu kupractice maana halisi ya ubunge(uwakilishi) pia kuondoa makando kando yaliopo sa hivi kwa hawa wawakilishi wetu.
 
Mara nyingi neno msaada linatumiwa vibaya, yaani mbunge kaamua kupeleka mabati katika moja ya vijiji vya jimbo lake, au kaamua kununua mifuko hamsini ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji fulani, huo sio msaada. Anachangia maendeleo ya wapiga kura wake, inafaa tutumie neno kuchangia maendeleo kuliko neno msaada. Nadhani hilo neno msaada halivutii masikioni, linabeba chembechembe za dharau ndani yake. Ni ushauri wangu.

Duh kweli tumeharibiwa; ndio maana mwanzoni tuliwaita "wafadhili" siku hizi tunawaita "washirika wa maendeleo"! From Donors to Development Partners! Na ombaomba wabadilishwe majina - kutoka Ombaomba hadi Wenye Kiu ya Maendeleo!
 
Hakuna haja ya kutunga sheria kuweka katazo hilo...ishauri serikali ihakikishe huduma zote zinawafikia wananchi...

Kama zahanati ipo kwa nini mbunge alete mabati.
Kama ambulance zipo kwa nini mbunge anunue kwa hela yake.
Ajira za uhakika ziwopo mbunge alete bodaboda za nini.

Naamini kwa ukaribu ulio nao na watawala watakusikiliza
 
Weka sababu za pendekezo lako otherwise umekula maharage ya wapi mzee?
Hujamjua huyo! Hapo anamtafuta Nasari kwa vile kanunua vitanda vya hospitali kule Arumeru. Huyo jamaa ni hatari sana anapoamua Kutumika katika propaganda. Issue ya Nasari kujitolea kwa moyo wake kuna watu imewaumiza
 
Mara nyingi neno msaada linatumiwa vibaya, yaani mbunge kaamua kupeleka mabati katika moja ya vijiji vya jimbo lake, au kaamua kununua mifuko hamsini ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji fulani, huo sio msaada. Anachangia maendeleo ya wapiga kura wake, inafaa tutumie neno kuchangia maendeleo kuliko neno msaada. Nadhani hilo neno msaada halivutii masikioni, linabeba chembechembe za dharau ndani yake. Ni ushauri wangu.
Pia hii "misaada" inaweza kuwa rushwa nzuri sana kwa wapiga kura ili kuhakikisha unaendelea kupigiwa kura uchaguzi unaofuata.
 
Hujamjua huyo! Hapo anamtafuta Nasari kwa vile kanunua vitanda vya hospitali kule Arumeru. Huyo jamaa ni hatari sana anapoamua Kutumika katika propaganda. Issue ya Nasari kujitolea kwa moyo wake kuna watu imewaumiza
Kama kungekuwa na huu upuuzi jimbo la nasari lingekuwa kama chamwino kule watu wanahakili kama punje ya haradani
 
Hoja au mapendekezo ya mtu aliye out of touch... Hata huko ulipo kuna viongozi wa kuchaguliwa wanatoa misaada uner their name of their charities, sasa sijui inakuaje unaleta haya wakati Tanzania unaijua

I think you are doing this simply kwasababu umeona mwamko wa wabunge wa ukawa kuchangia maendeleo ya majimbo yao... Kinakuwasha, kinakuuma, kinakukereketa na kukupwita

Wacha watanzania tuishi kitanzania, wewe kama unaipenda sana tanzania rudi nyumbani tuishi wote the "real life"
 
Hujamjua huyo! Hapo anamtafuta Nasari kwa vile kanunua vitanda vya hospitali kule Arumeru. Huyo jamaa ni hatari sana anapoamua Kutumika katika propaganda. Issue ya Nasari kujitolea kwa moyo wake kuna watu imewaumiza
It is funny, kinamuwasha kuona Lwakatare na Nassari wameanza kwa kasi

Jamaa anatafunwa na his own hypocrisy
 
Back
Top Bottom