Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

MASSHELE,
Wazo lako ni zuri sana sana.
Ila ili mafunzo yafanyike na kujifunza kuwepo, lazima kila somo au mada iwe na vitu vitatu

Wanafunzi (ambao wapo wengi sana)

Walimu/Wakufunzi/Wahadhiri (wapo japo sio wengi kwa uwiano wao vs wanafunzi ili mafunzo yafanyike kwa ufanisi na tija)

Vitabu vya kiada (text books) vitabu vya ziada (reference books) na supplementary materials (madesa ya ziada) kama journals, tafiti n.k.

Tuanze na darasa la kwanza mpaka kidato cha 4. Nianzie hapa juu. Kama ni fizikia, sayansi kilimo (agri. Sc), biolojia, kemia hata kwa vitabu vya kingereza vya (reference books na supplimentary) na vimeandikwa kwa ufasaha na watu wetu ambavyo hata tukijipa muda kuvitafsiri right away mwaka unaufuatia kiswahili liwe somo la kujifunza kwa masomo yote kuanzia chekechea mpaka kidato cha 4 au 6.

Tukiweza hapo msingi uko poa. Sasa kama bado watoto wanafaulu, madarasa tu baadhi ya shule hayawatoshi watoto. Madarasa ni product ya saruji na mchanga na mafundi wajenge, wapige paa; walimu wapo kwa waikiwepo shule inaanza.

Mchonga alikuwa muumini sana wa kiswahili na hakufanikiwa. Tunahitaji kwenda huko; ila sio kwa ku-rush
 
Naona haujanielewa, kiingereza ni lugha kama lugha zingine, ili kuielewa vizuri iwe lugha ya kufundishia toka primary school, sio kukutana nayo juu kwa juu secondary, hiyo ndio njia pekee, hauna sababu ya kufundishana kiswahili hata publication za kiswahili tu hamna itabidi tutafsiri publications kibao ambapo huo uwezo hatuna, kiswahili kingebaki kama somo, hao viongozi wenyewe watoto wao hawasomi shule zinazofundisha kiswahili, why? Sababu wanajua ni upuuzi! Mmebaki nyie wanyonge na watoto wenu.
Hata tukifundisha toka primary hatutakielewa vizuri ila tutakielewa kuliko sasa. Njia nzuri ya kujifunza lugha ni kuiongea. Kama hatutumii kiingereza sokoni, nyumbani nk, hatutakaa tukielewe vizuri.

Nani kasema hatuna uwezo wa kutafsiri hizo publications? au unaona uvivu. Hao viongozi na hata tunaunga mkono kiswahili tunapeleka watoto huko medium ili kumwandaa na kiingereza cha sekondari na siyo eti kuwa elimu inayotolewa kwa kiingereza ni bora. Tungekuwa tunasoma kote kiswahili kusingekuwa na haja.

Tatizo letu bado tunafikiri kujua kiingereza ndiyo usomi. Ni ujinga ndiyo unafanya tushabikie matumizi ya kiingereza na ni zao la ukoloni. Msumbiji wanaona kireno ni bora, Congo wanaona kifaransa ni bora ila kiswahili upuuzi. wanaona Kiingereza tujifunze kama lugha, tuanze na kujifunza na mandarin.

Huwezi kuwa nchi ya kisomi kwa wasomi wa kukariri. Ongea na mtu wa digrii Tanzania, utagundua ananukuu notes.

Kuna mfano kuwa kiswahili kinaleta ubunifu, wamisionari walitafsiri biblia, wakatufundisha na tukaielewa vizuri, leo kuna wabunifu kama Gwajima, Kakobe, mzee wa upako nk, wanaenda hadi ulaya kuhubiri. Unafikiri tungeweza kama tungefundishwa biblia na thy, thee na thou?
 
Yaan kuna mijitu inàpenda kudanganya wenzao,wengi wao wanaoanzshaga swala hili n ambao wameshakfaham kiingereza alafu hawatak wengne wakjue,KIINGEREZA N KAMA MAJI,USIPO KINYWA UTAKIOGA
 
Acheni ujinga kiswahili hakitoshi!hakina maandiko ya kutosha!!!wakenya wamejitahidi sana kuwekeza kwenye kiswahili!Na watz wasomi wameona Taaluma hailipi wote tunawaza kuwa wanasiasa kwasababu siasa inalipa!!!TZ ELIMU NI UJINGA TENA SIO HALISI NA HAILIPI BALI NI KAMA CV YA KUTUMIKA KISIASA!!!MWAKYEMBE,KABUDI NA NK. WANGEKUA CHUO KIKUU WANAFUNDISHA LAKINI WAKAONA NI UPUMBAVU HAO KWENYE SIASA!!!
 
