Pendekezo: Ingeundwa Wizara ya Dini ambayo ingesimamia mahusiano ya dini na siasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,768
141,632
Katika baadhi ya nchi kuna Wizara ya dini ambayo inaratibu mambo yote ya dini yanayohusiana moja kwa moja na siasa.

Viongozi wa dini wanaopendelea siasa kama akina askofu Bagonza, askofu Mwamakula, Shehe alhad Salum, askofu Gwajima nk nk hiyo ndio inakuwa forum yao ya kuongelea badala ya kuegemea Chadema au CCM.

Lowassa akiwa CCM aliahidi kuunda wizara ya dini endapo angechaguliwa kuwa Rais, nadhani aliona mbali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ni jambo ambalo kamwe halitowezekana.

Kwanza miongoni mwa wafuasi wa dini moja kuna mifarakano mikubwa ya kiimani sasa kama katika dini moja kuna hali hiyo utawezaje kuwaweka pamoja viongozi wa dini zenye imani tofauti na wakasikilizana???

Ili kulijenga taifa kiimani Kinachotakiwa ni kuandaa mitaala katika shule za msingi, mitaala itakayofundisha watoto "common morals" maadili.mema yanayokubaliiwa na dini zote, mfano, hakuna dini safi inayokubali: wizi, uzinifu, uongo, kusengenya, Ubadhirifu wa mali ya umma, ulevi, utii kwa viongozi katika mambo halali, kutetea nchi yako, kulinda amani, kutunza yatima na masikini, kupinga rushwa nk, hizi ndizo common marals ambazo viongozi wa dini wanahitaji wakae pamoja na wakubaliane na kitungwe kitabu kitakachofundishwa shuleni (primary). Hii ikiwa ni njia ya kuwafundisha watoto maadili ili wakikua wawe raia wema kwa nchi, na wazazi ndugu na jamii kwa ujumla.
 
Ni jambo ambalo kamwe halitowezekana.

Kwanza miongoni mwa wafuasi wa dini moja kuna mifarakano mikubwa ya kiimani sasa kama katika dini moja kuna hali hiyo utawezaje kuwaweka pamoja viongozi wa dini zenye imani tofauti na wakasikilizana?
Mbona kamati ya amani ina viongozi wa dini zote na wanaelewana vizuri tu!
 
Mbona kamati ya amani ina viongozi wa dini zote na wanaelewana vizuri tu!

Amani ni "common maral" ya dini zote ndiyo maana tunaona wanaelewana isitoshe hilo ni jambo moja tu, yakizidi mambo mengine ya imani za ndani (deep tenets) hapo shida zitatokea tu, mfano Wapo wanaosema Yesu ni mwana wa Mungu bali ni Mungu na wapo wanaosema Yesu ni mtume wa Mungu na kumwita Mungu ni Ushirikina na kufuru kubwa, 😒, katika hali kama hiyo unataraji watu hao wakae pamoja bila ya "Moto" kutokea???--- nani atawadhibiti kuzuia jazba zao na kwa muda gani???

Nadhani njia bora ndiyo hiyo niliyoisema kwamba zichukuliwe "common morals zote" zilizokubaliwa na wote kisha ziwekwe kwenye mtaala wa kuwafundisha watoto wote, na hii pia itawasaidia pakubwa haohao viongozi wa dini kuwalea waumini wao kwa urahisi kwani watakuwa tayari wamepata mafunzo ya msingi ya maadili ya kiroho toka walipokuwa primary schools.
 
Bwashee acha udini.....Serikali haina dini ila wananchi wake wana dini....Sasa inakuwaje serikali isiyo na dini ikaweka wizara ya dini?
Uko sahihi hapo itabidi katiba ya nchi ibadilishwe itamke wazo kuwa serikali ina dini ili ku justify kuundwa wizara ya dini

Nchi zenye dini moja hasa za kiislamu katiba zao hutamka wazi kuwa ni za kiislamu na zina hiyo wizara na hiyo wizara ina hadi askari wa dini na majaji wa dini ambao kazi zao ni kusimamia sheria za kiislamu mfano usipovaa hijabu mwanamke yaani unakamatwa na askari wa dini na kushughukikiwa ukikutwa unazini na but asiye mke au mume wa ndoa wanakukamata nk makosa ya kuvunja sharia za kiislamu mfano kula hadharani mwezi wa ramadhani nk utakumbana na askari wa dini na majaji wa dini
 
Katika baadhi ya nchi kuna Wizara ya dini ambayo inaratibu mambo yote ya dini yanayohusiana moja kwa moja na siasa.

Viongozi wa dini wanaopendelea siasa kama akina askofu Bagonza, askofu Mwamakula, Shehe alhad Salum, askofu Gwajima nk nk hiyo ndio inakuwa forum yao ya kuongelea badala ya kuegemea Chadema au CCM.

Lowassa akiwa CCM aliahidi kuunda wizara ya dini endapo angechaguliwa kuwa Rais, nadhani aliona mbali.

Maendeleo hayana vyama!
Misheard toka Waziri hadi maagizo wizara hii ilipwe na sadaka toka makanisani na swadhaka toka msikitini.
 
wizara ya dini yenye kusimamia masuala ya dini na siasa,panahitaji ufafanuzi zaidi hapo maana wengine wameingiza hadi tofauti za imani katika dini zetu kitu ambacho sidhani kama mleta mada amekusudia huko.
 
Mleta uzi ni mzee hivyo msamehe bure hata yeye hajui anaongelea nini hapa
 
Back
Top Bottom