Wanangu siwezi wafundisha kiswahili Mimi sijaona faida take! Kalugha ka kuunga unga kako kwa ajili ya kujazana ubishi tu. Hivi taaluma za kuunda meli, ndege, udaktari nk utatumua kiswahili gani kuwaelewesha wanafunzi? Hebu tuache ujinga basi!
Wewe ndiyo mjinga unapochukia kiswahili na kukumbatia lugha ya kigeni.
 
Huu ndio wakati wa kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini

Pamoja na Kiswahili kupitishwa na Sera ya elimu mwaka 2014 bado hakijaanza kutumika kufundishia masomo katika elimu ya upili na elimu ya juu.

Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inasema Kiswahili pamoja na kingereza zitakuwa ni lugha za kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu, lakini takribani miaka 6 imepita bila suala hilo kutekelezwa.

Tafiti nyingi zilizofanywa zilionesha kuwa lugha ambayo unaweza kuwapa maarifa na kuwafanya wanafunzi kuwa wavumbuzi ni kiswahili (rejea utafiti wa Mzee Makweta) licha ya tafiti kuonesha kuwa Kiswahili kilifaa kutumika kufundishia bado wadau wamekuwa wakilegalega kutoa maamuzi.

Mwaka 1991 ilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuanza kufundishia masomo yote kwa Kiswahili lakini ilishindikana kutokana na ugumu wa kufanya maamuzi badala yake wakaishia kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano rasmi chuoni hapo.

Wapo baadhi ya watu pamoja na wataalam wengine wasio fuatilia mambo na kufanya uchunguzi wanaobeba madai yasiyokuwa ya kweli kuwa hakuna vitabu!

Mwaka 1972 vitabu vya Kemia na Baiolojia vya Lambert na Habort vilitafsiriwa na kuwa kwa Kiswahili kama mataifa mengine ya ulaya yalivyotafsiri vitabu hivi kuwa katika lugha zao.

Pamoja na hayo kwa sasa kuna vitabu vya Kiswahili vya sekondari vya Historia, Biolojia, kemia, fizikia, Geografia nk. Vilivyoandikwa kwa kiswahili.

Kiswahili kinavyoweza kutumika kufundishia masomo yote
Kiswahili kinaweza kuwa lugha ya kupitishia maarifa huku lugha ya Kingereza na lugha nyinginezo zifundishwe kama kozi ya lazima kuanzia awali hadi vyuo vikuu kuliko kingereza cha sasa kinachofundishwa kama somo na kutofuata kanuni zozote za ufundishaji lugha ya kigeni.

MKAZO
Hakuna nchi yeyote yenye maendeleo ya kweli kwa kutumika lugha ya watu wengine, kwasababu lugha ni uchumi Na ukitaka kukuza lugha yako lazima ukuze uchumi na hatimaye lugha hukuza uchumi.

Mkosi ulipoanzia, kama asemavyo profesa Mbaabu (2007), kuchapishwa kwa Kitabu cha African Education (1953) pamoja na mkutano wa elimu ya kiafrika 1953, mkutano ambao uliripoti kuwa kuchapishwa kwa African education ni hatua mkubwa katika mabadiliko ya sera ya uingereza kuhusu elimu ya Africa hasa afrika mashariki.

Kitabu hicho kilipendekeza kwamba, kusomeshwa kwa kiswahili kukomeshwe kwa sababu ndicho kizuizi kikubwa dhidi ya maendeleo ya kingereza. Serikali ya uingereza ilikuwa tayari kuanzisha mabadiliko yeyote ambayo yangesaidia kukabiliana na mwamko wa uzalendo wa Mwafrika ambao uliyatishia mamlaka ya kikoloni kwa kupigania uhuru.

Kuondolewa kwa kiswahili kungepunguza uwezekano wa mawasiliano kati ya makabila na kungesaisia kuua mwamko na mtazami wa kitaifa kati ya RAIA.

Jambo hilo lingehakikisha kwamba uingereza ingeendelea kuathiri nchi hizo hata baada ya uhuru ( Mbaabu I.(2007) Historia ya usanifishaji wa kiswahili)

Hitimisho
Ni wakati sasa wa kuahamisha maarifa yaliyomo katika lugha nyingine na kuyahamisha katika lugha ya Kiswahili na kisha kujifunza maarifa hayo kwa lugha yetu kama walivyofanya kisumeri kwenda kiakadi 2350kk, na Kigiriki kwenda Kiingereza- Kijerumani-Kfaransa nk.
Kama sasa hivi watu wamesoma kwa kiingereza lakini wakitakiwa kuongea kiingereza wanaangusha maembe tu, itakuwaje watakaosomeshwa kwa kiswahili? Si wataporomosha matope kabisa?
Hoja zinazotolewa kuwa kama kiingereza ni kigumu tusome kwa kiswahili ni za kijinga, zimetokana na tafiti za wachumia tumbo wanaotafuta kazi za kutafsiri kiswahili, hakuna lolote la ziada la manufaa. kama hoja ni kuwa tusome kwa kiswahili kwa kuwa kiingereza ni kigumu, hatua itakayofuata ni kwamba tutaambiwa watu wa kanda ya ziwa wasome kwa kisukuma kwa kuwa kiswahili ni kigumu kwao (tunaona hata hotuba za kisiasa wanapewa kwa kisukuma). Mwishoni wote tutabakia washamba tu kwenye kakisiwa ketu hapa wakati wengine wanasonga mbele kwa maarifa kedekede yanayopatikana katika lugha ya kiingereza.
Hao wanaotaka watoto wa wenzao wasomeshwe kwa kiswahili wanasomesha watoto wao kwenye shule za English medium kuanzia nursery school! Danganyweni tu! Wenzenu wanataka muzidi kuwa mbumbumbu ili wazidi kuwatawala.
Binafsi sidanganyiki! Kiswahili nitakitumia kuongea, lakini suala la elimu ya wanangu lazima liwe kwenye lugha inayowapa exposure at a global scale. Tuwe wakweli.
 
Ujue mkuu hakuna anayekipuuza kiingereza wala kushindana nacho hata hizo nchi wanazofundishana kwa lugha zao haina maana kuwa wamekiepuka kabisa kiingereza,tatizo labda tunasahau kuwa kiingereza ni lugha kama zilivyo lugha zengine hivyo kufundishwa kwa kiswahili haizuii kujifunza kiingereza kama lugha.
 
Kwa maelezo haya bora tubaki na kiingereza.
Mambo ya kufundishwa kwa kiswahili ni kurudishana nyuma tu.
 
Kwa maelezo haya bora tubaki na kiingereza.
Mambo ya kufundishwa kwa kiswahili ni kurudishana nyuma tu.
Tunarudishana nyuma kwenye lipi?hii lugha ya kiingereza imetukalia kushoto wabongo pamoja na kufundishana kwa kiingereza bado hatuimudu vizuri.
 
Tunarudishana nyuma kwenye lipi?hii lugha ya kiingereza imetukalia kushoto wabongo pamoja na kufundishana kwa kiingereza bado hatuimudu vizuri.
Kwani kiswahili tunakimudu? Kwanini tunakwepa tatizo hatuchunguzi sababu halisi ya kushindwa masomo?
 
..kujua lugha mbalimbali siyo utumwa.

..kwa mfano, baba yangu anazungumza lugha ya kabila letu na lugha za makabila ya jirani. Je, yeye ni mtumwa?

..au alipojifunza Kiswahili ambayo siyo lugha yake ya asili, unaweza kumuita mtumwa?

..hoja yangu ni kwamba kama tunafundisha miaka 7 kwa kutumia Kiswahili basi wahitimu lazima wazungumze lugha hiyo kwa ufasaha.

..Na kama sekondari mpaka chuo kikuu ni Kiingereza basi waliohitimu ktk ngazi hizo lazima wazungumze Kiingereza fasaha.
Usiseme LAZIMA wajue, some people are just naturally bad in talking.
LAZIMA ni lugha za kidikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom